Wanachama wa CCM Ruvuma wacheza ngoma kumpongeza Magufuli!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,640
2,000
Mkoani Ruvuma wanachama wa ccm wamejitokeza na kucheza ngoma, huku wanaume wa mkoani humo wakipiga push up na akina Mama kujigalagaza kwenye vumbi kwa kile walichodai ni kumpongeza Magufuli.

Tukio hilo lililopambwa na makada wa chama hicho kuvaa mavazi ya kijani na njano a.k.a yeboboyebo, wakina mama wakiwa wamevalia matisheti na kanga za msaada za rangi hizo, lilisindikizwa na akina baba waliovalia makofia ya kijani na matisheti ya kijani pamoja na suruali nyeusi lakini zikionekana zimechakaa sana ama kwa kuvaliwa kwa muda mrefu, au zikiwa pengine zimeokotwa kwenye madampo!

Wanachama hao ambao kwa wingi wao walivyoonekana wamekuwa kwa muda mrefu wakiandamwa na matatizo mbalimbali, kubwa likiwa ukosefu wa elimu (yaani ujinga), mengine ni barabara mbovu, kukosekana kwa maji safi, umaskini, huduma mbovu za afya n.k walikuwa wakisifia juhudi za magufulk za kupambana na ufisadi lakini huku wao wakiwa hajui ni jinsi gani matatizo yao tatakavyotatuliwa!

Lakini kimsingi haya waliyokuwa wakifanya ina maana siyo siasa zile Magufuli alizokataa mpaka 2020?

Kwani siasa za hadharani ni mpaka iwe mikutano ya hadhara, hizi ni double standard!

Iweje haya maandamano ya kisiasa sijui ya kusifia yaruhusiwe...
 

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,421
2,000
...lilisindikizwa na akina baba waliovalia makofia ya kijani na matisheti ya kijani pamoja na suruali nyeusi lakini zikionekana zimechakaa sana ama kwa kuvaliwa kwa muda mrefu, au zikiwa pengine zimeokotwa kwenye madampo!
Wanachama hao ambao kwa wingi wao walivyoonekana wamekuwa kwa muda mrefu wakiandamwa na matatizo mbalimbali, kubwa likiwa ukosefu wa elimu (yaani ujinga), mengine ni barabara mbovu, kukosekana kwa maji safi, umaskini, huduma mbovu za afya...
Umeharibu habari yako na ubavicha bavicha uliotukuka.
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,381
2,000
Haya yanayofanyika yananikumbusha mwaka 1990 wakati raisi Ally Hassan Mwinyi alipofunga Chuo kikuu kwa muda usiojukikana, baada ya kuwepo kwa mgomo wa muda mrefu. Karibu mikoa yote ikihamasishwa na wakuu wa mikoa na wilaya wananchi waliandamana kumuunga mkono na kumpongeza raisi kwa kufunga chuo kikuu na kuwatimua wanafunzi wote kwa muda usiojulikana.
Hayo ndio maajabu ya watz, chuo kinachozalisha wataalamu kinafungwa halafu wananchi wanahamasishwa waandamane kumùunga mkono na kumpongeza raisi kwa hatua hiyo.
Sitashangaa pia nikiona wananchi wanahamasishwa waandamane kumpongeza Mwakyembe kwa kulifungia gazeti la mawio kwa sababu ya kuwataja maraisi wastaafu ktk mikataba mibovu ya madini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom