Wanachama 92 wa CCM watimkia TLP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachama 92 wa CCM watimkia TLP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Sep 11, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) katika Wilaya ya Arusha, kimepata pigo kubwa baada ya viongozi na wanachama wake 92 kuamua kujiunga na TLP.

  Wanachama hao walipokelewa juzi katika ofisi za TLP Kata ya Sokoni katika hafla iliyohudhuriwa pia na viongozi wa vyama vya upinzani mkoani Arusha.

  Wanaccm hao wa CCM wanatoka katika Kata ya Sokoni yenye idadi kubwa katika Manispaa ya Arusha na inayowakilishwa na Diwani wa TLP, Michael Kivuyo tangu mwaka 2000.

  Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi za TLP na kurejesha za CCM, viongozi hao na wanachama hao walisema wameamua kujiondoa katika chama hicho baada ya kuona kuwa viongozi wa CCM mkoani Arusha hawana dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi.

  Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Muriet, Salma Jumanne ambaye pia alikuwa katibu wa jumuiya ya wanawake wa CCM tawi hilo, alisema uamuzi wa kujiondoa CCM unalenga katika kutafuta chama mbadala ambacho viongozio wake watawasaidia wananchi.

  “Tumeona kwamba viongozi wa CCM mkoani Arusha, hawana mikakati bora ya maendeleo kwa wananchi, ni watu waliojawa na ubinafsi," alidai mwanachama mwingine.
  Sourc:Mwananchi.

  Huku Arusha bahati mbaya wakazi wake wengi hawana habari na CHADEMA.
  Mpambano ni baina ya CCM na TLP.Kata ya Sokoni na Sombeti inawapiga kura wengi na mara zote ukitaka kushinda kiti cha ubunge Arusha ni kuhakikisha unashinda hizi kata mbili.

  Tusisahau hakuna cha operesheni Sangara wa Zinduka wala hakuna kiongozi yoyote wa ngazi ya juu aliyehusika na zoezi la kuigaragaza CCM.Somo kubwa kwa wapinzani ni ushirikiano kwasababu kila chama kuna mahali kinakubalika zaidi ni vyema na busara kukubali na si kuparurana na kutoa nafasi kwa CCM kupita kwa urahisi.
   
 2. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh siasa bwana ni mchezo wa ajabu sana wako watu wameshaizika TLP na kuisahau kabisa lakini bado kinajikongoja mtakuja shangaa uchaguzi mkuu mambo yakavyowaendea vizuri.Hapa jamvini kuna watu wandhani siasa za upinzani ni chadema tu hata mijadala ya hapa jamvini imetawaliwa na uchadema chadema.

  Uchaguzi wa Chadema umedhiirisha kumbe nacho kina mapungufu kuliko watu walivyokuwa wakiifikiria.Kitendo cha kumwengua bwana mdogo Zitto kitakuwa na athari kubwa kuliko wazee wa Chadema walivyofikiri,Zitto ana uwezo mkubwa zaidi ya Mbowe nashindwa kuelewa ni kwanini wazee wa chadema wakiongozwa na Mzee Mtei walitanguliza maslahi ya familia zaidi kuliko chama.Chadema kwasasa kimekaa kama vile NGO ya watu fulani na si chama cha siasa.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wasiishie kuhama tu, bali kuendelea kuhamasisha mageuzi zaidi na kwa wananchi wengine na pia kuhakikisha wanapiga kura kwa mwamko huo huo na kwa wingi zaidi come 2010!
   
 4. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Next Level heshima mbele
  kuhama nayo ni hatua muhimu sana katika kuhakikisha jahazi la hawa mafisadi na chama chao wanaendelea kupata bakora hata kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

  CCM wanajua kwamba kata za Sombetini,Sokoni na Lemara zinawapiga kura wengi,hivyo kupoteza viongozi ambao pia ni wapiga kura na waamasishaji wakubwa ni pigo kubwa sana tena hasa baada ya kumnunua diwani wa TLP Mawzo Nelson ambaye sasa hana tena nguvu alizokuwa nazo mwanzo.

  Jimbo la Arusha kwa asilimia kubwa limeshawatoka CCM wanalijua hilo hasa baada ya mbunge F Mrema kutafuna fedha za ujenzi wa zahanati kata ya Sombeti.
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hao wote watarudi CCM muda si mrefu,tena kwa kutangazwa kwenye Tv.Imekuwa kamchezo kakuhamahama.
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Msimu wa mavuno ushawadia hii hama hama itakuwepo sana watu wapate riziki zao. Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake
   
 7. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata humu JF hujagundua!! post zinavyoletwa kwa mtindo wa kiutatanshi!
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hawa wamehama chama kumfuata mtu (siyo kutafuta chama mbadala). TLP? Nyerere aliwahi kutabiri kwamba hivi vyama vitakufa na vitakavyobaki ni CUF, CHADEMA, UDP & CCM.
   
 9. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako Magreth unapenda kusoma habari za Chadema tu habari nyingine lazima utasema zimekaa mtindo wa utatanishi

  Nani kakwambia wamemfuata mtu soma kwanza kabla ya kurukia mada.L A Mrema hakuwepo wala kiongozi yoyote wa ngazi ya juu.Hoja yako kwamba wamemfuata mtu haina mashiko hata kidogo.Wakaazi wengi wa Arusha hawawezi kwenda Chadema kwasababu wanajua si chama cha siasa bali NGO ya kina Ndesamburo na Mtei family & Co.

  Mambo mangapi Nyerere alisema yakajakuwa uongo au unataka nikuorodheshee ?.
  A.Umesahau Nyerere alimtembeza Mkapa nchi nzima kasoro Arusha akimnadi kwamba ni Mr Clean ?.
  B.Umesahau Nyerere baada ya vita vya Uganda alilitangazia taifa miezi 18 ya kujifunga mkanda ikajakuwa miaka 18 ya shida na taabu ?.

  Mkuu Cynic si kila jambo alilosema Nyerere lilitokea kuwa kweli tukiamua kutoa orodha ya mambo nakwambia utashangaa jinsi huyu baba wa taifa alivyotuzuga watanzania.


  Hivi Nyerere alijua Chadema itakuja kuwa chama cha ukoo na ukanda ?,nina hakika Nyerere angekuwa hai angeshauri Chadema ifutwe katika daftari la msajili wa vyama vya siasa isijeikaiingiza Tanzania kwenye ukabila na udini.
   
 10. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Masatu mlivyomchukua Lwakatare wa CUF mbona ukusema kafuata riziki ?.Tatizo hapa jamvini kila kitu chadema hamtaki kuamini kwamba kuna wananchi hawana habari na hiyo NGO yenu.

  Watu wanaojiunga na Chadema ukichunguza sana utakuta wanawafuata watu si sera nzuri hata kidogo.Mfano mzuri ni ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 iliweka wazi wataanzisha mahakama ya kadhi lakini wakristo wangapi waliisoma ilani ya CCM ?? laiti wangeisoma unadhani CCM ingepita au ingeshinda kwa kishindo.Wapiga kura wengi hawaangaiki kusoma sera za vyama kama baadhi ya wachangiaji wanavyotaka kutuaminisha.
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Mimi pia nimeukana uraia na kujiunga na republican party.
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Heh hehe heeee! hii mpya leo.... anyway Lwakatare tumemchukua kwa sababu ya njaa yake tu tena kama hajui kuwa ameingia choo cha kike!
   
 13. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Masatu umesema kweli Lwakatare kaondoka chama makini kakimbilia NGO ajabu bado anajiita mwanasiasa !.Nasikia Mtuhuru alimwahidi kumsaidia kulipa gharama za kesi yake na Kagesheki.Bila shaka katika kipindi kifupi alichokaa Chadema atakuwa amegundua amefanya kosa kubwa na nafasi ya kusahihisha hakuna tena.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hawa lazima wana matatizo au ni ulaji umewavuta!!!

  Na mie nahama kabila kabisaaa yaishe maana msimu wa mavuno unakuja
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Sherehe za kuwapokea wanachama wapya zilihudhuriwa na viongozi wote wa vyama vya upinzani [NCCR-MAGEUZI,CUF na UDP].

  Vyama vya upinzani katika level ya wilaya na mkoa vinaushirikiano mzuri tatizo linaanza kwa viongozi wa ngazi ya taifa.Nimetembelea sehemu wilaya nyingi sana Tanzania nimegundua umoja ndani ya vyama vya upinzani unakwamishwa na baadhi ya viongozi wa wachache wanaojiona wana uwezo wa kukabiliana na CCM bila kuhitaji umoja wa vyama vingine.

  Niliwahi kuwalaumu viongozi wa CHADEMA kwa kitendo chao cha kumpokea kiongozi wa CUF kwa mbwembwe na nderemo kubwa utadhani Lwakatare katokea CCM kumbe katoka chama kingine cha upinzani.Viongozi makini wa CHADEMA kama Dr Slaa alishiriki katika mchezo mchafu wa kumpokea Lwakatare,ingekuwa Zitto au Mbowe nisingeshangaa lakini kwa mpiganaji mahiri kama Dr Slaa kwa kweli ilikuwa ni pigo kubwa kwa kambi nzima ya upinzani.
   
Loading...