Wanafunzi zaidi ya 31000 kukosa mikopo ya elimu ya juu 2017/2018

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Tanzania ya viwonder

WANAFUNZI 31,000 KUKOSA MIKOPO ELIMU YA JUU
download-5-4.jpg


Na LEONARD MANG’OHA -DAR ES SALAAM

WANAFUNZI zaidi ya 61,000 wamewasilisha maombi ya mikopo katika Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa mwaka mpya wa masomo wa 2017/2018, unaotarajiwa kuanza Oktoba, mwaka huu, huku idadi kamili ya wanaotakiwa kupewa ni 30,000.

Pia kati ya hao, waliowasilisha maombi yaliyokamilika ni wanafunzi 43,811, huku 11,200 taarifa zao zilibainika kuwa na kasoro na upungufu mbalimbali.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kwa njia ya simu hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razak Badru, alisema wanafunzi hao ni wale waliofanikiwa kuomba katika muda uliofikia ukomo Agosti 11, mwaka huu.

“Hawa tunaweza kusema ni incomplete kwa sababu wako ambao wamekosa baadhi ya nyaraka kama vile vyeti vya kuzaliwa au taarifa za wazazi,” alisema.

Pamoja na kuwapo kwa kasoro hizo, alisema wale wote walioomba katika muda maalumu uliopangwa watapata fursa ya kusahihisha taarifa zao.

Alisema kwa sasa wanaendelea kufanya uchambuzi wa taarifa za waombaji ili kubaini walio na sifa za kupewa mikopo na baada ya kukamilika kwa uchambuzi huo watatoa majina ya wale waliopitishwa kupata mikopo hiyo na kuanza kuwapangia mikopo yao.

“Kwa mujibu wa kalenda yetu ambayo ndiyo inayotuongoza, inaonyesha kuwa, hadi kufikia Oktoba 10, mwaka huu, taratibu zote za uchambuzi na kutangazwa kwa majina ya wale walio na sifa ya kupata mikopo inatakiwa kuwa imekamilika na tayari wanafunzi waanze kupelekewa mikopo hiyo vyuoni kwao,” alisema.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole, alisema wataangalia vigezo mbalimbali kwa wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kupewa mikopo hiyo.

Alivitaja baadhi ya vigezo hivyo kuwa ni kwa wanafunzi waliopata nafasi katika vyuo vikuu, wawe raia wa Tanzania, wawe wamemaliza kidato cha sita si kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita na vingine vyote vilivyoelekezwa na HESLB.

Chanzo: Mtanzania
 
Nchi inanyooshwa sijui na pasi ya mkaa au ya umeme! lakini naona ni sura za majanga tu kila kona nchini. 31,000 ndoto zao kielimu ndiyo zimefikia ukingoni na asilimia kubwa ya hawa ni kutoka familia za kimaskini ambazo hazina uwezo wa kuwalipia elimu ya juu. Utasikia wataambiwa mjiajiri!

Dah!!!! 31,000!!!!!!

Ndo Tanzania yetu ilipofikia, naamini tumejifunza sasa!!!
 
Sana Mkuu, halafu hakuna yeyote Serikalini atatia neno. Watauchuna kimya kama haliwahusu! Mimi ni mtetezi wa wanyonge! Sijui wanyonge wapi wanaotajwa hapa.
Nasikia huyu dhalimu akiwa kule Arusha wakati anawavisha wanajeshi Nishan, amesema alisukumiziwa Urais maana yeye alikuwa anajaribu tu kwa kuchukua form.

Bora akubali tumkosoe maisha yasonge mbele, maana lori lake tochi zote zimeng'ooka halafu anaendelea kulisukumiza hivyo hivyo kuelekea shimoni
 
Alidhani Urais ni lelemama! Hutaki kukosolewa kaa pembeni waachie ambao wako tayari kukosolewa bila kuamuru watu wasiojulikana na SMG zao wawanyamazishe au kuwateka na kuwatesa wanaowakosoa.

Nasikia huyu dhalimu akiwa kule Arusha wakati anawavisha wanajeshi Nishan, amesema alisukumiziwa Urais maana yeye alikuwa anajaribu tu kwa kuchukua form.

Bora akubali tumkosoe maisha yasonge mbele, maana lori lake tochi zote zimeng'ooka halafu anaendelea kulisukumiza hivyo hivyo kuelekea shimoni
 
Back
Top Bottom