WanaCCM Chemba wafurahia maadhimisho ya miaka 42 ya CCM kuwafikia

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ndg. Lailah Ngozi ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Chema Kata ya Nyamshindo, Tawi la Mengu, akiwa huko amekutana na viongozi wa Matawi, Kata na Wilaya.

Wana CCM hao na viongozi wa Wilaya ya Chemba wamempongeza sana ndg. lailah Ngozi na CCM kwa kuwafikia wananchi wa Kata ya Nyamshindo na Mengu kwani tangu Uhuru hakuna kiongozi yoyote wa Kitaifa ambae amewahi kufika. Hivyo wameishukuru sana Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli kwa kukifanya Chama Cha Mapinduzi kuwa ni Chama kinachosikiliza na kutatua kero za wananchi. Na hii inadhihirika kwa vitendo.

Akiwa huko amepokea wana Chama wapya wapatao 100 sambamba na hilo uongozi wa Wilaya ukamweleza katika maadhimisho haya ya sherehe za miaka 42, mpaka kufikia tarehe 28 wanatarajia kupokea si chini ya wana Chama wapya elfu 20 hii inatokana na wananchi kutoridhishwa na utendaji kazi wa wapinzani kwani wako kinadharia zaidi kuliko matendo kitu ambacho CCM iko kivitendo zaidi.

Wananchi wamempongeza ndg. Lailah Ngozi na CCM kwa kuamua kuadhimisha sherehe hizo Wilayani kwao kwani huko awali haikuwahi kufanyika kwa kuwafikia wana Chama wa ngazi ya chini, hivyo sasa wanaiona dhana ya Chama Cha Mapinduzi kuwa karibu na wananchi wake.

"Tunakupongeza sana Ndg. Lailah na viongozi wote wa Kamati Kuu ya CCM mkiongozwa na Ndg. Magufuli kwa heshima mliyotupatia na kuamua kila Wilaya na Mkoa uadhimishe sherehe hizi na wewe kuja kusherehekea nasi. Tunakupongeza sana na kukukaribisha sana Chemba"Ni maneno ya taarifa ya viongozi wa CCM wa Chemba.

Pamoja na mambo mengine lakini pia Wameipongeza Serikali ya CCM kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo. Kwani maendeleo yaliyofikiwa wilayani Chemba ni juhudi kubwa zilizofanywa baina ya Chama na Serikali.

"Ni serikali ya CCM chini ya Dr.Magufuli ambayo imetufikishia umeme wa uhakika tena kwa gharama nafuu,Tumepokea Bil 11 kwa ajili ya uchimbwaji wa visima vya maji, Vituo vya Afya vitatu vimepatiwa mil 400 kwa ajili ya vifaa na madawa yanapatikana kwa asilimia 98 hatuna cha kumlipa Rais Magufuli na Serikali yake zaidi ya shukrani na kumhakikishia ushindi wa kishindo ifikapo 2020" Taarifa ya Serikali ya Wilaya ya Chemba kwa Ndg. Ngozi.

Katika taarifa hiyo waliendelea kuishukuru Serikali ya CCM kwa kuwapatia fedha kwajili ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya na kuwajengea barabara ya kiwango cha lami ikitoka Tanga na kupita hadi kwenye vijiji vyao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
IMG-20190210-WA0034.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom