Wanachama wa CUF wana nguvu kushinda Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke?

Nimejiuliza swali hili lakini bado majibu hayajitoshelezi.

Jeshi la Polisi hawawezi kuwadhibiti wana CAF ambao Ni wavamizi wa mkutano wa ACT Wazalendo?

Udhaifu huu wa Jeshi la Polisi umeanza lini kushindwa nguvu na chama Cha siasa tena Cha upinzani.?

Tunatakiwa kuwalinda wanachama wa ACT Wazalendo wanafanya mkutano wao wa ndani sisi tukiwa nje.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke sijaelewa nguvu yenu ya ulinzi iko wapi.Prof Lipumba na wafuasi wake wanaweza kuwashinda nguvu kweli? Siamini hata kidogo.
Wawadhibiti mara ngapi ndiyo uelewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanadhani watanzania ni wajinga kiasi hicho. Wakati wa maandamano ya Mange walipiga kwata nchi nzima na kufanikiwa kuyadhibiti sasa sijui kwenye hili wanakwama wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi hili linailinda ccm tu, wengine huko wakivurugana hiyo sio juu yao, nia ni kuhakikisha vurugu za kila aina zinatokea kwa wapinzani na wapinzani hawakutani iwe ndani au nje, ila si kwa ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom