Wanachama wa CCM Ruvuma wacheza ngoma kumpongeza Magufuli!

Nchi Yetu Bado Tuna Safari Ndefu Sana wajinga ni wengi sana unampongeza mtu kwa kazi ambayo kaomba mwenyewe Kwani kura kapigiwa Afanye nini mbona watanzania vichwa Maji kiasi hiki
 
Binadamu kama hawa huwezi kuwakuta arusha na kilimanjaro
Hiyo mikoa ni ya wanjanja, hata kama utakuta ambae hajasoma lazima awe mjanja na kamwe huwezi mkuta anafanya ubazozo kama hawa mazwazwa...
Labda wale wanoishi mapori ya kule madogo kuinama...
 
Ndiyo maana hata mazao yao yanakosa soko!Unakatazwa usiuze mahindi nje ili uuze sh 250 kilo halafu unapongeza
 
Mkoani Ruvuma wanachama wa ccm wamejitokeza na kucheza ngoma, huku wanaume wa mkoani humo wakipiga push up na akina Mama kujigalagaza kwenye vumbi kwa kile walichodai ni kumpongeza Magufuli.

Tukio hilo lililopambwa na makada wa chama hicho kuvaa mavazi ya kijani na njano a.k.a yeboboyebo, wakina mama wakiwa wamevalia matisheti na kanga za msaada za rangi hizo, lilisindikizwa na akina baba waliovalia makofia ya kijani na matisheti ya kijani pamoja na suruali nyeusi lakini zikionekana zimechakaa sana ama kwa kuvaliwa kwa muda mrefu, au zikiwa pengine zimeokotwa kwenye madampo!

Wanachama hao ambao kwa wingi wao walivyoonekana wamekuwa kwa muda mrefu wakiandamwa na matatizo mbalimbali, kubwa likiwa ukosefu wa elimu (yaani ujinga), mengine ni barabara mbovu, kukosekana kwa maji safi, umaskini, huduma mbovu za afya n.k walikuwa wakisifia juhudi za magufulk za kupambana na ufisadi lakini huku wao wakiwa hajui ni jinsi gani matatizo yao tatakavyotatuliwa!

Lakini kimsingi haya waliyokuwa wakifanya ina maana siyo siasa zile Magufuli alizokataa mpaka 2020?

Kwani siasa za hadharani ni mpaka iwe mikutano ya hadhara, hizi ni double standard!

Iweje haya maandamano ya kisiasa sijui ya kusifia yaruhusiwe...
Maendeleo yanakuja waendelee kujigalagaza na kupiga pushup korosho ikilimwa Kilimanjaro sijui watapata pa kutokea
 
Back
Top Bottom