Wanafunzi 426 Korogwe wapata daraja sifuri

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
BAADHI ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe zimegeuka viwanda vya kutengeneza daraja sifuri katika matokeo ya kidato cha nne kila mwaka. MTANZANIA Jumapili ilishuhudia Shule ya Sekondari Bungu ikifaulisha wanafunzi 426, ambao wamepata daraja sifuri katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Wakati Bungu ikitoa hizo, Shule ya Sekondari ya Kwashemshi imetoa wanafunzi wenye daraja sifuri wapatao 113 kwa miaka miwili, na Shule ya Sekondari Mlungui ikitoa wanafunzi 46 wenye daraja sifuri.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili wiki hii, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bungu, Dismas Kimweri, alisema kuwa mwaka 2011 wanafunzi 230 walihitimu kidato cha nne ambapo hakukuwa na daraja la kwanza na la pili, huku daraja la tatu waliopata ni wanafunzi 12, ambapo 86 walipata daraja la nne na 130 walipata daraja sifuri.

“Mwaka 2010, walihitimu wanafunzi 254 ambapo hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, la pili walikuwa 3, la tatu walikuwa 13, la nne walikuwa 90 na sifuri walikuwa 148...matokeo haya yanasababishwa na mambo mengi, ikiwemo uhaba wa walimu, hadi sasa nina walimu 12 na walimu watatu wako masomoni.

“Kwa sasa shule inachukua wanafunzi 640 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, kwa hiyo walimu wanazidiwa na mzigo mkubwa wa kufundisha kiasi cha kushindwa kukamilisha silabasi kwa wakati,” alisema Kimweri.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kwashemshi, Ezra Gweya, alisema uhaba wa walimu na utoro wa wanafunzi unachangia kupatikana kwa alama sifuri nyingi.

“Wanafunzi wengi ni watoro, wanakuja siku za mitihani na hii inatokana na kwamba jamii ya huku ni ya wakulima, kwa hiyo wanafunzi wanashirikishwa katika kilimo,” alisema Gweya.

Wakati walimu wakitoa utetezi huo, wanafunzi na wazazi katika maeneo hayo wamesema chanzo cha alama hizo ni uzembe wa walimu, kwa sababu wengi hawatimizi majukumu yao ya kufundisha.

“Hawa walimu waache kusingizia wanafunzi kwamba ni watoro au kwamba ni wachache, naamini kabisa wale walimu wachache wangekuwa wanatimiza wajibu wao ipasavyo hali hii isingekuwepo.

“Taarifa za Sekondari ya Bungu wakati inaanza, shule ilikuwa inafanya vizuri, lakini toka ameingia huyu mkuu aliyepo shule imekuwa na matokeo mabaya sana.

“Tatizo kubwa ni kwamba yeye mwenyewe hakai shuleni na hana muda wa kufuatilia walimu watimize majukumu yao, kwanza mimi nashangaa kwamba hadi sasa hivi anasubiri nini asiondolewe, tunaomba serikali ituangalie na sisi huku vijijini ili walimu wazembe kama hawa waondolewe mara moja,” alisema mmoja wa wazazi wa kata ya Bungu (jina tunalo).
 
Tatizo la walimu kutofundisha ni kubwa sana na linafumbiwa macho na wahusika. Inasikitisha sana kuona wanafunzi hasa katika shule za Kata wakikusanywa shuleni bila kuwapa maarifa yanayotakiwa. Shule za Kata zimefanywa kama vituo vya kulelea watoto kwani hakuna anayejali kama wamesoma au la. Kama hali hiyo haitarekebishwa shule hizo zitaendelea kuwa viwanda vya kuzalisha darala la sifuri
 
Mleta maada unatonesha kidonda watanzania, hakijapona!! ni tatizo la sehemu zote nchini! hakuna mwenye nafuu, wenye nafuu wanajikamua na kupeleka watoto wao shule nzuri kdg ambazo nazo ni kukariri bila kuelewa. Kwa kifupi shule nzuri nyingi ziko kibiashara zaidi, na shule mbaya ndo hivyo hakuna huduma nzuri kuanzia vyoo hadi walimu hakuna achilia mbali vifaa, vitabu, mazingira na hali ngumu za wananchi kuwahudumia vijana waweze kupata elimu nzuri.
 
Kwa hali ilivyo katika shule za kata haivumiliki hata kidodo. Wadau tufanyeje ili kunusuru taifa letu kuwa kisiwa cha mambumbu kwa miaka ijayo. Viongozi wanapeleka watoto wao nje au kwenye shule zenye gharama kubwa, nani atawakomboa watanzania wanyonge?
 
Hiyo Bungu ina afadhali kidogo zipo zingine kama Msiga Dindira Kwashemshi yupo mwl. ni dereva bodaboda hana muda wa kufundisha .Hakuna wakaguzi wanatembelea huko . Hazina bodi imara za shule na wananchi wengi hawana mwamko wa elimu .
 
Mbunge wao si ni yule Profesa Maji Marefu aliyemchanja Chale Mbunge mwenzake Lusinde kwenye Makalio?

Sasa Profesa mzima anashindwa kuwasaisia wananchi wake wasiwe Viwanda vya Mayai?

Korogwe bana, sasa mmekuwa Kuku wa kutotoa Zero nyie?

403882938.jpg


http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mbunge-mganga-wa-kienyeji
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom