VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
CCM ni chama kikubwa na kikongwe hapa nchini. Ni chama tawala. Ni chama dola. Kimeshinda chaguzi zote kuu za vyama vingi kuanzia ule wa 1995 hadi wa 2015. Pamoja na uwepo wa wagombea machachari na 'hatari' wa Urais (mfano wa Mrema, Slaa na Lowassa), CCM imekuwa ikiibuka kidedea na bendera kuendelea kupepea.
Hata kwenye Ubunge na Udiwani, CCM hulidhibiti Bunge na Halmashauri nyingi mno kwa kushinda kwa wingi wa Wabunge na Madiwani. CCM ni nambari wani! Huu wasiwasi uliopo sasa unatokea wapi? Huu wasiwasi hadi kuanza kampeni za Urais mapema unatokana na nini hasa? Hatumuamini mgombea wetu mtarajiwa? Hajafanya lolote? Hasemi na kufanya yaliyo mema?
Serikali hii imeimarisha miundombinu (barabara, reli, madaraja nk); imefufua Shirika letu la Ndege; inajenga Bwala la Umeme la Nyerere; imedhibiti nidhamu ya watumishi wa umma na kupunguza pakubwa rushwa na ufisadi; imewaweka akiba watumishi wa umma kuhusu mishahara na stahiki zao nyingine; imekifanya chama chetu cha CCM kubaki pekee kilicho 'active' na kadhalika.
Yote hayo hayatoshi na kutupa amani moyoni ya kuibuka kidedea mwaka huu? Kama chama, kama ilivyo kawaida yetu, tunazo lulu zetu za ushindi. Tunayo ile ya 'kupita bila kupingwa', Tume Huru ya Uchaguzi, Polisi, Wazee wa Suti na 'kekundu'. Wasiwasi wetu unatokea wapi kama chama kila kitu cha kuhakikisha ushindi unapatikana? Tujiamini
Inashangaza CCM kusafiria nyota ya Msanii kama Diamond ili kumpigia debe Dr. Magufuli na 'kumhakikishia' ushindi mwaka huu. Ni aibu na inatia ghadhabu. Tunamuogopa nani ikiwa tuna mema na vitendea kazi vya kuibuka washindi kuliko wahindi. CCM tunapaswa kutembea vifua-mbele hadi kwenye kilele. Kuanza kampeni mapema ni uoga na aibu kwa chama!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam