Wanachadema siyo sehemu ya Watanzania?

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Kila jambo baya wanafanyiwa wana CHADEMA ama wanasingiziwa wao kulifanya.

CCM wakishindwa kutimiza ahadi zao wanasema kwa kuwa CHADEMA "wanapinga" wasitimize hizo ahadi zao.

Barricks wakisema kuwa wanataka kulipa "kishika uchumba" walichoahidi inasemwa kwamba wana-CHADEMA watanuna.

Bunge la Katiba kushindwa kuja na Katiba iliyopendekezwa na wananchi, shutuma zinatupiwa kwa CHADEMA/UKAWA kwa nini walisusia bunge hilo

Samweli Sitta akiwa amestaafu tena akiwa nje ya nchi akitibiwa, aliongezewa hela na serikali kwenye matibabu yake kwa hoja kwamba ni "Spika Mstaafu". Lakini Mwana-CHADEMA Lissu ambaye alishambuliwa akiwa kwenye kazi zake za kibunge ananyimwa fedha za matibabu kwa maelezo eti hakufuata utaratibu.

Hivi kuwa mwana-CHADEMA haki na sifa yako ya kuwa Mtanzania huwa inakufa?
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Tumeshaamniwa wao ndiyo waleta maendeleo na wakiamua hawayaleti na cha kuwafanya hatuna.

By Heri James mwenyekiti UVCCM
Wakati mwingine unajiuliza ni nani anaongoza nchi kati ya CHADEMA na CCM. Wanapokataa hoja ya Katiba Mpya wanasema kuwa haikuwa hoja ya CCM, bali Kikwete alikopa hoja ya Katiba Mpya toka CHADEMA na CUF.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom