Wanachokosea ni kuendelea kuiamini CCM!!

Tatizo siyo waislamu kama waumini bali wale wanaojifanya kuzungumza kwa niaba ya waislamu. Wakati wa Uchaguzi utaona mpaka wanajiapia wakisema CCM ndiyo chama kinachojali waislamu, uchaguzi ukiisha tu wanaanzisha "mihadhara" na mpaka kusoma "Itkaf" kulaani waislamu kubaguliwa na serikali iliyoundwa na chama kile kile walichokipigia chapuo wakati wa uchaguzi!
kwanini hao waumini wapo kimya? wanakubali vipi watu wasio waisilamu kuwasemea mambo makubwa ili hali wakijua wanaingizwa chaka? tumewachoka bana
 
Hawa jamaa wanachezewa na ccm kila uchaguzi ukifika. Mara utasikia mahakama ya kadhi. Nasikia wengine wakipewa pilau tu wanalainika........
Waislamu wanajua mambo mawili tu
1. Yesu sio Mungu
2. Wanategemea kugawiwa mabikra baada ya kifo

ukweli wakichokozi
 
Mkaruka hoja yangu hapa kama "waislamu" wanaona kwamba wanaonewa na Serikali inayoundwa na CCM wakati kila wakati wa uchaguzi wao ndiyo huipigia chapuo CCM, basi kosa si la CCM kutokuwajali bali kosa ni lao wenyewe!!
 
Hivi sasa kuna fukuto kubwa miongoni mwa Waislamu kila unapofanywa uteuzi ndani ya Serikali wao huangalia kama kuna muislamu yeyote ameteuliwa. Mara nyingi huambulia patupu. Kwenye vyombo vya habari kama Gazeti la "Mizani" humo kina Sheikh Khalifa kwa juhudi kubwa kabisa hadi wamefikia kuchapisha majina ya waislamu ambao wanadhani wana sifa ya kuteuliwa kwenye teuzi zinazofanywa lakini hawateuliwi.

Mimi si muumini wa siasa au maisha kwa kuangalia vigezo vya dini ya mtu, lakini kama ipo dhana ya dini au kundi fulani la watu katika jamii linaona kama linabaguliwa ni vema jambo lenyewe likafanyiwa kazi. Ni kweli kwamba waislamu wanabaguliwa kwenye nchi hii na chanzo cha kubaguliwa kwao ni nini na anayewabagua ni nani?

CCM ni zao la TANU na ASP, kwa maana nyingine vyama hivyo viwili ndiyo asili ya CCM. Hapa hatuwezi kuijadili ASP kwa kuwa kwa muktadha wa mada hii yenyewe moja kwa moja haifai kujadiliwa. Mara baada ya Uhuru kulikuwa na vyama vingi vya siasa mpaka pale vilipopigwa Marufuku na TANU mwaka 1965. Jee waislamu waliunga mkono chama gani kati ya TANU na hivyo vingine?

Miaka 27 baadaye mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulirejeshwa hapa nchini na CCM iliyozaliwa kwa kuunganisha vyama vya ASP na TANU, nayo ikajivika uhai kabla haijazaliwa kisheria. Tangu hapo hadi sasa nchi yetu imekuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Jee kwa kipindi chote hicho waislamu unapofika wakati wa uchaguzi huunga mkono chama gani cha siasa kama si CCM?

Kwa nini kina Sheikh Khalifa na kina Mohamed Said huwa siwasikii wakisema chama kinachosababisha wao wabaguliwe ni CCM kwa kuiga tabia ile ile ya TANU badala yake wanazungumza kiujumla kwamba wanabaguliwa? Kama Serikaili ndiyo inawabagua waislamu na kuwapendelea wakristo hiyo serikali inatokana na chama gani cha siasa kama si hapo awali na TANU na sasa CCM?

Hao wanaoleta Orodha ndeefu za wasomi wa kiislamu ili wateuliwe na Magufuli mwaka jana walikiunga mkono chama gani kama si CCM? Sheikh Khalifa anasema kuwa wao walimuunga mkono Magufuli kwa kuwa hakuchangiwa na wafanyabiashara kwenda Ikulu. Hilo analisema kama ni ukweli anaousimamia ama kama ni Kada wa CCM kushabikia kauli ya Mwenyekiti wake Taifa kwamba hakuchangiwa na wafanyabiashara?

Waislamu wa nchi hii wakiongozwa na kina Sheikh Khalifa na BAKWATA kosa lao kubwa ni kuiamini CCM ambayo mwisho wa siku ikiunda serikali, wao huja kulalamika kwamba inawabagua kwenye kila nyanja ya maisha. Kosa ni lao wala si la CCM!
Kuna kitu kama nimekielewa hivi.
 
kwanini hao waumini wapo kimya? wanakubali vipi watu wasio waisilamu kuwasemea mambo makubwa ili hali wakijua wanaingizwa chaka? tumewachoka bana
Lazima ipo njia ya kutokea. La kwanza ni kuwaonesha nani ni adui yao. Wao wanakazana na "mfumo Kristu" wakati mzazi wa huo mfumo wanamkumbatia kama mti wa tambiko.
 
lumumba wanapochaguana wao tu kwenye nafs ambazo hata c za kisiasa wapinzan wakilalamika watu wanaponda, zenji wakilalamika wanapunjwa baadh ya nafas kwe sirikali ya muungano watu wanaponda,wanawake wakilalamika hawapati nafas sawa kwe teuz za viongoz kama wanaume watu wanaponda...sasa kama wewe ni mpenda haki basi isiwe tu kwe dini bali popoe pale unapoona hakuna usawa uwe wa kwanza kukemea sio tu kwe dini bali kwe kila sekta kwan ni dhahiri kuwa Mungu wetu anapenda haki.............
 
Ndugu yangu haya si mambo ya udini bali ni mambo halisi. Waislamu kila mahala iwe ni kwenye makongamano, kweye Hutuba za misikitini, kwenye mihadhara na hata kwenye vijiwe mitaani, wanalalamika wanabaguliwa na "mfumo Kristu" sasa kwa mtazamo wangu huo mfumo Kristu unalelewa na CCM na CCM ndiyo chama kinachoungwa mkono kwa wingi na waislamu. Sasa kuna haja ya kulalamika kwa matendo ya chama unachokipenda na kukichagua kwenye kila uchaguzi?

Halafu udini na Dini ni vitu viwili tofauti. Udini ni pale watu wawili wenye sifa sawa ukamchagua mmoja kwa sababu ni wa dini yako tu ama ni mmoja kazidiwa sifa na mwenzie wewe ukamwacha yule mwenye sifa na kumchagua asiye na sifa kwa kuwa ni wa dini yako.
Unakokokotea Siko, Watanzania ni Waelewa sana ktk Chaguzi zote zilizofanyika Upinzani haujakua na Mgombea anayekubalika.

Hii ikiendelea CCM itaendelea kutawala.
 
Hawa jamaa wanachezewa na ccm kila uchaguzi ukifika. Mara utasikia mahakama ya kadhi. Nasikia wengine wakipewa pilau tu wanalainika........
Waislamu wanajua mambo mawili tu
1. Yesu sio Mungu
2. Wanategemea kugawiwa mabikra baada ya kifo
Tumia viungo vya kawaida kufikiri.
 
"Kote huko unataka kusema kuwa jina la kislamu likifika wanalipinga chini na kuchukuwa wa dini nyingine?,"

Kipengele hiki ungemlenga ama kumtaja jina yule aliyeleta orodha ya majina ya wale waislam wenye sifa za kuteuliwa lakini hawakuteuliwa.

Pia ukisima vizuri andiko la Allen amewashauri tu wanapokosea hajasema wachague chama fulani yaani kwa mfano unakula wali kila siku unakuletea matatizo unalalamika then unaambiwa tatizo lako ni kula wali kila siku? Je hapo amekwambia uwe unakula ugali? Hebu soma vizuri andiko na ondoa u-siasa kichwani kabla ya kujibu, mbona vyama pinzani viko vingi kwa nini ukitaje CHADEMA? kuna CUF, ACT, nk
 
Alleni kilewela naamini ww ni mtu mzima na unaakali timamu.. Hivi haya mambo ya kusema waislamu wanabaguliwa inakusaidia nn?
Kwan waislamu wanaenda kuendesha madrasa kwenye hizo nafasi watakazo chaguliwa?

Hivi kwamfano Leo hii na wao wakakubaliana na kauli yako wakaamua na wao kuanzisha Dora yao ww unafikir utakuwa ktk hali gani?

Mambo mengne acheni msiwe wapumbavu kwa kwaendeshwa na mihemko ya kisiasa..
 
Unakokokotea Siko, Watanzania ni Waelewa sana ktk Chaguzi zote zilizofanyika Upinzani haujakua na Mgombea anayekubalika.

Hii ikiendelea CCM itaendelea kutawala.
Kama huyu aliyeko ndiye aliyekuwa bora kwenye uchaguzi uliopita, kwa nini anapofanya teuzi kina Sheikh Khalifa wanalalama magazetini kwamba waislamu hawateuliwi?
 
Mwanzi1 mbona huwa hamuwakemei kina Sheikh Khalifa wanapo "Generalize" kwamba wanaongea kwa niaba ya waislamu? Unakumbuka waliposema ni dhambi kwa "waislamu" kushiriki kwenye maandamano ya UKUTA? Halafu unataka kusema kwamba huko ambako majina ya wateuliewa "hupitia" ni majina ya waislamu tu hukwama?
Labda na wao viongozi wa dini wanatakiwa wajiridhishe na uhalisia wa upatikanaji wa viongozi nchini, lakini kulaumu kuwa kuna ujanja unafanyika mimi hilo nilikataa. Kama nilivyosema awali, muumini au kiongozi wa dini yoyote nchi ana haki ya "KUSHAURI" na sio "KULAZIMISHA" waumini wenzake wafate mfumo gani au wa support kikundi kipi. Lakini wanasiasa hawaruhusiwi kwenda kwenye dini na kuanza kushauri au kuomba support ya kichama. Viongozi wa dini kupinga kusupport UKUTA ni haki yao kwasababu wako huru. Na hata kama kuna kitu kina taka kufanya na CCM na wao hawapendezwi nacho, wanahaki ya kupinga. Sasa waislamu wakilalamika, Hindu na Bohora wasemenini? Na wao si watanzania pia?
 
mi sioni kosa hapo... cha msingi ni je!?. haki zao kisheria kama raia na kama taasisi zinapatikana???
 
Mgirik anayesema waislamu wanaonewa siyo mimi ni kina Sheikh Khalifa na wenzake. Halafu ninachoshangaa ni wao mwaka jana walikuwa wanawashawishi watu waichague CCM!
 
Alleni kilewela naamini ww ni mtu mzima na unaakali timamu.. Hivi haya mambo ya kusema waislamu wanabaguliwa inakusaidia nn?
Kwan waislamu wanaenda kuendesha madrasa kwenye hizo nafasi watakazo chaguliwa?

Hivi kwamfano Leo hii na wao wakakubaliana na kauli yako wakaamua na wao kuanzisha Dora yao ww unafikir utakuwa ktk hali gani?

Mambo mengne acheni msiwe wapumbavu kwa kwaendeshwa na mihemko ya kisiasa..
Aliyesema waislam wanabaguliwa SIYO Allen Kilewella, yeye ameleta mada kama malalamiko ya waislam wenyewe yalivyo jitokeza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Allen anawaambia waislam wanalalama nini kubaguliwa ikiwa wao ndiyo wanachagua mfumo huu unaowabagua? Hivyo kumbe kuna mahala ameona wanalalamika kubaliwa, Ila muulize Allen umeona wapi waislam wanalalamika?
 
Kama huyu aliyeko ndiye aliyekuwa bora kwenye uchaguzi uliopita, kwa nini anapofanya teuzi kina Sheikh Khalifa wanalalama magazetini kwamba waislamu hawateuliwi?
Nadhani wengi wenu hamjui ama Ubishi ni Kanuni yenu Sikiliza:

Kuna Makubaliano Mabaya yaliyofanywa kwa Hila kwamba Uongozi utafanywa kwa Kupokezana kati ya Dini Hizo ingawa haikuandikwa popote, malalamiko toka kwa upande mmoja yalipoanza ndipo Neno Tanzania haina Dini lilipoanza kutumika kuanzia Kikao cha Maaskofu mpaka Kikao cha Masheikh Zanzibar.

Wapiga Kura wanaangalia Badala yenye Kufaa siyo kubadili tu.
 
Allen Kiwella ulichokusudia ndicho tunachojadili unapewa Majibu kwa Ujazo.
 
Back
Top Bottom