Elections 2010 Wanachama wa CCM Mtibwa wanajuta....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Wanachama wa CCM Mtibwa wanajuta

Imeandikwa na John Nditi, Mvomero; Tarehe: 15th December 2010 @ 20:30

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mtibwa, Tarafa ya Turiani, Mvomero mkoani Morogoro, wamebainisha kuwa kupoteza kiti cha Udiwani Kata ya Mtibwa, kumechangiwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya wafanyakazi na wakulima wa nje wa miwa dhidi ya Menejimeti ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa, imeelezwa.

Mgogoro huo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, ulipata ufumbuzi wakati wa ziara ya Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa mgombea urais.

Baada ya pande hizo zilisainiwa mkataba wa maridhiano ya mbele ya Uongozi wa Serikali ya Wilaya, Mkoa na Taifa nchini.

Rais Kikwete alipokuwa Mtibwa wakati huo wa kampeni za urais, mwanzoni mwa Oktoba hiyo alitumia muda wake kwa kukutana na wawakilishi wa viongozi wa pande hizo kwa kushirikishwa na watendaji wa Serikali juu ya kumalizwa mgogoro huo na hatimaye kusainiwa kwa maridhiano ya pande hizo.

Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo , Suleiman Msasa, akizungunza kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Kidudwe pamoja na Madizini yaliyopo eneo la Kata hiyo, alisema kushindwa kwa CCM kumechangiwa na mgogoro huo.

Mkutano huo uliitishwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, kwa lengo la kutoa shukurani kwa wananchi wa kata mbalimbali za jimbo hilo kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa mbunge wao.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, kata hiyo ya Mtibwa haina wanachama wa kutosha wa kuitwa ni wapinzani dhidi ya CCM, bali alisema kilichojitokeza ni uasi wa baadhi ya wanaCCM waliowashawishi wananchi kutokipigia na badala yake waipigie kura Chadema kwa nia ya kuikomoa Serikali ya CCM.

“Lazima tujijutie sisi wenyewe…hapa Mtibwa hakuna upinzani…kilichotokea ni hasira za wananchi zilizochangiwa na mgogoro wa muda mrefu wa kiwanda, wafanyakazi na wakulima wa miwa …na pia kuiona Serikali haiwatendei haki katika hili,” alisema Msasa.

Alisema, Mbunge wa Jimbo la Mvomero, bado anakubalika na wananchi wengi katika jimbo hilo na kwamba, sura iliyojitokeza ya CCM kushindwa kwenye kata hiyo muhimu na ya kiuchumi katika Wilaya ya Mvomero hakumaanishi kuwa upinzani ni imara ndani ya Jimbo hilo.

“Tujiangalie wapi tumejikwaa …na sasa tufanye nini ili kukiletea chama ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao, kama tatizo ni kiwanda basi ni muda muafaka wa kulijadili jambo hili,” alisema.

“…wakulima wanalilia wapatiwe asilimia 25 zilizokuwa za Serikali ambazo alipewa tena mwekezaji na hivyo kumiliki asilimia 100, kitendo kinachowanyima wakulima kuwa na uwakilishi kwenye Bodi kutokana na kunyimwa kununua hisa hizo zilizokuwa za Serikali,” alisisitiza Msasa.

Kwa upande wake, Makalla akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Kidudwe na Madizini, alisema kati ya mikakati ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo ni pamoja na kulivalia njuga tatizo la Kiwanda cha Mtibwa.

Alisema, tatizo la wakulima wa miwa, wafanyakazi dhidi ya uongozi wa kiwanda hicho ni wa muda mrefu licha ya kupatiwa ufumbuzi wa mara kwa mara, lakini jibu la kudumu halijafikiwa ipasavyo.

Hivyo alisema jukumu lake kama mtetezi wa wananchi wa Jimbo hilo ni kuona mgogoro huo unamalizwa na moja ya hatua hizo ni kuhitajika kuwepo na wawekezaji wengine wa viwanda vya sukari eneo la Mtibwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom