Wanachadema tuhojiane kwa hekima

Mleta mada umetuwakilisha wengi......inasikitisha sana chadema ya leo, hakuna way foward.
Mie nilitamani (siko kwenye vikao) wakati wa kumkaribisha mamvi kwakuwa ilikuwa ni kama mchezo wa ku bet basi wangekubaliana japo kwa siri kuwa ikiwa mamvi atashindwa uchaguzi mkuu astaafu siasa then sie kama chama tungeendelea kuwa hai kwa kushambulia badala ya sasa mbali ya kushambuliwa (hoja) na ccm lakini pia tunakosa hoja kabisa
Hapana shaka, sasa Chadema nao watakuja na sera ya kujivua gamba la sivyo CCM itawaumiza 2020
 
Brother...chadema yetu siku hizi imevamiwa na kundi la ccm la kina lowasa.

Binafsi nampongeza mtoa hoja...amehoji mambo ya msingi sana...ndio demokrasia yenyewe...watu waweze kutoa hoja popote pale na wajibiwe kwa hoja...unavyodai eti angesemea kwenye vikao...huna tofauti na wale wanaomwambia kakobe asikosoe kiuwazi aende sirini.

Chadema...imedanganywa na lowasa kuwa ameongea na magu ...waende tu kwenye uchaguzi..na utakuwa huru na haki.hautavurugwa.

Hivi seriously...kweli tuendelee kushiriki chaguzi kwa hisani ya ccm.

Maamuzi ya chadema kususia yalipongezwa kila kona ya nchi...na ulikuwa ni wakati wa kuanzisha movement kubwa kuhusu tume huru na katiba.

Ghafla...wanaamua kushiriki uchaguzi...kipi hasa kimerekebishwa...namaanisha kipi tangible.

Kushiriki uchaguzi huu ni kuendelea kuwapa ccm uhalali wa kutawala...na sababu ya kutojali hoja ya tume huru...zaidi inawajenga zaidi serikali ya ccm kwenye macho ya watu na jumuiya ya kimataifa kwamba kuna demokrasia..tume huru na madai ya lissu ni ya kipuuzi.

Ifike mahali tuseme ukweli lowasa na mbowe ni tatizo pale chadema...chama kimekuwa hakina msimamo ...usanii usanii tu kama lowasa
Sijui nini kimemkuta Mbowe, Lowassa kwenda Ikulu ilikuwa ni sababu tosha ya kuagana naye na kuanza kuwarudishia imani wanachama. Kweli pesa ni ibilisi.
 
Bora hao wenzenu hata hiyo kamati kuu ilikaa, nyie c mliwateua juu kwa juu kutokana na ahadi ya ile biashara.

Yaani umeumiaa na kuamua jana ujiunge na jamii forum ili ulete hz Propaganda mfu.

Kama wagombea wenu wako vizuri, bhasi tulieni wakapambane na kina Salum Mwalimu.

Inawezekana hao Chadema waliwachezea mind game kama za Mourinho na Babu Fergue enzi zileee, sasa na nyie mkawaamini mkapeleka front line hao viazi waliomuunga mkono Presidaa kwa hiari yao kuachia ubunge.

Sasa mnaona baada ya kutaja kikosi chenu na hawa wasusaji wameleta watu wanaoonekana kutishia Vimala. ....mlivyovipeleka Kwa wananchi mnaanza kuweweseka. Pambaneni na hali zenu mana mna mbinu nyingi, hata vyombo vingi vileeeeee vipo upande wenu.

Ni hayo tu, naomba kuwasilisha.

Unatia aibu.
 
Unatia aibu.
Ulipenda nifuate mtazamo wako eeh? Kila mmoja ana mtazamo wake. So pambana na hali yako mkuu, kama vipi jenga hoja tukupime kama hoja zako zina mashiko au kama zile with no legs to stand. Nb: If you think Properly, you will understand Properly.
 
Hongera sana kwa kuhoji na umehoji mambo ya msingi sana na hoja zako ziko wazi kabisa. Umesema ww ni mwanachama wa cdm na wengine wanaogopa kuhoji. Je hapa ulipohoji ww ni kwenye vikao vya cdm? Kuna tofauti gani na unaowalaumu wanaogopa wakati ww mwenyewe umehoji kwa fake ID?

Sawa ni kweli cdm wamewapitisha hao wagombea kwa makosa kama ccm, hata mimi hili kwangu ni ukakasi na huo ni udhaifu wa dhahiri kwa hili cdm wajitathmini. Umesema sababu walizozilalamikia hazijarekebishwa, umeambiwa zinarekebishwa lini kisha cdm ndio waanze kushiriki? Katika nchi za kiafrika walioko madarakani huwa wanarekebisha mambo bila kuonyeshwa upinzani wa wazi na hata machafuko? Hicho kitendo cha kususia kina impact hata kama ww kwa sababu zako hukubaliani nazo. Nilitaraji ungeweka ni mbinu gani itumike badala ya kutetea kwa kusema kwamba walicholalamikia hakijarekebishwa, na unaona ni sifa kabisa kwamba waendelee kususia. Kama cdm hawafanyi unavyotaka unaonaje ukaanzisha chama chako kikafanya unavyotaka ww? Kama mwanachama wa cdm umetibu watu wangapi waliojeruhiwa kikatili mpaka leo uone ni sawa kufanyiwa ukatili bila kutuma ujumbe maridhawa kwamba kuna shida?

sio lazima kujibu kila thread
 
Brother...chadema yetu siku hizi imevamiwa na kundi la ccm la kina lowasa.

Binafsi nampongeza mtoa hoja...amehoji mambo ya msingi sana...ndio demokrasia yenyewe...watu waweze kutoa hoja popote pale na wajibiwe kwa hoja...unavyodai eti angesemea kwenye vikao...huna tofauti na wale wanaomwambia kakobe asikosoe kiuwazi aende sirini.

Chadema...imedanganywa na lowasa kuwa ameongea na magu ...waende tu kwenye uchaguzi..na utakuwa huru na haki.hautavurugwa.

Hivi seriously...kweli tuendelee kushiriki chaguzi kwa hisani ya ccm.

Maamuzi ya chadema kususia yalipongezwa kila kona ya nchi...na ulikuwa ni wakati wa kuanzisha movement kubwa kuhusu tume huru na katiba.

Ghafla...wanaamua kushiriki uchaguzi...kipi hasa kimerekebishwa...namaanisha kipi tangible.

Kushiriki uchaguzi huu ni kuendelea kuwapa ccm uhalali wa kutawala...na sababu ya kutojali hoja ya tume huru...zaidi inawajenga zaidi serikali ya ccm kwenye macho ya watu na jumuiya ya kimataifa kwamba kuna demokrasia..tume huru na madai ya lissu ni ya kipuuzi.

Ifike mahali tuseme ukweli lowasa na mbowe ni tatizo pale chadema...chama kimekuwa hakina msimamo ...usanii usanii tu kama lowasa

Mkuu nakubaliana na hoja zako kwa kiwango kikubwa. Sasa twende hoja kwa hoja. Huyu mleta hoja kasema yeye ni mwanachama na wengine wanaogopa kuhoji ili yeye haogopi. Je haogopi hapa jukwaani kwa kutumia fake ID au alipaswa kuhoji akiwa ndani ya vikao ndio kudhibitisha sio muoga? Mimi sio mwanachama wa chadema bali ni shabiki hivyo naweza kuhoji hapa jukwaani. Ni kweli kususia uchaguzi ilikuwa ni kwa ajili ya mambo yarekebishwe hilo sikatai. Je ni lini unatarajia yatabadilishwa lini ili cdm washiriki? Cuf wamesusia uchaguzi huko Znz, je kuna lolote la maana uliloona limetokea? Waliosusiwa wanampango wowote wa kurekebisha au wangalau wanatafuta maridhiano?

Je baada ya kususia wangalau wewe umependekeza nini kifanyike au ni kususia tu mpaka wao wapende kurekebisha hizo kasoro.? Hivyo movement kubwa unayoisema ulipanga au ulitaka ianze lini maana kwenye michango yako sijawahi kuona ukipanga siku ya kuanza hilo. Nilitarajia ili nione mfano wangalau kwako ungeenda mahakamani kufungua mashitaka kwa ule ukatili uliofanyika. Naomba uniambie kipi kifanyike na wewe umeshafanya nini mpaka sasa ili hilo tatizo la tume kuibeba ccm lifikie mwisho?

Kwa hili la kwamba Lowassa hafai kuendelea kuwa mshauri wala kupewa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya cdm halina ubishi, na hili halikuanza leo bali ni toka alipoingia cdm. Sijafurahishwa na utaratibu wa kumpata huyo mgombea wa Kinondoni kwani hakuna tofauti na upatikanaji wa wagombea wa ccm. Mbowe kwangu naamini amefanya kazi nzuri, ila kwangu demokrasia nzuri kwa viongozi wa kuchaguliwa haipaswi kuzidi miaka 10. Hili iwe ni kwa rais, mbunge, diwani ama yoyote wa aina hiyo. Hivyo kwa Mbowe ni muda sahihi kupisha wengine ili kuiishi demokrasia.
 
Makamanda nawasalimu kwa salamu zote za chama, people's........!! Kuna suala la msingi leo naomba TUHOJIANE na TUHOJI viongozi wetu na hasa hawa wanao itwa "wa kamati kuu". Ni kupitia viongozi hao hao, chama chetu (CHADEMA) kilitangazia watanzania kwamba kimesusia uchaguzi mdogo uliopita kwa sababu ya kasoro zilizojitokeza ikiwemo uvunjwaji wa haki za kibinadamu, Demokrasia kuchezewa na rafu nyingi za kisiasa.

Katika lawama zile nakumbuka wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa walibebeshwa mzigo wa lawama. Wanachama tuliaminishwa kuwa kushiriki uchaguzi bila kero za msingi kutatuliwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, na tulikubali hivyo. Tuliiamini kamati kuu na viongozi wengine wa chama, tukawa watiifu, siku zikapita, uchaguzi ukapita, CCM wakapeta!!

Baada ya muda kupita, chama cha Mapinduzi, CCM, kikatangaza kuwapitisha wagombea wake wa majimbo ya Siha na Kinondoni bila kupitia mchakato muhimu wa kidemokrasia wa kupigiwa kura na wajumbe husika. Chadema tukalibeba suala hilo kama agenda na hoja yetu. Viongozi wetu wakalalamika utaratibu huo kuwa siyo halali, haufai, umepoka haki za wengi na kadhalika. Wanachama wengi wakaamini CCM ilifanya ujinga!!

Tobaaaaaaaaa!! Leo, taarifa ya kamati kuu ya Chadema kupitia kiongozi wetu John Mrema ina sema hivi;

"Kamati Kuu ya CHADEMA imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018" Taarifa hiyo ina endelea kwa kusema MAAJABU yafuatayo;

"Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1. Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma. (Tukumbuke huyu ni naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, ni nafasi ya juu sana ndani ya chama chochote cha siasa).

2. Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi.

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018, kwa ajili ya uteuzi.

SASA TUJITATHMINI NA TUJIULIZE WANA CHADEMA WENZANGU:

Ni jambo jema sana kamati kuu kuamua kushiriki uchaguzi huu,

1. Tulitumia vigezo gani kususia uchaguzi wa marudio kule Songea na Singida pamoja na maeneo mengine?? Vigezo hivyo kwenye uchaguzi huu wa Siha na Kinondoni havihusiki??

2. Kamati kuu imeamua kuteua yenyewe moja kwa moja kama kamati kuu ya CCM?? Ikiwa tuliiponda na kuishambulia CCM kwa aina ya uteuzi ambayo na sisi tumeufanya, CCM wana tuonaje sisi?? Ikumbukwe kuwa chama chetu kina itwa "Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo", mpaka hapo demokrasia tuliyo ipigia kelele kwa wana CCM iko wapi kwetu??

3. Kilicho fanya chama changu Chadema kikasusia uchaguzi mdogo uliopita, ni nini?? Je, yaliyo lalamikiwa yame pata ufumbuzi kwenye majimbo haya ya Siha na Kinondoni mara hii?? Tumepata tume huru ya uchaguzi?? Tuna uhakika kwamba wakurugenzi na wakuu wa wilaya na mikoa hawataingilia uchaguzi huu kwa namna yoyote??

4. Ni lini kamati kuu imetoa mrejesho wa faida ya chama chetu kususia uchaguzi wa marudio kwa jimbo la Singida na Songea?? Je, baada ya kususia, serikali ilichukua hatua zozote?? Tume ya uchaguzi imebadilishwa?? Wakuu wa mikoa na wilaya wame badilishwa na kwamba hawana "nasaba" za CCM??

Yamkini kulikuwa na sababu nyingine ya kususia uchaguzi mdogo uliopita na siyo zile sababu tulizo aminishwa!! Kuna wanachama wengine hawapendi kuhoji, ni waoga, hawana uwezo mpana wa kukifikiria chama kitaaminiwa vipi baadae, wao kila suala ni kukubali tu kwa sababu limetoka kamati kuu, I will never be part of them. Kuna mahali chama kimepwaya, Chadema ya sasa haiko sawa kiuongozi na kimikakati, huu ndiyo ukweli usio pendwa na wengi. Tukikosoa kuna wajinga watasema tuna nunuliwa, tukikaa kimya tuna onekana wote hatuna uwezo wa kuhoji, HAPANA, nimechagua kuhoji na huu ndiyo uzalendo wa kweli kwa taifa na chama changu.

TUJITATHMINI, TUJIKOSOE, TUJISAHIHISHE.
CDM hakuna mwanachama mwenye issue za kike kike kama wewe mkuu

Tuliza mshono dawa ikuingie tunavyochukua majimbo
 
Kuna sehemu niliandika hii kamati kuu ni masifuri ama hawafikiri kwa umakini.
Sioni chochote kilichobadilika toka tususie chaguzi ndogo za Singida,Longido na Songea.
Wameamua kwenda kuidhalilisha chama maana watapigwa kipigo cha mbwa mwizi na sijui watasemaje safari hii maana wanajua matokeo kabla ya kuchukua fomu.
Wanawafanya wale wagombea wa majimbo ya Longido ,Songea na Singida wajione kama hawajathaminiwa kabisa.
Hebu fikiri mgombea wa Longido alipambana na kesi kwa gharama zake mwenyewe mwishoni unamnyima kugombea na bila sababu nyingine ya msingi unawaruhusu wengine wagombee,huo si ujuha?
Mi naona kama Mbowe ameamua kuhalalisha matumizi yake binafsi kwa ruzuku ya chama
 
Makamanda nawasalimu kwa salamu zote za chama, people's........!! Kuna suala la msingi leo naomba TUHOJIANE na TUHOJI viongozi wetu na hasa hawa wanao itwa "wa kamati kuu". Ni kupitia viongozi hao hao, chama chetu (CHADEMA) kilitangazia watanzania kwamba kimesusia uchaguzi mdogo uliopita kwa sababu ya kasoro zilizojitokeza ikiwemo uvunjwaji wa haki za kibinadamu, Demokrasia kuchezewa na rafu nyingi za kisiasa.

Katika lawama zile nakumbuka wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa walibebeshwa mzigo wa lawama. Wanachama tuliaminishwa kuwa kushiriki uchaguzi bila kero za msingi kutatuliwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, na tulikubali hivyo. Tuliiamini kamati kuu na viongozi wengine wa chama, tukawa watiifu, siku zikapita, uchaguzi ukapita, CCM wakapeta!!

Baada ya muda kupita, chama cha Mapinduzi, CCM, kikatangaza kuwapitisha wagombea wake wa majimbo ya Siha na Kinondoni bila kupitia mchakato muhimu wa kidemokrasia wa kupigiwa kura na wajumbe husika. Chadema tukalibeba suala hilo kama agenda na hoja yetu. Viongozi wetu wakalalamika utaratibu huo kuwa siyo halali, haufai, umepoka haki za wengi na kadhalika. Wanachama wengi wakaamini CCM ilifanya ujinga!!

Tobaaaaaaaaa!! Leo, taarifa ya kamati kuu ya Chadema kupitia kiongozi wetu John Mrema ina sema hivi;

"Kamati Kuu ya CHADEMA imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018" Taarifa hiyo ina endelea kwa kusema MAAJABU yafuatayo;

"Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1. Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma. (Tukumbuke huyu ni naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, ni nafasi ya juu sana ndani ya chama chochote cha siasa).

2. Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi.

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018, kwa ajili ya uteuzi.

SASA TUJITATHMINI NA TUJIULIZE WANA CHADEMA WENZANGU:

Ni jambo jema sana kamati kuu kuamua kushiriki uchaguzi huu,

1. Tulitumia vigezo gani kususia uchaguzi wa marudio kule Songea na Singida pamoja na maeneo mengine?? Vigezo hivyo kwenye uchaguzi huu wa Siha na Kinondoni havihusiki??

2. Kamati kuu imeamua kuteua yenyewe moja kwa moja kama kamati kuu ya CCM?? Ikiwa tuliiponda na kuishambulia CCM kwa aina ya uteuzi ambayo na sisi tumeufanya, CCM wana tuonaje sisi?? Ikumbukwe kuwa chama chetu kina itwa "Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo", mpaka hapo demokrasia tuliyo ipigia kelele kwa wana CCM iko wapi kwetu??

3. Kilicho fanya chama changu Chadema kikasusia uchaguzi mdogo uliopita, ni nini?? Je, yaliyo lalamikiwa yame pata ufumbuzi kwenye majimbo haya ya Siha na Kinondoni mara hii?? Tumepata tume huru ya uchaguzi?? Tuna uhakika kwamba wakurugenzi na wakuu wa wilaya na mikoa hawataingilia uchaguzi huu kwa namna yoyote??

4. Ni lini kamati kuu imetoa mrejesho wa faida ya chama chetu kususia uchaguzi wa marudio kwa jimbo la Singida na Songea?? Je, baada ya kususia, serikali ilichukua hatua zozote?? Tume ya uchaguzi imebadilishwa?? Wakuu wa mikoa na wilaya wame badilishwa na kwamba hawana "nasaba" za CCM??

Yamkini kulikuwa na sababu nyingine ya kususia uchaguzi mdogo uliopita na siyo zile sababu tulizo aminishwa!! Kuna wanachama wengine hawapendi kuhoji, ni waoga, hawana uwezo mpana wa kukifikiria chama kitaaminiwa vipi baadae, wao kila suala ni kukubali tu kwa sababu limetoka kamati kuu, I will never be part of them. Kuna mahali chama kimepwaya, Chadema ya sasa haiko sawa kiuongozi na kimikakati, huu ndiyo ukweli usio pendwa na wengi. Tukikosoa kuna wajinga watasema tuna nunuliwa, tukikaa kimya tuna onekana wote hatuna uwezo wa kuhoji, HAPANA, nimechagua kuhoji na huu ndiyo uzalendo wa kweli kwa taifa na chama changu.

TUJITATHMINI, TUJIKOSOE, TUJISAHIHISHE.
mkuu hapo umenena vyema kabisa shida ni kwamba jiandae kuitwa msaliti na matusi mengine utayapata mmoja akitukana kama kawaida yao wote ni matusi tu hakuna kingine
 
Tatizo la chadema ni kupoteza mueleo baada ya kukosa cha kupigania
Tume iliosusiwa,ni ile ile,wakurugenzi ni wale wale na ma Dc na katiba ni ile ile.
Safari hii ccm watapeleke maguvu yote kuhakikisha wanashinda ili kuwafanya chadema wajione wapumbavu
 
Unaamini watu ni wajinga sana kwamba watajali ccm kushinda na sio kuangalia wameshindaje? Na toka lini kushindwa ikawa aibu? Iwapo ccm itashinda kwa kukiuka taratibu na sheria cdm watapataje aibu?

Nikuambie ukweli unaoumiza, hii ccm unayodanganywa ni imara haina tofauti na vyama vingine, bali nguvu yake iko ndani ya mwenyekiti wake ambaye ni amiri jeshi mkuu, hivyo anatumia cheo chake cha urais kuhakikisha chama chake kinafaidika. Siku rais anatoka nje ya ccm, kesho yake tu ccm itakuwa mortuary. Kwa hiyo unachojivunia hapa ww na wenzako sio kukubalika kwa ccm bali ni nguvu ya rais kuhakikisha chama chake kinashinda kwa vyovyote bila ridhaa ya wapiga kura.
 
Back
Top Bottom