Wanafunzi 234 waliofaulu darasa saba wahawajui kusoma, kuandika!

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Na Jimmy Mfuru
20th March 2012







Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo


Wanafunzi 234 kati ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Mbeya hawajui kusoma wala kuandika.

Akizungumza na NIPASHE jana ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema wanafunzi hao wamegundulika baada ya kufanyiwa mtihani wa majaribio.

Alisema aliagiza maofisa elimu nchini kuhakikisha wanafunzi wanaojiunga na shule zote za sekondari wanafanya mtihani wa majaribio. Mitihani huo ulifanyika kuanzia Februari 28, mwaka huu, baada ya kubaini kuwapo udanyanyifu.

Alisema Mkoa wa Mbeya hadi jana ndio walianza kutuma taarifa za mitihani hiyo wizarani na kwamba anasubiri mikoa mingine kutuma. Alisema wakishapata mikoa hiyo wanafunzi watarudishwa nyumbani.

Alisema wizara imeunda tume ya kutembelea shule zote nchini, kuanzia Aprili Mosi ili kutafuta ukubwa wa tatizo hilo kisha watakaa kama kamati kulijadili na kwamba, walimu watakaobainika walihusika katika udanganyifu huo wa mitihani watawajibishwa.

Mwaka jana katika mtihani wa kumaliza darasa la saba, kulikuwapo na udanganyifu mkubwa katika mitihani na kufanya wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kujikuta hawajui kusoma wala kuandika.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka jana, ni 43,240 wavulana wakiwa 21,104 na wasichana 22,104.



CHANZO: NIPASHE
 
Yani tuna hasara na uongozi wowote wa serikali tawala!

Ila tumegundua ya kwmb wanachotaka kwa wazazi wa hawa watoto hao ni pesa tu!

1.ADA.
2.PESA YA DAWATI
3.PESA YA TAHADHARI
4.,,,,,,kwa ujumla ni wezi ful!
 
Hali ni mbaya sana tena sana.
Binafsi nilipata bahati ya kutembelea shule moja wakati mitihani hii ikifanyika, ni aibu. Mtoto tunayeambiwa amefaulu hajui hata kuandika jina lake.
Nawalaumu sana walimu hasa wa shule za msingi kwani wanachoandaa ni taifa la vilaza na ambao hawataweza kuwa washindani katika dunia hii ya utandawazi.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom