Wanafunzi 5,000 Kujiunga na JKT:Maswali ya Kujiuliza...

Chipolopolo

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,425
725
Serikali kupitia wizara husika imetangaza mpango wa wanafunzi 5000 waliomaliza kidato sita kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria, kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya mpango huo kusitishwa. Lengo ni kuwajengea uzalendo, ukakamavu na mengineyo

Wanafunzi hao 5,000 ni kati ya 40,000 waliohitimu hivi karibuni.Kwa maana nyingine wameachwa wanafunzi 35,000. Iwapo hao 5,000 watajiunga na jeshi hilo, miongoni mwa 35,000 wenye matokeo mazuri wataendelea na masomo katika ngazi mbalimbali:Diploma, Shahada nk.

Moja ya maswali ya kujiuliza: Je, serikali haoni kama itakuwa imewaonea hao walioteuliwa kwenda kupiga kwata kwa takribani mwaka mzima wakati wenzao wakiendelea na masomo...?
 
Labda mi ndio sikuelewi,scenario ilotumika kuwagawa 5000 na hao 35000 ni ipi ndugu?ni kwamba hao 5000 ndio waliofaulu vizuri au anyway sijakupata vizuri hapo mtoa mada.
 
kama kweli itakuwa watangaziwe mapema kuwa utaenda jkt kukitokea hiki na kile. wanaoenda inabidi wapewe upendeleo fulan maana weng kwasasa wanaona huko sio. jkt ni nzuri kwangu lakin umakin unatakiwa kuiendesha. watakaolazimishwa kwenda wakat wengine hawaend nahis watajiskia vibaya.
 
Hao 5000 waliteuliwa kutoka katika shule mbalimbali nchini.Wahitimu wa kidato cha sita 2012 walikuwa takribani 40000, kati yao 5000 ndio walioteuliwa kujiunga na JKT
 
kama kweli itakuwa watangaziwe mapema kuwa utaenda jkt kukitokea hiki na kile. wanaoenda inabidi wapewe upendeleo fulan maana weng kwasasa wanaona huko sio. jkt ni nzuri kwangu lakin umakin unatakiwa kuiendesha. watakaolazimishwa kwenda wakat wengine hawaend nahis watajiskia vibaya.

Walioteuliwa wameshapewa taarifa.Wanajifahamu.
 
Labda mi ndio sikuelewi,scenario ilotumika kuwagawa 5000 na hao 35000 ni ipi ndugu?ni kwamba hao 5000 ndio waliofaulu vizuri au anyway sijakupata vizuri hapo mtoa mada.
kama sikosei kuna shule maalum zilizoteuliwa kwa kuanza zoezi,nadhani watakuwa wakiendelea kuongeza idadi ya shule kadri siku zinavyo kwenda!
 
kama sitaki kwenda inakuaje?kwani ni lazima?
Ni kwa mujibu wa sharia dogo, kama hutaki unaacha lakini upande wa pili ni kwamba huwezi kupata ajira serikalini au kwenye shirika lolote la umma unless una cheti chako cha JKT.....!!
 
Hao 35000 si watajiunga na JKT wakimaliza shule, Kama zamani hupati kazi mpaka upitie JKT! Nadhani hata wale ambao hawakupitia kabisa nao itabidi wapitie pia! HAKI SAWA KWA WOTE
 
Serikali bado haijajipanga kifedha. Ni gharama kubwa.Hao 35 000 itakuwa imetoka....
 
walioteuliwa kwenda huko waende na kondom za kutosha hasa wa kike maana kule kila kitu ni kutii amri ya kamanda
 
Serikali kupitia wizara husika imetangaza mpango wa wanafunzi 5000 waliomaliza kidato sita kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria, kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya mpango huo kusitishwa. Lengo ni kuwajengea uzalendo, ukakamavu na mengineyo

Wanafunzi hao 5,000 ni kati ya 40,000 waliohitimu hivi karibuni.Kwa maana nyingine wameachwa wanafunzi 35,000. Iwapo hao 5,000 watajiunga na jeshi hilo, miongoni mwa 35,000 wenye matokeo mazuri wataendelea na masomo katika ngazi mbalimbali:Diploma, Shahada nk.

Moja ya maswali ya kujiuliza: Je, serikali haoni kama itakuwa imewaonea hao walioteuliwa kwenda kupiga kwata kwa takribani mwaka mzima wakati wenzao wakiendelea na masomo...?

Mkumbuke kuwa CCM wana maana sana kuanzisha JK-T. Hapa hakuna lolote bali kutengeneza watu wa ZIDUMU FIKIRA ZA MWENYAKITI. NIkiangalia viongozi wengi wa TZ ambao hawaezi kuoji wakati mwingine wakiwa wanaonewa ni wale wote waliopitia JK-T.

Nch inakaribia kurudi kwenye zidumu fikira za mwenyekiti. Wameona jinsi vijana wanvyoleta shida kwenye vikao vingi sasa wanataka kuwadhibiti
 
Back
Top Bottom