Wanachokifanya Marekani na NATO kwa ujumla dhidi ya Urusi ni sawa na kumbana paka kwenye kona; atakachokufanyia utakisimulia masha yako yote

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Wanachokifanya Marekani, NATO na mataifa ya magharibi kwa ujumla dhidi ya urusi ni kuifunga mikono na miguu Urusi wakati ikipigana na ukraine, ili kuisaidia Ukraine kwenye vita hivyo. Hakuna asiyejua kuwa nguvu ya kiuchumi ndiyo mikono na miguu inayohitajika sana wakati wa vita ili kuwezesha vita.

Kwa hiyo kuifunga nchi inayopigana miguu na mikono ni sawa na kumbana paka kwenye kona. Akijiridhisha kuwa umembana na hana mahali pa kutokea, atabadilika ghafla na kuwa mnyama mkali na mwenye nguvu hujawahi kuona!! Lazima akuvamie na aondoke na pua zako!

Urusi inaishiwa nguvu za kiuchumi kwa haraka sana kutokana na vikwazo vya kiuchumi na kuporwa mali zake zote ilizowekeza nchi za nje.

Niamini, urusi itafanya unyama wa kutisha maana haiwezi kukubali kushindwa hata kama imefungwa miguu na mikono, lakini kichwa kiko wazi. Tutegemee vita vya nyuklia muda wowote tangu sasa na mlengwa wa kwanza ni marekani na uingereza.

Wenye ndugu nchi hizo waambieni warudi nyumbani kabla hawajachelewa!! Mark my words!
 
Kuna Jeshi la Urusi na wananchi wa Urusi

Jeshi la Urusi linapiga Ukraine nchi za Magharibi zinapigana ndani ya Urusi kwa kupitia vikwazo

Sasa hivi hakuna mwananchi wa Urusi asiyelia kwa vikwazo

Benki sasa hivi huruhusiwi kuchukua dola kwenye akaunti yako ya benki

Kitakachofuata ni wananchi kuangusha Serikali ya Putin

Sasa hivi Jeshi la Urusi na wananchi Hawaiivi hawaungwi mkono na raia sababu ya vikwazo
Nchi za Magharibi zimeingia ndani ya Urusi kupigana kisayansi kwa kupitia vikwazo
 
Na ndicho kinachoenda kutokea.

Kwanini waandishi na wadadavuzi wa mambo msijikite kuandika nini kinaenda kutokea iwapo makombora ya nyuklia yatatumika?
Athari zake ni zipi kwa dunia?
Unawezaje kujikinga na hayo madubwana? Na....
Sahau hizo nyukilia

Jeshi la Urusi halina support ya wana Ukraine na nyumbani halina Support ya Raia wa Russia

Kimataifa pia halina support

Linapigana unpopular war
 
Russia atapoteza uchumi wake na hataweza shambulia USA kwa nuclear mana anajua huo ni mchezo wa piga nikupige ikiwa atafanya hivyo atajulikana mapema kabla ya USA haijawa moto RUSSIA itakuwa ni moshi na majivu tu tambua USA na washirika wake NATO ambao ni majirani kabisa na Russia tayari wanachukua tahadhari mana wanajuwa saa yoyote mwendawazimu anakurupuka hivyo atapigwa kwa ukaribu zaidi yani atachakaa..
 
Tatizo la Urusi ilitumia raslimali zake zote kujenga Jeshi badala ya uchumi

Nchi za Magharibi zenyewe zilitumia Raslimali zake kujenga uchumi kwanza na baada ya uchumi kukomaa ndio zikajenga Jeshi imara.

Walibalance Urusi haikubalance ndio maana sasa uchumi hoi na uchumi ukiwa hoi kupigana vita sio rahisi. Mahitaji mengi ya Jeshi yanahitaji uchumi imara.Ukiyumba uchumi na jeshi litayumba.Na linaweza kuasi muda wowote
 
Kuna Jeshi la Urusi na wananchi wa Urusi

Jeshi la Urusi linapiga Ukraine nchi za Magharibi zinapigana ndani ya Urusi kwa kupitia vikwazo

Sasa hivi hakuna wanamchinja wa Urusi asiyelia kwa vikwazo

Benki sasa hivi huruhusiwi kuchukua dola kwenye akaunti yako ya benki

Kitakachofuata ni wananchi kuangisha Serikali ya Putin

Sasa hivi Jeshi la Urusi na wananchi Hawaiivi hawaungwi mkono na raia sababu ya vikwazo
Nchi za Magharibi zimeingia ndani ya Urusi kupigana kisayansi kwa kupitia vikwazo
Wafia Vita ya mabomu hawatakuelewa kamwe.
 
Hili jambo ukilitafakari kwa undani bila muhemuko utapata majibu haya kwamba ipo siku nuke itatumiwa hasa kwa msimamo anaounesha Putin.

naona tahadhari zinazidi kutolewankwa raia wa marekani kwenda kujitolea kwamba hali ya huko ni mbaya na tahadhari kwa NATO ni wazi kwamba wameshajua kitakachotumika ni nini siku za baadae.
 
Russia hawezi kuamua tu kiholela kutumia bomu la nyuklia, na hata Biden nae kasema wazi hawezi kutuma majeshi Ukraine wala kuzuia anga la Ukraine kwani hiyo itakuwa WW3.

Russia mida hii wapo maporini wajipanga kuisambaratisha Kyiv iwe majivu.

Siku si chache Russia ataitwaa Kyiv.
 
Na kwa nini umbane paka kwenye kona anaweza kuwa kakukosea nini hadi umfanyie mnyama ukatili wote huo ? Wewe ni lazima utakuwa ni psychopath, kwanza hata hao Wamarekani wakisikia unawaambia wanambana mnyama wa Mungu kwenye kona, watakuona una matatizo ya akili!
 
Urusi hawana unyama wowote ni maneno yenu tu timu Putini, mulitegemea siku 2 tu mnamaliza kazi ukrean sasa kinachowatokea mbele yenu hamuamini macho yenu, Putini alidanganywa ni majenerali wake kuhusu vita ya ukraine walimpasha vibaya sasa yanayomkuta haamini, leo amewafukuza kazi 8 lakini 3 wamefariki

Putini hakuwa na hesabu za kisayansi wenzake wanatumia sayansi vizuri zaidi, yeye anadanganywa ni idadi ya silaha alizonazo, warusi wengi wamekamata Ukraine kama mateka, mipango yao imefeli, sasa putini anakasirika ovyo mara atumie kemikali kuua ndugu zake au aweke sawa vinu vyake vya nuclear kutisha tisha
 
Watu wengi wanakimbilia kusema urusi atatumia nuclear kumnyamazisha m Amerika akibanwa.urusi kumpiga Mmarekani moja kwa moja kwake ni mahesabu ambayo sidhani kama yapo kwa putin, ni ujinga kwa dunia ya sasa.Shambulio hilo litahitaji nguvu nyingi za Mrusi sababu ukishambulia unajitayarisha na kujikinga pia, kufanya ivo kutafungua mlango wa mataifa mshiriki wa Marekani ambayo yapo ulaya nao kujisogeza karibu na urusi.

Ulaya imepigana vita kuu mbili za dunia,na kama kuna watu wamebobea katika haya mavita ni wajerumani,hawa kupitia hitler walitetememesha sana dunia.Pia ikumbukwe,mataifa mengi ya ulaya magharibi yana hizo nuclear, na uwezo mkubwa wa kijeshi,kiuchumi na kitechnolojia na hawatatataka kuonewa au kutawaliwa tena na taifa wanaliona kwao ni tishio.Hii ndo moja ya sababu ya kuundwa kwa NATO,ku shughulikia migogoro ya aina hii.

Sahau China kuingilia huu mzimamzima,wataaangalia watanufaika ki vipi kwani nao bado wanawahitaji wazungu sababu ya Technology na uchumi wao.
 
Nope !!!!

Kinachotokea ni kama kujifungia ndani ili kuua panya unaondoa hewa ndani ya chumba, unasahau kwamba ukosefu wa hio hewa hata wewe inaweza kukuua.

America isipoangalia sanctions hizi ni double edge sword; ushirikiano wa Russia, China na nchi nyingine in long term unaweza kumuacha America na Dollar zake.

Ingawa Europe kutokana na hili inaweza kuwekeza zaidi kwenye sources nyingine za Energy hence kuwa more energy independent.

As for wananchi Russia wananchi wengi walishazoea umasikini ni hao ma Oligarchy ndio wanaweza wakawa wanalia na visenti vyao (jambo ambalo hata Putin alishaanza kuwabana wengine ambao walikuwa mlengo mwingine)

To illiterate; hapa anayeumia ni raia wa Ukraine wanaotumika kama Pawns kwenye Others Political Chess Board; Sio NATO wala America wanaojali kuhusu Ukraine but their own self interests.
 
Russia atapoteza uchumi wake na hataweza shambulia USA kwa nuclear mana anajua huo ni mchezo wa piga nikupige ikiwa atafanya hivyo atajulikana mapema kabla ya USA haijawa moto RUSSIA itakuwa ni moshi na majivu tu tambua USA na washirika wake NATO ambao ni majirani kabisa na Russia tayari wanachukua tahadhari mana wanajuwa saa yoyote mwendawazimu anakurupuka hivyo atapigwa kwa ukaribu zaidi yani atachakaa..
Jaribu kuweka ushabiki pembeni! Russia ameingia vitani akijua vikwazo vitakuwepo kabisa na ambavyo siyo vinaiumiza Russia pekee yake bali hata wazungu wenyewe! Russia ilijiandaa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom