Wanachokosea ni kuendelea kuiamini CCM!!

Hivi sasa kuna fukuto kubwa miongoni mwa Waislamu kila unapofanywa uteuzi ndani ya Serikali wao huangalia kama kuna muislamu yeyote ameteuliwa. Mara nyingi huambulia patupu. Kwenye vyombo vya habari kama Gazeti la "Mizani" humo kina Sheikh Khalifa kwa juhudi kubwa kabisa hadi wamefikia kuchapisha majina ya waislamu ambao wanadhani wana sifa ya kuteuliwa kwenye teuzi zinazofanywa lakini hawateuliwi.

Mimi si muumini wa siasa au maisha kwa kuangalia vigezo vya dini ya mtu, lakini kama ipo dhana ya dini au kundi fulani la watu katika jamii linaona kama linabaguliwa ni vema jambo lenyewe likafanyiwa kazi. Ni kweli kwamba waislamu wanabaguliwa kwenye nchi hii na chanzo cha kubaguliwa kwao ni nini na anayewabagua ni nani?

CCM ni zao la TANU na ASP, kwa maana nyingine vyama hivyo viwili ndiyo asili ya CCM. Hapa hatuwezi kuijadili ASP kwa kuwa kwa muktadha wa mada hii yenyewe moja kwa moja haifai kujadiliwa. Mara baada ya Uhuru kulikuwa na vyama vingi vya siasa mpaka pale vilipopigwa Marufuku na TANU mwaka 1965. Jee waislamu waliunga mkono chama gani kati ya TANU na hivyo vingine?

Miaka 27 baadaye mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulirejeshwa hapa nchini na CCM iliyozaliwa kwa kuunganisha vyama vya ASP na TANU, nayo ikajivika uhai kabla haijazaliwa kisheria. Tangu hapo hadi sasa nchi yetu imekuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Jee kwa kipindi chote hicho waislamu unapofika wakati wa uchaguzi huunga mkono chama gani cha siasa kama si CCM?

Kwa nini kina Sheikh Khalifa na kina Mohamed Said huwa siwasikii wakisema chama kinachosababisha wao wabaguliwe ni CCM kwa kuiga tabia ile ile ya TANU badala yake wanazungumza kiujumla kwamba wanabaguliwa? Kama Serikaili ndiyo inawabagua waislamu na kuwapendelea wakristo hiyo serikali inatokana na chama gani cha siasa kama si hapo awali na TANU na sasa CCM?

Hao wanaoleta Orodha ndeefu za wasomi wa kiislamu ili wateuliwe na Magufuli mwaka jana walikiunga mkono chama gani kama si CCM? Sheikh Khalifa anasema kuwa wao walimuunga mkono Magufuli kwa kuwa hakuchangiwa na wafanyabiashara kwenda Ikulu. Hilo analisema kama ni ukweli anaousimamia ama kama ni Kada wa CCM kushabikia kauli ya Mwenyekiti wake Taifa kwamba hakuchangiwa na wafanyabiashara?

Waislamu wa nchi hii wakiongozwa na kina Sheikh Khalifa na BAKWATA kosa lao kubwa ni kuiamini CCM ambayo mwisho wa siku ikiunda serikali, wao huja kulalamika kwamba inawabagua kwenye kila nyanja ya maisha. Kosa ni lao wala si la CCM!
Allen,
Umesema maneno mazito sana na ya kufikirisha.

Nimgependa sana kama Waislam wangepata nafasi ya kusoma
maneno haya yako kwa ukamilifu wake wote.

Mimi huenda sijaeleza nafasi ya chama katika ubaguzi wa Waislam.

Lakini nimetaja nguvu ya Kanisa Katoliki katika kuendesha nchi na
hili limekuwa tatizo kubwa kiasi hujui lipi la serikali na lipi la Kanisa.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeandika maneno haya:

''Kanisa limekuwa na nguvu na udhibiti wa mambo kiasi kwamba wakati mwingine watendaji, hasa Wakristo katika serikali na ndani ya chama tawala CCM hawajui utii wao upo kwa nani, serikalini au katika Kanisa? Ni katika kuchanganyikiwa huku kwa watendaji wa serikali kuhusu uhusiano wao na Kanisa na serikali ndiko kulikoamsha kutoaminiana kati ya Waislam na serikali mara tu baada ya uhuru kupatikana. Serikali ikaonekana kama moja ya taasisi za Kanisa na Waislam wakiwa ni watazamaji tu. Mara baada ya uhuru Kanisa likaangalia nafasi yake na serikali mpya iliyokuwa madarakani. Wakati wa kudai uhuru Kanisa lilijiweka mbali na siasa na ikaonekana kuwa Kanisa lilikuwa likiheshima ule mpaka kati ya dini na siasa. Wakati ule mgongano kati ya Kanisa na serikali haukupata kusikika hata kidogo. Baada ya uhuru kupatikana tu na serikali ikawa mikononi mwa wananchi, Kanisa likaanza kusikika likisema kuwa lina haki na wajibu kuwa na ushawishi ndani ya serikali, kuikosoa serikali na kuingooza pale inapoona serikali haifanyi mambo sawa kwa matarajio yake. Katika msimamo huu mpya, Kanisa likajipa fursa ya kuwa msemaji wa watu. Huu ulikuwa ni mwelekeo mpya katika mambo ya siasa na utawala.''

Allen,
Kanisa limekuwa likisemea watu wote au maslahi yake?

Ni wazi Kanisa limekuwa likiangalia maslahi ya waumini wake
kwa kuwatumia viongozi Wakristo na watumishi walio katika
serikali kujijenga na kupiga vita Uislam na Waislam.

Tuanze hapa tutaendelea In Shaa Allah hadi tufike kwa nini
Waislam wanaunga mkono CCM ilhali inawabagua.
 
Tuanze hapa tutaendelea In Shaa Allah hadi tufike kwa nini
Waislam wanaunga mkono CCM ilhali inawabagua.
Nitafurahi sana kama utatoa huo ufafanuzi ili na siye wengine tujue inakuwaje chama kinachowabagua lakini bado kikawa na sifa ya kuchaguliwa na Waislamu.

Shukran Jaazera kwa kuchangia!!
 
Hata humu kuna mabandiko mengi sana ya kulalamika waislamu kubaguliwa pamoja na lile lenye Orodha ya wasomi waislamu.
Nilitaka umjibu yule jamaa niliyemkot maana inaonekana hajakuelewa as if wewe ndiye unalalamika kuwa waislam wanabaguliwa
 
Nitafurahi sana kama utatoa huo ufafanuzi ili na siye wengine tujue inakuwaje chama kinachowabagua lakini bado kikawa na sifa ya kuchaguliwa na Waislamu.

Shukran Jaazera kwa kuchangia!!
Allen,
Kubwa lililofanywa ni kuvunja nguvu ya Waislam katika TANU na kufuta
historia yao.

Hili lilifanyika mwaka wa 1963 kwa kuvunja Baraza la Wazee wa TANU
ambalo lilikuwa na wajumbe Waislam watupu na si kwa kuwa Wakristo
hawakutakiwa ila kwa sababu harakati za kupigania uhuru ziliongozwa
na Waislam.

Mwaka wa 1964 viongozi wa Waislam wengi wao wakiwa masheikh
walikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kisingizio kuwa walikuwa na
mkono katika maasi ya Tanganyika Rifles.

Mwaka wa 1968 EAMWS taasisi kubwa ya Waislam ikapigwa marufuku
na badala yake Waislam wakaundiwa BAKWATA.

Mipango yote ya kujenga shule na kujenga chuo kikuu ikafa pamoja na
EAMWS.

Ikawa sifa kubwa ya kuwa kiongozi wa Waislam ni lazima uwe mtu wa
kulamba nyayo za waliokuwa latika madaraka.

Sambamba na haya mkakati ukawekwa wa kuwanyima elimu Waislam
kwa kuwahujumu kupitia Wizara ya Elimu.

Wizara ya Elimu ikawa moja ya idara ya Kanisa ikitumika kuutia nguvu
Ukristo kwa kuwapa fursa vijana wa Kikristo na kuwahujumu Waislam.

Taratibu TANU ikawa inatolewa kwa waasisi wake wa asili na kukabidhiwa
kwa watu wapya na hawa watu wapya wakawa wanaifuta historia ya TANU.

Ikawa mwiko mkubwa kwa mtu yoyote kuinasibisha TANU na waasisi wake
pamoja na Uislam.

Uislam na Waislam ikawa kitu nyeti kabisa na mwiko mkubwa kutafiti au
hata kuandika historia yake.

Wakati haya yakitendeka sambamba na haya wakajengwa Waislam ndani
ya mfumo huo wakapewa vyeo na kufanywa mfano wa kuwapo kwa Waislam
katika serikali na taasisi za nchi.

Ikawa sasa akitokea Muislam yoyote kuuliza na kutaka kujua kwa nini kuna
ubaguzi dhidi ya Waislam huyu alishughulikiwa na kutolewa madarakani kwa
kutumia kila aina ya hila.

Haukupita muda Waislam wakawa raia daraja la pili hawana mbele wala nyuma.
Hawawashi wala hawazimi.

Sivalon (1992) akasema Wakatoliki wamehodhi 74% ya Bunge la Tanzania na
26% imo kwa Wakrsito wa madhebu nyingine pamoja na Waislam.

Katika huo mgawo unaweza wewe mwenyewe ukakisia mgao wa Waislam
utakuwa asilimia ngapi.

Waislam wakawa jamii masikini kwa hali na elimu.

Katika hali kama hii Waislam hata kama watataka kupigania haki yao wanaweza
kweli kwa njia hizi za kura kuangusha ngome hiyo ya CCM na wakasalimika na
Sheria ya Ugaidi?

Allen tusimame hapa kwanza In Shaa Allah tutaendelea.
 
Katika hali kama hii Waislam hata kama watataka kupigania haki yao wanaweza
kweli kwa njia hizi za kura kuangusha ngome hiyo ya CCM na wakasalimika na
Sheria ya Ugaidi?

Allen tusimame hapa kwanza In Shaa Allah tutaendelea.
Ingawa Maelezo yako mengine sikubaliani nayo sana, lakini unataka kusema kuwa waislamu wakitaka kuwa kinyume na CCM wataitwa magaidi? Kwa nini?
 
Waislamu wanalalmika kuwa serikali inawabagua, na hata ile orodha ya wale waislamu wasomi, Sheikh Khalifa hakuitoa ili Mbowe aitumie bali ili Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa aitumie. Na kwako wewe Mwalimu Salum na Profesa Safari ni wakristo. Halafu Mbona CUF viongozi wake wengi ni waislamu na wala hamuiungi mkono?

Maajabu Lipumba ambaye ni Professa Muislamu alifanya "Jitihada" ili CCM ishinde wakati yeye akiwa ni mwenyekiti wa CUF.
99%
 
Tena jana Sheikh Khalifa karudia kulalamika ingawa analalamika kwa haki, lakini amerudia tena kusema yeye ni CCM. Sasa CCM ndiyo ina viongozi kama Balozi Seif Idd ambao wanafurahia hao anaolalamika sheikh Khalifa kwamba wanadhalilishwa!
 
Back
Top Bottom