Wanachama 171 wa CHADEMA wachukua, kujaza na kurejesha fomu za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi mbalimbali 109

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,793
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Jumla ya wanachama 171 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamechukua, kujaza na kurejesha fomu za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi mbalimbali 109, za uongozi ngazi ya taifa ndani ya chama na katika mabaraza yake, Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) na Baraza la Wazee Chadema.

Baada ya shughuli ya uchukuaji, ujazaji na urejeshaji wa fomu kukamilika na kuwasilishwa Makao Makuu ya Chama, zoezi la kuzichambua fomu hizo tayari limeanza, kuelekea vikao vya vya chama vitakavyoketi kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi mkuu ndani ya chama.

Vikao hivyo vya mchujo na uteuzi vitaanza kwa Sekretarieti ya Makao Makuu ya Chama kuketi na kufanya uchambuzi utakaowasilishwa na mapendekezo kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama itakayoketi kwa ajili ya kufanya uteuzi wa wagombea, ambapo siku ya Jumamosi, Disemba 7, 2019, Kamati Kuu itakutana kufanya uteuzi wa wagombea wa mabaraza ya Chama, kisha itaketi tena Disemba 16, mwaka huu, kuteua wagombea wa nafasi za uongozi wa Chama ngazi ya taifa.

Wakati huo huo, uchaguzi za kuwapata viongozi wa ngazi za kanda 10 za Chama, uliokuwa umepangwa kufanyika kuanzia Novemba 28 hadi Disemba 1, mwaka huu, umekamilika rasmi jana kwa mujibu wa ratiba, wakipatikana jumla ya viongozi 29, ikihusisha nafasi ya Uenyekiti wa Kanda, Makamu Mwenyekiti wa Kanda na Mweka Hazina wa Kanda. Viongozi waliopatikana kwenye kanda zote na nafasi zao ni kama ifuatavyo;

1. KANDA YA SERENGETI (Simiyu, Mara na Shinyanga)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Esther Nicholas Matiko (Mb)
ii. Makamu Mwenyekiti ni Gimbi Dotto Massaba (Mb)
iii. Mweka Hazina ni Maendeleo Bernard Makoye

2. KANDA YA VICTORIA (Mwanza, Kagera na Geita)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Ezekia Dibogo Wenje
ii. Makamu Mwenyekiti ni Sylvester Makanyaga
iii. Mweka Hazina ni Upendo Peneza

3. KANDA YA PEMBA (Kaskazini Pemba na Kusini Pemba)

i. Mwenyekiti wa Kanda Hafidh Ali Saleh
ii. Makamu Mwenyekiti wa Kanda Time Ali Suleiman
iii. Mweka Hazina Ali Khamis Ali

4. KANDA YA UGUNJA (Kaskazini Unguja, Mjini Magharibi na Kusini Unguja)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Said Mzee Said
ii. Makamu Mwenyekiti wa Kanda ni Hassan Abeid
iii. Mweka Hazina wa Kanda ni Asiata Said Abubakari.

5. KANDA YA KUSINI (Ruvuma, Lindi na Mtwara)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Seleman Mathew
ii. Makamu Mwenyekiti ni Salum Khalfan Barwan
iii. Mweka Hazina ni Mario Efrem Millinga

6. KANDA YA NYASA (Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe na Rukwa)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Peter Msigwa (Mb)
ii. Makamu Mwenyekiti wa Kanda ni Joseph M. China
iii. Mweka Hazina wa Kanda ni Aida Khenan (Mb)

7. KANDA YA PWANI (Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala na Pwani)

i. Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti utarudiwa
ii. Makamu Mwenyekiti ni Baraka Mwago
iii. Mweka Hazina ni Dkt. Michael Mtaly

8. KANDA YA KATI (Dodoma, Singida na Morogoro)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Lazaro Samwel Nyalandu
ii. Makamu Mwenyekiti ni Aisha Yusuf Luja
iii. Mweka Hazina ni Devotha Minja (Mb)

9. KANDA YA MAGHARIBI (Tabora, Kigoma na Katavi)

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Gaston Shundo Garubindi
ii. Makamu Mwenyekiti ni Masanja Katambi Musa
iii. Mweka Hazina ni Aidan Ndowa

10. KANDA YA KASKAZINI

i. Mwenyekiti wa Kanda ni Godbless Jonathan Lema (Mb)
ii. Makamu Mwenyekiti ni Yosepher F. Komba (Mb)
iii. Mweka Hazina ni Anna Joram Gidarya (Mb)

Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ya Mwaka 2006, Toleo la Mwaka 2016, pamoja na majukumu mengine yaliyoainishwa na Katiba, Mwenyekiti wa Kanda ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Makamu Mwenyekiti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama katika kanda husika.

Imetolewa leo Jumanne, Disemba 3, 2019 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
 
Tunataka mwenyekiti mpya

Huyu wa sasa amevuna vya kutosha
Kwani wewe ni CHADEMA? Ni lazima uchangie kila uzi unaoanzishwa? Au ndio source pekee ya income unayoitegemea kwa sasa?
Angalia namna nyengine ya kujipatia kipato ndugu. Unachokifanya kwa sasa ni aibu!
 
Huyo M/Kiti amevuna nini kutoka kwako na mbulula wa Lumumba!!???
Tulia uone mziki wa CDM 2020 Utaipenda!!
 
Back
Top Bottom