EDIBIL MJENJWA
Member
- Oct 30, 2016
- 60
- 36
WANACCM wenye akili wamchoka Pombe? Waanza kufunguka hadharani
....Shikamoo Kilimba
WANACCM TUNA NAFASI YA KUMSHAURI MKUU , TUFANYE HIVYO KWA FAIDA YA CHAMA NA TAIFA LETU.
Ndugu wanaCCM wenzangu kwa unyenyekevu na upendo mkubwa nawasalimu sana hongereni kwa majukumu ya kulijenga taifa na chama chetu kikongwe Afrika na duniani kote .
Ndugu wanaCCM kwa nia njema na mapenzi makubwa niliyonayo kwa chama changu ukizingatia chama chetu tunaheshimiana, tunavumiliana, tunasahihishana na kuelekezana kiuungwana naomba niseme nanyi kizalendo kwa faida ya chama chetu , wananch wetu na taifa letu
Sisi wanaCCM viongozi mpaka wanachama tuna nafasi ya kusema na mkuu wetu kuliko Watani zetu na huenda maneno yetu ni muhimu sana maana tuna sifa moja kubwa inayotuweka pamoja "SOTE NI WANACCM " kwa faida ya chama chetu tumkumbushe mkuu wetu mambo haya muhimu sana vinginevyo uchaguzi ujao wapiga kura hawawezi kutuelewa , nawasihisi wanaCCM wenzangu tutumie undugu na ukaribu wetu kumkumbusha mkuu wetu haya ili tubaki salama kama chama , tusikubali kujizika kama KANU na vyama vingine vikongwe vilivyokufa kifo kitokanacho na mazoea
Mosi, Tumshauri aache kupuuza njaa kali inayowatafuna wapiga kura wenye mapenzi makubwa kwake na chama chetu, tuseme nae watanzania wanampenda na wanatarajia faraja kwake na matumaini yao yapo kwake mifugo inakufa, mazao yananyauka, wapo hoi huenda wasaidizi wake wanapotosha lakini ukweli hali ni mbaya sisi wanaCCM tuna nafasi kubwa kusema nae tusiogope kumshauri mkuu wetu ni muungwana wala hana tatizo na mtu tena ni mcha Mungu nina hakika maneno yetu yana nguvu na ushawishi mkubwa kwake tuseme nae ili chama chetu kibaki salama kupuuza njaa ya wapiga kura itajenga chuki na matokeo ya chuki ni visasi na visasi vya wapiga kura vipo kwenye sanduku la kura. WanaCCM kwa pamoja tumshauri mkuu wetu kuepuka kura za visasi dhidi ya chama chetu.
Pili , tumshauri mkuu wetu apunguze ukali kwa wasaidizi wake pamoja na faida kubwa inayotokana na ukali wake dhidi ya wasaidizi wake wazembe bado ukali wake umesababisha vituko kwa wasaidizi wake mpaka wengine wanasema uongo kulinda vibarua vyao , tazama wakuu wa mikoa na wilaya wanalazimisha watanzania wenye njaa waimbe na kucheza ngoma za shibe, tazama wataalam wa afya wanasema dawa zipo za kumwaga wakati sehemu nyingine hata panado hakuna, tazama wasaidizi wake wanavyofanya maamuzi ya kushangaza dunia mpaka wengine wanavunja sheria kulinda vibarua vyao. Kwa pamoja tumshauri mkuu wetu hawa wasaidizi wake wengi siyo waomba kura kwenye uchaguzi hawana kazi kubwa kama sisi wanaCCM tulio karibu na wapiga kura .
Tatu, wanaCCM tumshauri mkuu wetu aelekeze jicho lake la huruma kwa watumishi wa umma wapo wenye haki ya kuhama hawajui hatima yao, wapo waliostaafu hawajui lini watapewa matunda yao ya utumishi, wapo wenye kudai malimbikizo hawajui hatima yao , wapo wenye haki ya kupanda madaraja hawajui kesho yao , watumishi wa umma hawajui dhamira ya mkuu wetu dhidi yao na hakuna mtu wa kusema na mkuu zaidi ya wanaCCM sisi ndiyo tunapaswa kusema nae kwa unyenyekevu ikiwezekana hata ilani yetu itumike kumkumbusha hata kurejea maneno yake kwenye kampeni dhidi ya watumishi tufanye hivyo kwa faida ya mkuu wetu, chama chetu na taifa letu . Watumishi wakionesha hasira zao hatuwezi kubaki salama tusikubali kabisa waoneshe hasira tumshauri awatimizie mahitaji yao kuliko kulazimisha wafanye kazi kwa hofu
Nne, tumshauri mkuu wetu aruhusu siasa ya vyama vingi watani zetu wafanye siasa zao ili watanzania wazoee vijembe na kejeli zao mwisho wawapuuze kuwazuia ni hatari sana maana watanzania wakuwa na kiu ya kuwasikiliza tumshauri mkuu wetu kuwabana watani zetu anawafanya wawe spesho sana mbele ya jamii kitu kilicho hatari kwa maisha ya chama chetu. Kwa pamoja tumshauri awaruhusu wafanye mikutano halali, wafanye vikao halali ili jamii isipate kiu ya kusikiliza maneno yao , wala mkuu wetu hana madhambi asiogope awaruhusu waseme tu watanzania watamsheshimu kwa kazi yake ya kutekeleza ilani ya chama chetu.
Tano , tumshauri mkuu wetu wape nafasi wataalam watafute suluhisho la kuyumba kwa uchumi wetu , aruhusu mijadala ya wazi namna ya kurejesha mzunguko wa pesa , aruhusu wataalam wajadili waje na majawabu kwanini uchumi unakua kwenye makaratasi huku watanzania wakiendelea kuwa hoi kiuchumi. WanaCCM tumshauri mkuu akubali changamoto ya kuyumba kwa uchumi tufanye hivyo kwa faida ya chama chetu watani zetu wanatumia maneno makali mno huenda ndiyo maana anawapuuza sisi wanaCCM wenzake tuungane pamoja tumshauri kwa sauti za upole na unyenyekevu atatusikiliza mkuu wetu ni muungwana.
Sita , tumshauri mkuu apunguze maneno yenye kuchukiza wapiga kura ni kweli taifa letu lilipoteza uadilifu kwa kiasi kikubwa, ni kweli kuna mambo yanakera sana ndani ya nchi yetu , ni kweli tunahitaji kiongozi asiyeogopa kusema kizalendo kwa faida ya watanzania wote lakini hasira, uchungu na maumivu ya mkuu wetu asipelekee atamke maneno mazito ya kushtua na kukatisha tamaa wananch wanyonge wanaomlaza bila amani kwa kufikria maisha yao duni hasa akiwaza namna ya kuwavusha tazama kagera wanaogopa hata kusikia sauti yake , tazama watumishi wanavyoziba masikio akianza kuzungumza, tazama wakulima na wafugaji wanavyoiogopa sauti yake ilivyokuwa sauti yenye matumaini kipindi cha uchaguzi, tazama watanzania wanavyozima televisheni na radio akianza kuzungumza wakati awali walikuwa wanajazana kumsikiliza. WanaCCM kwa umoja wetu , upendo wetu na uungwana wetu tumshauri mkuu atumie maneno yenye kutia moyo , maneno yenye faraja, maneno yenye huruma, maneno yenye ukarimu na kuguswa kama ilivyo kwake historia yake inaonesha alivyo mkarimu kwa wananch tumshauri aishi katika historia yake apunguze hasira wakati mwingine hasira zake zinawatimulia vumbi wasio na hatia kabisa , pamoja na maumivu aliyonayo kutokana na mapenzi kwa taifa na watu wake achague maneno ya kuzungumza kutokana na mazingira.
Saba , wanaCCM tumshauri mkuu atumie Mamlaka yake kupanga timu yake upya kwa faida ya chama na taifa letu asiendelee kusikiliza maneno matamu yasiyo na vitendo, asidanganywe na picha , video na taarifa za habari za kupamba timu yake mawaziri wengi wameshindwa kazi wapo bize na maigizo, wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, na viongozi wengine wapo bize kutafuta picha za kuweka kwenye magazeti ili kuonesha wanafanya kazi wakati huku hamna lolote wanalofanya, tazama WAZIRI WA VIWANDA anavyopiga kelele pasipo vitendo, tazama timu yako kwenye AFYA ilivyochemka, tazama WAZIRI WA KILIMO alivyo hoi kiutendaji, tazama migogoro ya ardhi inavyonoga huko KIGOMA wananch wanapigwa na askari wa Wanyama pori , wanapokonywa mali zao , tazama kwenye MAHAKAMA mambo siyo shwari achana na hizo taarifa za habari za kufurahisha na kupendeza machoni. wanaCCM tumshauri mkuu tutumie lugha zetu zenye kuvutia kumsihi atazame upya timu yake wengi wapo hoi wamekosa ubunifu kabisa ndiyo maana wapo bize kuweka matukio kwenye mitandao angalau waonekane wanafanya kazi wakati ukweli hakuna lolote wanalofanya, kila habari ni kutumbua, kusimamisha kazi hakuna habari za kumaliza tatizo la maji , hakuna taarifa za kumaliza changamoto ya njaa, hakuna habari za kumaliza matatizo ya watumishi zaidi ni habari za mbabe kumpiga mnyonge wake . Tumsihi mkuu apange upya timu yake siyo dhambi wala udhaifu kuanza upya.
Nane , wanaCCM tumshauri mkuu wetu aanze kutatua changamoto zenye kugusa maisha ya watanzania moja kwa moja , tumshauri na kumsihi hizo ndege mbili zinatosha kabisa ni mwanzo mzuri sasa atazame kuhusu shida ya maji Dodoma makao makuu hakuna maji na kisima cha kisasa ni million 20 tu aache kwanza kuongeza ndege alete maji , tumsihi wanyonge wengi wanatumia mabasi na train siyo ndege hivyo aboreshe usafiri wa reli na barabara ndiyo atawagusa wanyonge hakuna mnyonge mwenye kumudu gharama za ndege , tumshauri afikrie sasa kuhusu million 50 kila kijiji kabla ya mwaka wa bajeti kuisha, tumkumbushe atumie pesa kwa faida ya wanyonge wenye uhitaji zaidi .
Tisa , tumshauri mkuu wetu afuate mkataba wetu (ilani yetu ya uchaguzi) ni kweli kabisa ni muhimu kunyoosha nchi na kurejesha nidhamu , uadilifu na uzalendo lakini haitoshi kupuuza mahitaji mengine ya ilani yetu , tumshauri atazame suala la ajira lipo kwenye ilani, atazame suala la katiba lipo kwenye ilani, atazame suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa umma lipo kwenye ilani , atazame suala la mikopo ya Wanachuo lipo kwenye ilani, atazame suala la kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji lipo kwenye ilani na mengine mengi , pamoja na kutumbua majipu, kuhakiki watumishi hewa, pamoja na kunyoosha nchi lazima mkataba wake na chama chetu ufuatwe vinginevyo uchaguzi ujao wapiga kura watatuadhibu bila huruma. Tumshauri mkuu wetu wala hana tatizo tufanye hivyo kwa faida ya chama chetu.
Kumi , wanaCCM tumshauri mkuu wetu awaondoe wasiwasi wabunge wa CCM na viongozi wengine wa CCM waache tabia ya kufanya mambo kwa kumfurahisha badala yake wafanye kazi kuboresha na kuimarisha utendaji wake ulio mwema tazama suala la ukata wa sukari waliongea kumfurahisha, tazama uhaba wa dawa wanamfurahisha eti dawa zipo , tazama suala la njaa wanalazimisha wananch waimbe na kucheza ngoma za shibe ili wamfurahishe, tazama suala la watumishi kudharilishwa na wasaidizi wake wabunge na viongozi kadhaa wa CCM wanasifu eti ni kurejesha nidhamu , tumshauri mkuu wetu awaambie wao ndiyo kioo chake lazima wamuoneshe ubora wake , makosa yake na udhaifu wake tena wamsahihishe awe bora zaidi unafiki wakupongeza na kupiga vigelele gharama yake ni kubwa mbele ya safari tena gharama yake inaweza kuangamiza chama chetu tumsihi awaondoe wasiwasi wapunguze kumuogopa kiasi cha kupongeza mpaka mabaya maana hata yeye ni mwanadamu ndiyo maana anafanya ibada kumuomba Mungu. WanaCCM tumshauri atambue hakuna Tanzania ya viwanda wala ya uchumi wa kati ndani ya wabunge na viongozi wanafiki wenye kuogopa kukosoa, kurekebisha na kuonesha njia zilizo bora zaidi.
Mwisho, Mkuu wetu ni mwenye dhamira ya kutuvusha maneno yake, matendo yake vinaonesha kabisa dhamira yake ni njema dhidi yetu tatizo lipo ndani ya timu yake, sisi wanaCCM washangiliaji na wapiga vigelele tusiotaka kusema ukweli pale inapobidi, wanaCCM wengi wanadhani kuwa mtiifu ni kusema ndiyo na kucheza mpaka midundo ya furaha kwenye msiba , sisi wanaCCM lazima tujue fujo za CUF hazina tija kwenye kutekeleza ilani yetu na ahadi zetu kwa wananch, vurugu za LEMA wala hazina hata faida moja kwenye utendaji wetu kama chama chenye dola hivyo ni udhaifu na uzembe wa kufikri kushinda kwenye mitandao, vyombo vya habari na vijiweni kushangilia kukamatwa kwa wapinzani na ugomvi wao badala yake tuwe bize kumshauri mkuu wetu afanye kazi bora kwa faida ya chama na taifa .
Ndugu wanaCCM wenzangu lazima tujue dunia imebadilika , Tanzania kuna wasomi wengi sasa wenye kudadisi hakuna tena kura za bure wapiga kura wataomba mrejesho hivyo tuache mazoea kudhani wapiga kura ni wale wale wa miaka yote . Mazoea yamepoteza vyama vingi Afrika na duniani kote nawasihi tuwe kitu kimoja tumshauri mkuu wetu kwa lugha tamu za unyenyekevu nina hakika atatusikiliza wala hatatupuuza pengine anapuuza Watani zetu (wapinzani) kwa kudhani wanampotosha kwa faida yao , sisi ni ndugu yetu kiitikadi hivyo tumshauri tusiogope wala hana shida ni muungwana.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Ndimi LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331