Wanafunzi 18000 wa kidato cha 3 hawajui kusoma na kuandika-nani alaumiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 18000 wa kidato cha 3 hawajui kusoma na kuandika-nani alaumiwe?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by engmtolera, Dec 13, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Haya wadau
  mkoa wa pwani unawanafunzi zaidi ya elfu 18 wa shule ya msingi na sekondary wa kidato cha 3,hawajui kusoma na kuandika je
  nani wakulaumiwa hapo?

  kwa upande wangu mimi nailaumu serikali kwani nimekuwa mwalimu wa fizikia na hisabati huko malinyi ulanga,nimekumbana na matatizo mengi sana na haya yote yanasababisha na sera mbovu zilizowekwa na kulazimishwa ziwepo ktk elimu yetu,

  1. tunalazimisha wanafunzi wote waliomaliza darasa la saba wajiunge na sekondary hata kama mwanafunzi huyo hajui kusoma wala kuandika
  na shule zinazofelisha mala nyingi zimekuwa zikipewa adhabu.

  2.Kuondoa adhabu za viboko kwa wanafunzi kiasi kwamba mwanafunzi yupo huru kufanya lolote lile atakalo, mliopo nje ya system ya ualimu hamuoni tatizo lakini tuliokuwepo humo hili ni tatizo kubwa sana,

  3.Serikali imeondoa mitihani ya kidato cha pili na hata kama ipo mwanafunzi haruhusiwi kurudia darasa hata kama akiferi,hii imeondoa nguvu ya wanafunzi kusoma na wanafanya bora liende tu wamalize kidato cha nne

  4.Pia serikali imeondoa mtihani wa darasa la nne kama ulivyokuwa zamani huu wa sasa hata ukiferi ni lazima usonge mbele

  5.Ktk shule za kata mamlaka yapo chini ya kata husika kiasi kwamba inakuwa ni vigumu kwa viongozi wa kata kufuatilia maendleo ya shule husika kutokana na viongozi hao kuwa na upeo tofauti wa uelewa kuhusu elimu na kutingwa na mambo mengi nje ya kusimamia shule za kata

  6. Maslahi ya walimu kutokutiliwa mkazo na kuwafanya walimu hao kuona kuwa ualimu ni kazi yakitumwa zaidi ukilinganisha na kzi nyingine

  Yapo mengi sana matatizo yanayopelekea tuwe na idadi kubwa ya wasiojua kusoma na kuandika kubwa zaidi ni

  kutaka kuwaonyesha wananchi na watoa misaada kuwa tumeweza kuingiza wanafunzi wengi shule ya msingi,wote wamefauru kwenda sekondari na wote wamemaliza sekondari,pasipo kuangalia mwisho wa siku tunazalisha wasomi watakao kuja kuididimiza nchi hii na kuimaliza kabisa
   
 2. MWL MTZ

  MWL MTZ Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba walimu wapo kwenye mgomo siku nyingi sanaaa. ndo mana wanafunzi wengi hawajui kusoma. usione wanakwenda kazini lakini hawafundishi kabisa sababu ni mishahara midogo na malimbikizo ma madai yao. habari kamili uliza cwt.
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  sikubaliani na hili,kwani tatizo hili la kupata wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika imeanza tu baada ya kuondoa mitihani ya Darasa la nne,na kuingiza sera za kuandikisha wanafunzi wengi kwa mkupuo kwa lengo la kuwa na wanafunzi wengi wanaomaliza Darasa la saba na kuingia Sekondari

  walimu wamekuwa na moyo sana wa kufundisha ingawaje wanamatatizo mengi moja wapo likiwa hilo ulilolitaja

  sera mbovu ktk elimu yetu bado ni tatizo mkuu
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  Engineer!

  Mtihani wa Darasa la nne umeondolewa mwaka gani?

  Mimi nakubaliana na MWL MTZ - Walimu wa shule za Serikali walishaacha kufundisha zaidi ya miaka 6 iliyopita! Walimu (kwenye shule za umma) hawafundishi bali uenda ku-sign na kusoma magazeti na kupiga soga... Halafu siku za mwisho wa wiki wanafundisha "tuition" wanafunzi wale wale ambao wamekuwa nao juma zima!

  Tuition inalipiwa sh 200-500 kwa kila mwanafunzi ... then ... wanafunzi wakifanya mazoezi baada ya tuition ... walimu wanawaambia wasahishane wenyewe!

  Katika sector ya Elimu (Msingi & Secondary) kumekufa kabisa wanasubiri kuanua matanga!
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Yaani huelewi kuwa mtihani wa sasa wa Darasa la nne upo tofauti na ule tuliofannya sisi zamani? hujui kuwa mwanafunzi wa darasa nne akiferi sasa hivi anaruhusiwa kuendelea na darasa la tano?
  fikilia kuwa kijana huyo kapitishwa bila kupingwa kuendelea na darasa la 5 unategemea nini mbele ya safari,ukizingatia tena wanafunzi wote wanatakiwa kupita bila kupingwa kuingia sekondari na elewa kuwa mtuhani wa kidato cha pili haumzuii mwanafunzi kurudia darasa,kwa hiyo ulemwendelezo wa kumpata kujana asiyejua kusoma na kuandika unaendelea hadi amalizapo kidato cha nne
   
 6. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Shukrani kwa serikali ya awamu ya 4, imeweza kujenga shule kilakata na sasa kila mwanafunzi anakwenda shule, au mnataka nini zaidi?! Kwani sisi watanzania shida yetu si shule bwana! Haya mambo ya kufaulu na kujua kusoma ni anasa tu.

  Hata hili la mchakato wa katiba nalo lipo hivyo hivyo. Sisi shida yetu ni kutoa maoni tu. Kama yatafanyiwa kazi au kuwekwa tu si shida yetu. Ndio maana hata hotuba ya Mh. Dokta alipoongea na wacheza bao wa dar ilitosha kumaliza kiu yetu. Mkumbuke Mh. Dokta alisema wote tutatoa maoni, sasa kazi kwenu mnaotaka maoni yenu yafanyiwe kazi.

  Juzi waziri alikuwa anajisifia kuwa ni Tanzania pekee ndio imefanikiwa kupeleka sekondari 80% ya wahitimu wa darasa la saba. Nichukue nafasi hii kutoa pongezi kwa Mh. Dokta na serikali yake kwa kukuza idadi ya wahitimu.
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160

  Engineer,

  Nadhani sikuelewi!

  Kwanza, Mimi sijawahi kuafanya mtihani wa darasa la nne - nilianza darasa la kwanza najua kusoma na kuandika mwaka 1975 - hatukuwa na mtihani wa Darasa la nne!

  Pili, Kujua kusoma na kuandika haitegemei mtoto amefanya mitihani mingapi bali inategemea mtoto amefundishwa na kufahamu, hata kama hajawahi kufanya mtihani - nadhani unakumbuka Elimu ya Watu Wazima kwenye miaka ya 70-80 - hawa hawakuwa na mitihani bali walifundishwa na kufahamu kusoma na kuandika ...

  The bottom line is - Siku hizi watoto hawafundishwi (kwa sababu walimu hawapendi kufundisha), on top of that walimu wengi ni wale waliopata "credit" za chini katika masomo ya O- or High- Level!
   
 8. MWL MTZ

  MWL MTZ Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
Loading...