Wanachama wa CCM mnaposhangilia ushindi mkumbuke kuwa kuna kipindi kigumu cha maisha kinakuja mbele yetu

Tumewazoea na Matamko na tabiri zenu kila siku zisizotimia.

People's power lazima iheshimiwe. Uchaguzi umefanyika salama kabisa,Pia kula zinahesabiwa mbele ya mawakala wenu,
Kwahiyo CHADEMA mlitegemea mtaishinda katika Uchaguzi huu??

I think you are too disappointed, Sababu mlikuwa na matarajio makubwa bila strategies zozote.
Mawazo finyu
 
Nyie ni Wapumbavu sana, Dunia nzima inaelewa na inathamini mchango na uongozi wa Magufuli. Hicho kipindi kigumu unachosemea umekaririshwa tu, miaka mitano iliyopita tuli survive vipi?, Au ulikuwa nje ya nchi?

Umiza kichwa maisha ndo yalivyo, hakuna Rais atakayekuja kuwaletea mkate mezani. Upinzani wa kupinga kila kitu bora utokomee kuzimu tu. Mmedanganywa na wanasiasa eti tunataka maendeleo ya watu sio vitu na nyie mkazungusha viuno.

Ila nawashukuru sana wananchi sio wajinga wamewanyoosha kwenye box la kura na huyo mnyoa panki wenu. Narudia wananchi sio wajinga wanaona aliyoyafanya Magu heshima ya mwananchi wa kawaida umerudi kipindi hiki cha Magu. Watu wamesogezewa huduma muhimu nyie mnabeza eti maendeleo ya vitu, nani awape kura?
Mawazo finyu
 
Wewe ni Nani kuyazungumzia haya kwani hii dunia ni yako .....kwani hii dunia ni yako we kidera
 
Mimi bado kijana mdogo, around 31. Nimeanza kujitegemea 2015. Nishajenga dar na nina usafiri wa uhakika. Ni mtumishi wa umma. Hivyo sina maisha magumu kivile.
Nimezungumza kwaajili ya umma wa Kitanzania
Kijana hivyo vinyumba na kagari ulichonacho sio kitu kupotea ni maramoja sasa kuja kuvirudisha kwa mfumo huu mpya itakuwa kazi Omba sana Mungu acha majivuno
 
Fanyeni kazi kwa bidii, acheni kulialia hapa kazi tu.Tundu Lissu anzisha chama chako,achana na hilo genge la wahuni.
 
Habari,

Kuna watu wanajua ila wanajisahaulisha kuwa nchi za Magharibi ndizo zinazotusogeza mbele au kutusapoti kwenye sekta ya Afya na Elimu kwa kiasi kikubwa.

Hii iko wazi miaka na miaka.

Watu wa Magharibi hakuna kitu wanajali kama Demokrasia ambayo imeminywa kwa miaka 5 yote ya Magufuli. Akaachia miezi 2 ya campaign na jana umefanyika uchaguzi wa kiini macho.

CCM wameshinda kwa kishindo. Hiki kishindo haramu kitawafikia sponsors huko Ng'ambo na ndipo watajitoa kusapoti mambo muhimu. Hapo tutaanza kuuziwa huduma zote za afya kwa bei kamili. Hapo ndipo elimu yetu itatikisika.

Uchumi utayumba, hapa mwananchi wa kawaida, mtumishi wa umma wa kawaida, mfanyabiashara mdogo na wa kati, mkulima n.k lazima ataisoma.

Tushangilie na kupongezana ila tutambue kuwa kikija kipindi kigumu hao viongozi wakuu hawatapata taabu.
Watz wanaipenda sana ccm
 
Back
Top Bottom