Wanafamilia 3 wakamatwa kwa mauaji Micheweni, RPC aingilia kati

G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
64
125
WATU watatu wa familia moja akiwemo Baba,Mama na Mtoto wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa tuhuma za mauwaji ya Mohamed Omar Salim (45).

Wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi ni Mwanaarabu Khamis Abdalla (32), Nassor Said Nassor (38) na Khamis Nassor Said (14) wote ni wakazi wa Shehia ya Msuka Magharibi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ,Kamishina Msaidizi Juma Sadi Khamis akizungumza Ofisini kwake amesema chanzo cha mauwaji hayo ni ugomvi uliosababishwa na watoto.

Aidha Kamanda Sadi amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi mwao bali wafuate utaratibu wa sheria.

Tayari mwili wa marehemu Mohamed Omar Salim umekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi na daktari wa serikali.
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
4,769
2,000
Hizi tabia za kujichukulia sheria mikononi zinatutesa sana wa TZ. Jamii haipo tayari kubadilika kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom