Wanafunzi 400 uhasibu wakwama kwa Msolla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 400 uhasibu wakwama kwa Msolla

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Zee la shamba, Nov 15, 2007.

 1. Zee la shamba

  Zee la shamba Member

  #1
  Nov 15, 2007
  Joined: Oct 17, 2007
  Messages: 55
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  WANAFUNZI wapatao 400 wa Chuo cha Uhasibu Arusha wako hatarini kufukuzwa masomo baada ya Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, kuwathibitishia kuwa hawawezi kupata mkopo wa Bodi ya Mikopo, kwa vile hawana sifa.


  Juzi wanafunzi hao walikwenda Dodoma kuonana na Waziri Peter Msolla ambaye aliwaeleza hana uwezo wa kutengua uamuzi uliokwisha kufanywa na mamlaka za juu.


  Wanafunzi hao walikwenda kuanza masomo baada ya majina yao kuorodheshwa kwenye tovuti ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuonyesha kuwa baada ya kufanyiwa tathmini ya uwezo wa uchumi watapewa mkopo na kutajwa asilimia wanayostahili kupewa.


  Lakini baada ya kufika chuoni na kuanza kufuatilia mkopo huo, Bodi iliwaeleza kuwa ingawa wamefanyiwa tathmini ya uwezo wao wa uchumi, hawawezi kukopeshwa kutokana na kutokuwa na sifa. Moja ya vigezo ni kutokuwa na alama ya daraja la kwanza au la pili, wengi wao wana daraja la tatu katika mtihani wa kidato cha sita.


  Baada ya kutoridhika na majibu hayo ya bodi, wanafunzi hao walituma wawakilishi wapatao 76 kwenda kwa Waziri Msolla aone namna ambavyo anaweza kuwasaidia. Lakini majibu ya waziri huyo jana yanaonyesha kuwakatisha tamaa wanafunzi hao.


  Akizungumza jana, Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Erick Gabriel, alithibitisha kuwa Profesa Msolla aliwaambia kuwa bajeti iliyopo haikidhi kuwakopesha wanafunzi waliopata daraja la tatu badala yake aliwaambia kuwa wenye sifa ni wale waliopata daraja kuanzia la pili.


  “Tulimwomba atusaidie ili wanafunzi hawa wasifukuzwe masomo, lakini amesema hana uwezo huo, kwa vile tayari serikali imepitisha sera hiyo,” alisema Gabriel.


  Kutokana na hali hiyo, Gabriel alisema wanamwomba Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Rais Jakaya Kikwete waingilie kati suala hilo, waone namna ambavyo watawasaidia wanafunzi hao ili wasifukuzwe masomo yao.


  Alisema wanafunzi hao hawakufanya makusudi, bali tangazo la kwenye tovuti ndilo lililowapa matumaini na hivyo wakaona kuwa wamebahatika kupata mkopo huo. Alisema wengi wa wanafunzi hao wametoka mikoani na wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.


  Gabriel alisema kutokana na utata uliojitokeza, Profesa Msolla aliahidi kuwa katika mwaka ujao watahakikisha usumbufu wa namna hiyo haujitokezi.


  Kwa mujibu wa taratibu za Bodi ya Mikopo, wanafunzi ambao wana sifa za kupewa mkopo bila kujali madaraja yao ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na fani nyingine za sayansi.


  Lengo la kutoa ahueni kwa watu wanaosomea fani hizo ni kuhamasisha wanafunzi zaidi ili fani hizo zenye upungufu wa wataalamu ziweze kukidhi mahitaji yaliyopo.


  Lakini wanafunzi wengine wanaosoma fani za sanaa, sheria, uhasibu watapewa mkopo huo tu kama
   
 2. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Msola Must go Out,Anshindwa vipi kumshauri RAis Apunguze Safari ili pesa wapewe Wanafunzi hawa ?
  Mie nawashauri hawa wanafunzi waandamane na Mabango leo wakati waziri wa Fedha wa Marekani atakopokuwa Arusha,wamueleze usumbufu wanaoupata kutoka kwa serikali wakitaka pesa za mikopo huku zinatolewa na wahisani. anaweza kumuuliza Muungwana kwanini hajawapa pesa,Mie najua Msola ndio anamalizia kazi,
  Plan B,Najua huyu waziri ataendelea kuwapo mpaka kesho,Nawashauri hawa wanafunzi wafanye utaratibu wa kumuona.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 15, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,379
  Trophy Points: 280
  sheria hiyo ya bodi ya mikopo ni kinyume cha Katiba. Katika Ibara ya 13:2 Katiba inasema:

  Sasa hiyo inaweza kueleweka vizuri ukisoma na kipengele kifuatacho cha Katiba:

  Ibara 11:
  (2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia
  atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia
  upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.
  (3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu
  wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata
  elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo
  vinginevyo vya mafunzo.


  sasa ni nani huyo aliyekuja na wazo la kusema kuwa ukiwa na daraja la tatu basi hustahili elimu na sheria ikubague?
   
 4. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mkjj,
  hilijambo tumelijadili sana bila mafanikio,na kama katiba ndio inasema hivyo kwa nini hivi vyama vya wanafunzi wasifungue kesi mahakamani ilikudai haki yao ya kikatiba.
  Mnyika uko wapi kuhamasisha ilisuala liwezekupatiwa ufumbuzi.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 15, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,379
  Trophy Points: 280
  Katibu Tarafa.. sikiliza kwa makini kutokea kwenye kongamano la vijana wikiend hii..
   
 6. M

  Manyiri Member

  #6
  Nov 18, 2007
  Joined: Oct 27, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hapo Uhasibu Kuna Watu Wanasoma Advanced Diploma Za Computer Science Na Information Tecknology Na Wao Bado Hawajapata Fedha Yoyote Toka Bodi Japokuwa Bodi Ilisema Ndo Vipaumbele Katika Fani Za Sayansi Na Teknolojia Vile Vile Watu Wa Mwaka Wa Pilim Bodi Iliwatangazia Kutuma Maombi Ya Kuomba Mkopo Ikiwa Ni Pamoja Na Kulipia Fomu Ya Loan Board Tsh10000 Wengi Wakiwa Ni Wanaosoma It Na Computer Science Lakini Mpaka Sasa Hawajapata Pesa Yoyote Japokuwa Wanasoma Kprogram Ambazo Zimo Katika Vipaumbele
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2016
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,463
  Trophy Points: 280
  Haya majanga yalianzishwa na ile Timu yetu ya Boyz Two Men
   
 8. nusuhela

  nusuhela JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2016
  Joined: Jan 26, 2014
  Messages: 2,640
  Likes Received: 2,120
  Trophy Points: 280
  Hapa kazi tu. Nadhani namba tunaisoma
   
 9. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2016
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mambo ya 2007 yanarudia 2016.
   
 10. Quarterpin

  Quarterpin JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2016
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 1,257
  Likes Received: 925
  Trophy Points: 280
  Nahitaji kufahamu kama huu uzalendo bado upo.
   
Loading...