Wanachuo waliomwangukia mwambungu na funzo kwa vijana wa kizazi hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachuo waliomwangukia mwambungu na funzo kwa vijana wa kizazi hizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luther3, Feb 13, 2012.

 1. Luther3

  Luther3 Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa ya habari tbc imeonesha jinsi vijana yaani wanachuo cha walimu songea waliokwenda kumwangukia mkuu wa mkoa wa ruvuma mwambungu.hii ni baada ya kugomea kufanya mtihan wa somo ambalo hawakuwahi kufundishwa.kwa mshangao wangu mkubwa ni jinsi vijana hawa wasomi wa kitanzania walivyojiaibisha kwa kupiga magoti mengi na kulialia hovyo mbele ya mkuu wa mkoa huyo.kwasababu mgomo wao unasababu za msingi sasa kulialia kule ni aibu na wamekizalilisha kizazi chetu.waligoma nini sasa kama watu wenyewe ni waoga kias hiki lol!!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu kunguru mwoga hukimbiza ibawa wake
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  tbc?usikute wamefabricate story hiyo,ushasahau wanavogeuzaga na habari zingine kwa manufaa wanayoyajua wao?
   
 4. k

  kuzou JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kiukweliwanachuo na wanafunzi wengi huwa hawana pakwenda baada ya kutoswa ni kuigana mkiwa wengi chuoni,waliyoyafanya vijana kwenye tv ni uhalisia na uugwana ila mkuu wa mkoa ndio ameniboa asingewaruhusu kufanya hivyo kwani nikuonyesha umungu mtu,pia hakuwasaidia ni kama vile alijua nakuita tv
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wale ni watoto wa maskini na pale ndio wanaona jahazi linazama hivyo!Ulitaka wafanyaje kama sio kulia?
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ni Propaganda za TBC na serikali yao mfu how would it happen Msigwa akajuwa wako kwa mkuu wa mkoa walitoa press realise
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Waalimu wa bongo Wana taahira ya akili
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Huu ni uvivu wa mwafrika. Anaangalia maisha kwenye angle moja tu. Nimesoma gazeti kuna ji-mwalimu jingine limecharazwa viboko na mwekezeza wa ki-korea huko Dodoma. Watanzania tukelegea namna hii tutakuja chokonolewa hata na kusipofaa
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Be real!! what is reality?? kuwa wakifukuzwa chuo wanaenda wapi?? they are bright!
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,912
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 160
  Sababu za kumwangukia wakati walikuwa wamegoma ni nini hasa?
  Mleta habari naomba ufafanuzi.
   
 11. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania bwana yaani tunaomba HAKI?
   
 12. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Niliangalia habari ile ikanisikitisha kiasi cha kutosha. Nilijiuliza, uu wapi uelewa wa waTanzania? Kama hao ndio waalimu wanaotegemewa kuwafundisha vijana kujiamini na kusimamia mambo ya msingi, uu wapi ujasiri wao? Haikuingia akilini mwangu hata kidogo kwamba mgomo wa kukataa kushiriki mtihani ambapo somo halikufundishwa kuwa linaweza kuwa kosa kubwa kiasi kile.

  Nilijiuliza zaidi, katika ulimwengu wa leo, kweli Mkuu wa mkoa anapigiwa MAGOTI!! Sijui yeye (mkuu wa mkoa) na hao wanachuo walijisikia vipi. Laiti ningekuwa mimi, ningekataa wasinipie magoti kwani mie siyo MUNGU.
  Lakini hii ilinirejesha nyuma na kujiuliza, labda ndio sababu mkuu fulani wa wilaya aliwahi kuwashikisha waalimu chini na kuwachapa viboko! Kupiga magoti na kulia kiasi kile kulikuwa na tofauti na kuchapwa viboko? Je, mkuu wa mkoa angewaambia kuwa wanastahili adhabu ya viboko baada ya kuwaona katika hatua ile, ili waweze kusamehewa wangeikataa hiyo adhabu?

  Nafikiri bado sisi waTanzania tuna shida ya msingi ambayo tunatakiwa kuifanyia kazi ili tuweze kusimamia haki zetu.

  Nasikitika kwa udhalilishaji na kujidhalilisha nilikokuona jana! Sijui tumlaumu nani, labda sisi wenyewe and mfumo unaotuandaa watanzania.
   
 13. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Imeniuma sana kuona wanavyopiga magoti nikapandwa na hasira yaani wale wallimu hawafai bora wafukuzwe jumla,wale ni magoi goi kuomba msamaha sio kosa ni jambo jema lakini the way walivyo humble ni aibu tupu hata kwa Mungu wametenda dhambi kumpigia magoti mwanadamu,ndo maana mwanangu wa ujana nimpeleka kusoma Nairobi sio kwamba hakuna shule TZ bali MOTTO wa shule za kikenya zinasema Watamfanya mtoto kujiamini,sio kwamba nahusudu ukabila hivi wale ni kabila gani? Kile kitendo walichonyesha wale vilaza ni mwiko kule kwetu mkoa maalum wa kipolisi!
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndo nchi yatu.... Nashangaa hata huyo aanayewatahini, hivi anawatahinije watu ambao hajawafundisha? Si wendawazimu huo?
   
 15. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Shame even to watch kiukweli mi nilikua naangalia pembeni kila walinyokua wakiwaonesha vijana wenzangu hii ilinikumbusha enzi zile niko chuo miaka kama 2 hivi iliyopita tuligoma darasa nzima kufanya paper za mwisho wa mwaka (mwaka wa 4 semester ya mwisho)kwa sababu kama ya hao vilaza wa ualimu ila tulikua na ushirikiano na msimamo wakakaa kikao wakisema tunapewa supplemantary tutakaa mwaka mzima kadi tuje kufanya na wengine kutokana na weledi wetu haraka tulitinga mahakamani kusimamisha mitihani hadi haki itendeke hapo ndo ikawa ngoma nzito maana walishindwa kutubana na sheria ikachukua mkondo wake tukaruhusiwa kufanya paper
  ss hawa nguruwe pori wao wamekimbilia kwa mkuu wa mkoa ni sahihi but wangechukua hatua mapema zaidi kabla janga halijawa kubwa kiasi hicho
  hata hivyo na wasiwasi na wakufunzi wa pale chuo maana nahisi na wao ni miungu mtu wasiotaka kuguswa nafaham vizuri system za vyuo vya ualim vilivyo na ubabe juu ya waalimu ndo maana waalimu wengi wakimaliza vyuo hivi huwa na visasi visivyo na maana kumbe walitendwa vibaya tangu wako chuo
   
Loading...