Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,372
- 6,078
Tarehe 12 July mwaka 2015 huko Dodoma alikamatwa mtu mwenye asili ya kiasia akiwa na mabilioni ya fedha za kitanzania ambazo inasemekana mmoja wa ugombea urais alikuwa na mpango wa kuwanunua wajumbe ili wamchague awe mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
Kitendo kile kililetea sifa mbaya sana CCM kiasi ambacho ni mojawapo ya sababu katika uchaguzi wa 2015 CCM ilipata wakati mgumu katika kampeni zake.
Sasa hivi Mwenyekiti wa CCM John Magufuli ameonyesha wazi anachukia rushwa ki kweli kweli, ni wajibu wenu kama wanachama kumsaidia katika kuchagua viongozi wazuri wenye elimu, wasio na dosari yeyote na wanaochukia rushwa ili apate wasaidizi wazuri katika kuijenga Chama cha Mapinduzi kipya.
Tayari kuna malalamiko kwenye chaguzi za wilaya na kata kuna baadhi ya viongozi wamejaribu kutumia rushwa kwenye chaguzi zilizofanyika.
Naomba uongozi mkuu wa CCM makao makuu kuwaijibisha wasimamizi wote wakiwemo makatibu wa wilaya ama mkoa kama itabaiinika wameruhusu rushwa kutumika kwenye chaguzi zinazokuja ngazi za mikoa.
Tanzania Bila Rushwa Inawezekana.