Wanachadema na wanamageuzi tusitiswe na kelele za chura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachadema na wanamageuzi tusitiswe na kelele za chura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbaneingoma Zom, Mar 16, 2011.

 1. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida siku za hivi karibuni tumewaona viongozi wengi wa serikali ya CCM akiwemmo rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakihaha huku na huku kueneza propaganda ya udini na umwagaji wa damu, hili limekuja mara tu baada ya hotuba ya raisi ya mwisho wa mwezi ambapo alitunia muda mrefu kuzungumzia mwenendo wa chama cha democrasia na maendeleo chadema, kuwa kinahatarisha amani ya nchi ingawa hakuelezea ni kwa vipi chama hicho kinahatarisha amani ya nchi, kwa upande wake yale maandamano ya chadema, na kauli za umma kwamba walioko madarakani wameshidwa kufikia matarajio yao na kwamba umma unauwezo wa kuwafanya wajiudhulu ni kutishia amani. Huu ni uwezo mdogo wa kufikiri mambo kwa kina!!! kwani kama kuna rais nchi hii aelewwe kuwa umma ndio uliomweka madarakani na huo huo umma unauwezo wa kumng'oa madarakani ikiwa hakufikia matarajio ya wananchi. Kitendo cha serikali ya ccm kureact negatively katika madai ya wanchi kinaonyesha ufinyu wa uwezo wa kufikiri mambo. Sisi tulitegemea mwitiko wa raisi wetu ungekuwa wa kukabiliana na madai ya wanchi ya kupanda kwa gharama za maisha yaani umeme,sukari, usafiri na bidhaa karibu zote pia angejikita katika kuwaelewesha wanchi hatua zinazochukuliwa na serikali kuhusu sakata la dowans!! Lakini badala yake akaunyesha udhaifu wa serikali yake wazi kwa kutojibu hoja za wanchi zilizoko mezani na kuendelea kukipa ummaarufu chadema, jambo ambalo si baya kwetu wapenda mageuzi. haikuishia hapo sasa amewatafuta kasuku wengi kila kukicha utakuta anaamka kasuku mmoja na kuiga wimbo wa mwajiri wake eti oh chadema wanataka kumwaga damu, oh wanahatarisha amani ya nchi, na hao makasuku wanapotokea kwenye media ili ujue ni waoga hawatoi nafasi ya watu kuwauliza maswali kwani wanajua wazi hawana majibu!!. Sasa ombi langu kwa wanachadema na wapenda maendeleo wote tusitishike na vitisho vyao sisi mwendo mdundo mpaka tuikomboe nchi yetu kutoka kwenye makucha ya mafisadi. wamebuni vimbinu uchwara vya kutuzuilia maandamano kwa kujifanya eti kulikuwa na maandamano ya wanaomuunga mkono JK ila polisi wameona haifai, hiyo ni janja yao ili tutakapo anza, ngwe nyingine waje na visingizio vya kiintelejensia. TUSIKUBALI,TUSIKUBALI, WALA TUSILUHUSU MAFISADI KUTUZUIA KWA NAMNA YOYOTE!!!
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngojeni nguvu za dola ziwangukie tena kwa kishindo kikubwa sana. Muulizeni Godbless Lema analitambua hilo.N
   
 3. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu unakazi, baada ya akina Zemarcopolo na Bado nipopo kukimbia, saiv naona unawakilisha vilivyo.
  Hivi wewe ni nani mbona hujielewi kiasi hicho, yaani unachofanya Jf ni kupindua ukweli tu na kwa taarifa yako unadhalilisha wenzako afadhali ubadilishe id, maana unakera, hakuna lolote unalojua. Hivi hali ya taifa unaionaje? Mbona sikuelewi, kila post yako ni ushudu tu, hakuna hata chembe ya maana. Wanajf tumieni muda mfupi mtembelee post za HM Hafif muone, huyu jamaa ametumwa lakini hana uwezo wa kutoa hoja wametuma boya.
   
 4. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo nguvu ya dola anayoisema haina uwezo wa kushindana na nguvu ya umma!! labda ana maana nyingine
   
Loading...