Wanachuo wanatarijiwa wasafiri toka mikoani kufuata admission letter na kitambulisho

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
537
Katika hali ya kushanganza chuo kikuu cha Dar es salaam kimewatangazia wanafunzi wanaotarajia kujiunga na chuo hicho kuja kuchukua admission letters kuanzia jumatatu ya leo (Tar. 18/10/2010). Tangazo hilo limewafanya wanafunzi watarajiwa walioko mikoani kumiminika dar kwa ajili ya kuchukuwa barua hizo, huku wengine wakiamini kuwa chuo kimeshafunguliwa. Ukweli ni kuwa chuo kitafunguliwa kuanzia 05/11/10, cha kushanganza ni kwa nini wawaite vijana mapema namna hii? Nani atagharamia nauli ya kwenda na kurudi mikoani mpaka chuo kitakapofunguliwa? nani atagaramia malazi na chakula? Kwa nini wasingetumiwa hizo barua huko huko waliko? au kwa nini wasingechukuwa hizo barua wakati wa orientation week?
Chuo kikuu Dar ni chuo kikongwe ambacho tunategemea kuwa kitafanya mambo yake kisomi bila kuwaingiza katika gharama zisizo za lazima watanzania wengi maskini. Cha kushangaza wanafanya mabo yao kama vile sio wasomi. UD mnaboa sometimes
 
Yawezekana ni mbinu ya kuwakwamisha baadhi Dar ili wasipige kura huko makwao walikojiandikisha.
 
hii ni balaa, yaani wachuo wanapelekwa makwao na wanyumbani wanaletwa vyuoni, ili mradi vijana wasipige kura, kura zibaki za wazee tu
 
Hatuna watu viongozi amkini ktk taifa letu wengi wao ni vibaraka wakubwa wa ccm. Wanaturudisha nyuma kimaendeleo.
 
Bwana sisi ni wagumu wa kuelewa mambo sana. Unajua wanafanya hivi ili wanafunzi hao watingwe na hiyo mikikimikiki ya safari na kutafuta nauli ili wasipige kura. Wanataka siku ya kupiga kura wengi wawe kwenye maeneo mengine na vituo walivyojiandikishia
 
Back
Top Bottom