MwanaPekee
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 382
- 385
Leo 17/11/2019 zinaanza rasmi kampeni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa kote nchini. Ikumbukwe kuwa hivi karibuni viongozi wa vyama kadhaa vya upinzani vikiwemo CHADEMA, ACT-Wazalendo, na NCCR-Mageuzi; walitangaza kuwa wagombea wao wanajiondoa kwenye uchaguzi huo kutokana na sababu walizozibainisha.
Leo ukipita katika baadhi ya mitaa unakuta kuna shamrashamra za hapa na pale kwa wanachama wa vyama vilivyotangaza kujitoa kwenye uchaguzi, hali inayoonesha kuwa wanachama wa chini huku mitaani, na matawini hawakubaliani na maamuzi ya viongozi wao.
Wanachama huku chini wanataka kuchagua viongozi wanaowataka wao, hasa baada ya serikali kutangaza kuwa mgombea yeyote aliyechukua fomu na kuirudisha basi anaingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Kitu ambacho viongozi wa upinzani inabidi wajifunze ni kuwa maamuzi yao ya kukurupuka yanawaumiza sana wanachama wao. Na hali hiyo imepelekea wanachama wao wengi kukosa imani nao.
Wanachama wa mitandaoni ni asilimia ndogo sana, hivyo ku-rely kwenye comments za mitandaoni kama ndiyo maamuzi ya wanachama walio wengi ni kosa kubwa sana, ambalo kimsingi ni sawa na kujichimbia kaburi lao wenyewe katika uringo wa siasa.