Wanafunzi 27 udom wasimamishwa masomo kwa muda usiojulikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 27 udom wasimamishwa masomo kwa muda usiojulikana

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mpiganiahaki, Apr 28, 2011.

 1. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wanafunzi wa UDOM kitivo cha Teknolojia ya mawasiliano na Elimu Angavu(College of Informatics&Virtual Education) tunaendelea na mgomo wa kutoingia darasani ili kushinikiza Utawala kuwarudisha wenzetu 27 waliosimamishwa masomo kurudishwa chuoni.

  Msimamo huu ulianza tokea Alhamis ya wiki iliyopita baada ya wanafunzi wenzetu wapatao 10 kusimamishwa masomo kwa madai kuwa ndio waliokuwa vinara wa maandamano tuliyofanya jana yake Jumatano hadi Ofisi ya W/Mkuu kuhitaji kutimiziwa mahitaji yetu ya muda mrefu,ambayo W/Mkuu Pinda aliahidi kututimizia alipokuja chuoni kwetu Tar.15 Jan. 2011.

  Sisi wana-informatics dai letu kuu lilikuwa kupatiwa mahitaji yetu muhimu ya kitivo(Special Facult Requirement),dai ambalo halijawahi kutimizwa toka kuanzishwa kwa college hii mwaka 2007.

  Ndipo Jumatano ya wiki iliyopita wanafunzi wote wa college hii tukaamua kuandamana hadi Ofisi ya W/Mkuu iliyoko Dodoma Mjini ili kufaham hatma ya madai yetu.Tulipofika ofisini kwake tulipewa majibu ambayo tuliridhika nayo kuwa madai yetu bado yanashughulikiwa na hadi kufikia tar. 6 May 2011 madai yetu yatakuwa yameshashughulikiwa.


  Cha kushangaza siku iliyofuata ambayo ilikuwa Alhamis,yalibandikwa majina ya wanafunzi 10 ambao walihitajika utawala na walipofika walipewa barua za kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana kwa madai kuwa ndio vinara wa maandamano tuliyofanya jana yake J'5 na walitolewa nje ya chuo kwa ulinzi mkali wa Polisi.


  Siku hiyo hiyo wanafunzi wa college hii tuliandamana hadi utawala tukishinikizwa wenzetu warudishwe na pia tukaweka azimio la kutoingia darasani hadi hapo wenzetu 10 watakapo rudishwa chuoni.


  Msimamo huo wa kutoingia darasani ndipo ukaanza leo Jumatano tar.27 kutokana na mfululizo wa sikukuu toka siku tuliyoweka azimio la kutoingia madarasani.


  Katika hali iliyotushangaza wengi,leo Jumatano wakati tukiwa katika mgomo wa kutoingia madarsani,tukaletewa tena list ya wanafunzi wengine 17 ambao utawala imewaona kuwa ndio vinara wa migomo na kuwakabidhi barua za kuwasimamisha masomo;

  Hivyo kufanya idadi ya waliosimamishwa masomo kufikia 27.

  Napenda kusema kwa niaba ya wana-informatics wenzangu kuwa,tunaipenda na kuitakia mema sana college yetu ,chuo chetu na Nchi yetu kwa ujumla.Lakini njia hii utawala wanayotumia haitakwenda kusaidi kabisa, bali inakwenda kusababisha matatizo makubwa zaidi na zaidi.

  Naomba kuweka wazi jambo hili,College yetu ya Iformatics ndiyo College pekee ya UDOM ambayo ilikuwa haijawahi kufanya maandamano yoyote wala mgomo wowote toka ianzishwe na hii inatokana na viongozi wetu ambao walikuwa wakitupa matumaini na kutuongezea moyo wa subira,hivyo kutufanya kuendelea kuwa wavumilivu.

  Ila sisi kama wana-informatics tunajiuliza toka college nyingine zifanye maandamano&migomo hatujawahi kusikia kuna hata mwanafunzi mmoja kasimamishwa masomo,lakini sisi tuliofanya peaceful demonstration kwa mara ya kwanza wenzetu 27 wanasimamishwa masomo katika college ya wanafunzi 1200!


  Pia wana JF najiuliza, semester iliyopita wahadhiri wa UDOM walifanya mgomo wa kutofundisha kwa muda wa wiki moja wakati walipokuwa wanapigania maslahi yao, lakini hakuna aliyefukuzwa wala kusimamishwa kazi.

  Iwaje sisi wana-informatics tunaopigania maslahi yetu,ambayo utawala umeshindwa kuyafuatilia tangu kuanzishwa kwa college hii mwaka 2007,wenzentu wasimamishwe masomo?


  Tunasema hatutaacha kuedelea na mgomo wetu wa kutoingia darasani na hatutishiwi na staili ya utawala kutusimamisha masomo, na kama hawawezi kuwarudisha wenzetu wote 27 basi tufukuzeni wote!


  Mwisho, wana-informatics tunatoa wito kwa college nyingine zote za UDOM kama Education, Social Science, Humanity na nyinginezo kutuunga mkono katika mgomo huu ili kuweza kuishinda dhuluma hii tunayofanyiwa na utawala.
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  jitahidiNI kuwa kama COET aka FOE WANAUME WAKAZI HAKIKISHENI WENZENU WANARUDI NA HAKI ZENU MNAPATA NIMEKAA MLIMANI 4YRS NA MIGOMO NDIO INFINITY SOLUTION YA CRITICAL PROBLEMS KAMA HIZO .YOUR INTELLECTUAL NAJUA HAMJAKULUPUKA MTASHIDA PAMOJA PAMBANO YA KIANZA NI NON STOP MPAKA USHINDI NA NI LAZIMA PANAPO HAKI YENU
   
 3. m

  mkulimamwema Senior Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini vijana wa UDOM mnaturudisha nyuma wapambanaji wenzenu katika vyuo vyote ninyi peke yenu ndio mlimchangia pesa JK agombee urais mkasema slaa mpotoshaji hayo tuache cha kufanya vyuo vyote Tanzania tufanye badiliko la kweli la kuiondoa ccm 2015 maana kila uchaguzi tunanyimwa haki ya kupiga kura "JAMANI INATOSHA TUMWONDOE ANAYETUNYANYASA"
   
 4. Joyum

  Joyum Senior Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hawa si ndo kipenzi cha CCM na sasa inakuaje! au nao wanatakiwa wajivue magamaba nini...(kidding).
  Kazeni buti mpate haki yenu,
  kila lakheri
   
 5. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Poleni sana watu wangu!
  Hatimaye chuo chao kimefungwa na wanafunzi wote wameambiwa warudi makwao!
  Ila cha kushangaza hao wanafunzi 10 wa mwanzo kufukuzwa chanzo kilikuwa na video clip ndicho kilicho wabaini wale waliokuwepo mbele. Swali je uongozi wa chuo ulipata wapi iyo video clip? je ni nani aliyechukua iyo video kwani hakukuwa na mtu aliyekuwa akichukua iyo clip?
  Wana JF hawa ndugu zetu hawakutendewa haki.
  Mbaya zaidi baada ya hao kutangaza wanaendelea na mgomo na kuomba vitivo vingine viwaunge mkono ila Prof. Kikula alikutana na raisi wa kitivo cha sayansi na jamii maeneo ya mjini nje ya chuo, Je kulikuwa na agenda gani kwati ya hao?
  Wana JF haki haiombwi ila inatafutwa kwa kuwa kama unauwakika na unachokidai na daima uwoga ndio adui wa maendeleo.
   
 6. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Acha wakapumzike. Wakirudi watakuwa na akili ya kusoma kwani kila siku migomo tu.
   
 7. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kipindi college zingine zilipokuwa zikigoma zilipoomba support yenu mlijifanya mpo bize na kitabu. Haya sasa chuo kimefungwa ludini mkapumzike sawa!
   
Loading...