Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 3
WANAFUNZI wapatao 400 wa Chuo cha Uhasibu Arusha wako hatarini kufukuzwa masomo baada ya Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, kuwathibitishia kuwa hawawezi kupata mkopo wa Bodi ya Mikopo, kwa vile hawana sifa.
Juzi wanafunzi hao walikwenda Dodoma kuonana na Waziri Peter Msolla ambaye aliwaeleza hana uwezo wa kutengua uamuzi uliokwisha kufanywa na mamlaka za juu.
Wanafunzi hao walikwenda kuanza masomo baada ya majina yao kuorodheshwa kwenye tovuti ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuonyesha kuwa baada ya kufanyiwa tathmini ya uwezo wa uchumi watapewa mkopo na kutajwa asilimia wanayostahili kupewa.
Lakini baada ya kufika chuoni na kuanza kufuatilia mkopo huo, Bodi iliwaeleza kuwa ingawa wamefanyiwa tathmini ya uwezo wao wa uchumi, hawawezi kukopeshwa kutokana na kutokuwa na sifa. Moja ya vigezo ni kutokuwa na alama ya daraja la kwanza au la pili, wengi wao wana daraja la tatu katika mtihani wa kidato cha sita.
Baada ya kutoridhika na majibu hayo ya bodi, wanafunzi hao walituma wawakilishi wapatao 76 kwenda kwa Waziri Msolla aone namna ambavyo anaweza kuwasaidia. Lakini majibu ya waziri huyo jana yanaonyesha kuwakatisha tamaa wanafunzi hao.
Akizungumza jana, Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Erick Gabriel, alithibitisha kuwa Profesa Msolla aliwaambia kuwa bajeti iliyopo haikidhi kuwakopesha wanafunzi waliopata daraja la tatu badala yake aliwaambia kuwa wenye sifa ni wale waliopata daraja kuanzia la pili.
Tulimwomba atusaidie ili wanafunzi hawa wasifukuzwe masomo, lakini amesema hana uwezo huo, kwa vile tayari serikali imepitisha sera hiyo, alisema Gabriel.
Kutokana na hali hiyo, Gabriel alisema wanamwomba Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Rais Jakaya Kikwete waingilie kati suala hilo, waone namna ambavyo watawasaidia wanafunzi hao ili wasifukuzwe masomo yao.
Alisema wanafunzi hao hawakufanya makusudi, bali tangazo la kwenye tovuti ndilo lililowapa matumaini na hivyo wakaona kuwa wamebahatika kupata mkopo huo. Alisema wengi wa wanafunzi hao wametoka mikoani na wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.
Gabriel alisema kutokana na utata uliojitokeza, Profesa Msolla aliahidi kuwa katika mwaka ujao watahakikisha usumbufu wa namna hiyo haujitokezi.
Kwa mujibu wa taratibu za Bodi ya Mikopo, wanafunzi ambao wana sifa za kupewa mkopo bila kujali madaraja yao ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na fani nyingine za sayansi.
Lengo la kutoa ahueni kwa watu wanaosomea fani hizo ni kuhamasisha wanafunzi zaidi ili fani hizo zenye upungufu wa wataalamu ziweze kukidhi mahitaji yaliyopo.
Lakini wanafunzi wengine wanaosoma fani za sanaa, sheria, uhasibu watapewa mkopo huo tu kama