Wanachuo watatu wafa maji Kigamboni

Small Boy

Senior Member
Jul 12, 2007
142
38
Wanafunzi 3 wa chuo kikuu Muhimbili wamekufa maji jana jioni wakati wakiogelea kwenye ufukwe wa Geza Ulole huko KIgamboni.

Wanafunzi hao ni:
Issa Kennedy MD mwaka wa nne
Khatibu Mzee MD mwaka wa pili
Abdalah omary Msangi MD mwak wa pili
Wote ni wanafunzi wa udaktari na kwa mujibu wa taarifa toka chuoni hapo, wanafunzi wawili, ndio waliozama kwanza na ndipo Isaa akaamua kwenda kuwaokoa wenzake bila mafanikio hali iliyopelekea mauti ya wote watatu.

Tayari mmoja wa marehemu amesafirishwa kwenda Zanzibar kwa maziko nyumbani kwake, mwingine atasafirishwa jioni ya leo kwenda Mwanga kwa maziko na aliyebakia atazikwa hapa Dar
 
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea..., Mwenyezi Mungu awalaze pema.
 
RIP wanafunzi wa muhimbili.

Ila hapa lazima tujifunze kidogo kuhusu fukwe zetu, ina maana kuna sehemu zina kina kirefu zaidi na kusababisha watu kuzama kama wanatumbukia kisimani ilikuwa vipi. Ufanywe utafiti na wataalam wetu ili kujua ni fukwe gani salama kwa kuogelea na zipi hatari, maana miaka michache iliyopita kuna mwanafunzi wa hapo hapo muhimbili aliliwa na papa.
 
Poleni sana wafiwa, ni wakati sasa kuwe na jamaa wa misaada huko fukweni inapotokea wanaojifunza kuogolea wanataka kuzama, ili waweze kuwaokoa.
 
Inatisha na inatia huruma. Wasomi kama hao wanakufa kabla hawajatoa michango yoa kwa Taifa. Je wlienda kuogelea kama Leisure au ni moja ya somo la udaktari?
 
Inatisha na inatia huruma. Wasomi kama hao wanakufa kabla hawajatoa michango yoa kwa Taifa. Je wlienda kuogelea kama Leisure au ni moja ya somo la udaktari?

Mkuu ni kweli kuwa inasikitisha na kutia huruma kwa vifo vya madaktari hao watarajiwa ambao wao,wazazi wao na ndugu zao walikuwa na ndoto kubwa tofauti juu yao.
lakini nasikitishwa zaidi na mtazamo wako hata unauliza ikiwa walikwenda kuogelea kama sehemu ya somo la udaktari.Kwanza ungesoma vizuri mada nzima.Mtoa mada ametujuvya kuwa walikwenda kuogelea juzi(kwa mujibu wa tarehe ya leo) jioni.Siku hiyo ni siku ya mapumziko kitaifa, hivyo shughuli rasmi za darasa huwa zinasimamishwa.Tena jioni.
Naungana na mawazo ya Hofstede kuwa ufanyike utafi kujua fukwe zipi ni salama ni zipi si salama.Ama sehemu ya ufukwe upi ni hatari.Fukwe za kigamboni ni salama na safi, ila kuna maeneo fulani kuanzia pale Shule ya Msingi Mjimwema hadi kule Sunrise beach, pia maeneo fulani ya Gezaulole kuna kina kirefu.Kuna cliff. Hivyo mwanzoni unaweza ona kama pafupi kumbe umbali si mrefu unakutana na kina kirefu ghafla.
Taarifa ya Polisi ndiyo itakayotupa ukweli sababu za kifo chao.lakini mimi nafikiri walikutana na hicho kina kirefu cha ghafla kisha wakasombwa na mawimbi.Ikumbukwe kuwa huu ni wakati wa bahari kujaa mapema.Na kwa uzoefu wa Beach hizo mara nyingi zikijaa kunakuwa na mawimbi ya makubwa ama ya kati kutegemea uvumi wa upepo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom