MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Huwa ninawashangaa sana baadhi ya wanaCCM wanaopiga kelele kumtaka Freeman Mbowe aachie cheo cha uenyekiti wa CHADEMA Taifa. Ninadhani hawajui nafasi ya Mbowe katika Maisha ya CCM tokea awe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Baadhi ya wanaCCM hawajui kuwa CCM imeendelea kushika dola kutokana na mchango mkubwa wa Mbowe kama Mwenyekiti wa CHADEMA.
Siwezi kujua kwa sasa CCM ingekuwa na hali gani kama Mbowe asingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa lakini ninachojua kuwa mchango wake ndani ya CHADEMA umeiwezesha CCM kuendelea kushika dola.
Ieleweke kuwa Mbowe sio mwanasiasa bali ni mjasiliamali wa kisiasa. Kwa Mbowe, money talks than politics. Ukiweka dau la pesa au siasa mezani na ukamtaka kipi achukue, Mbowe atachukua pesa na kukuachia siasa. Mwaka 2006 wakati akiwa London akiongea na Watanzania kwenye Hotel ya Holiday Inn alinukuliwa akisema, “Politics to me is not a profession. I am a businessman and will remain one.
Historia inachagiza hoja zangu kuhusu msaada wa Mbowe kwa CCM kama ambavyo Mbunge Zitto Kabwe alivyowahi kubainisha katika andiko lake ambalo linapatikana hapa;
LINK>>>Zitto aanika siri nyeti za Mbowe, Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
Zitto alibainisha hayo kwa kuandika, "Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?’’
Zitto aliendelea kuandika, ‘’ Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas’’.
Ukisoma andiko la Zitto utagundua kuwa kwa kiasi kikubwa Mbowe amekuwa akiisaidia CCM kuendelea kushika dola.
Hata pale ambapo CUF ilionekana kutishia uhai wa CCM mwaka 2000-2005, Mbowe alijitokeza na kuisaidia CCM. Hata mwaka 2015 ambapo alionekana CCM iko kwenye hali ngumu sana ya kisiasa, Mbowe aliibuka tena baada ya kuchukua ''dau'' ili kuisaidia CCM kuendelea kushika dola kwa kutoa tiketi ya kugombea Urais kwa Edward Lowassa ambaye alijua vizuri kuwa hatashinda Uchaguzi Mkuu kutokana na Mbowe na kundi lake kumdhoofisha sana kwa kumvisha taji ya ufisadi papa kwa miaka zaidi ya miaka 8 huku wengine wakisema hafai hata kuchukua fomu ya kugombea Urais achilia mbali kupitishwa kuwa mgombea Urais. Msaada wa Mbowe ukaiwezesha CCM kuendelea tena kushika dola lakini kikubwa zaidi hata pale ambapo baadhi ya wapenzi na wanachama wa CHADEMA walipoanza kutoa shikinizo la kutaka kufanya fujo baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, Mbowe alijitokeza na kuwapiga stop. Mission accomplished!
WanaCCM watambue kuwa hata mwaka 2020 atawasaidia tena kuendelea kushika dola!
Kumshinikiza Mbowe ili aachie Uenyekiti wa CHADEMA ni kukaribisha tatizo/matatizo ambayo hayajulikani utatuzi wake.
CCM kumbukeni Waingereza wana msemo usemao, ‘if it ain't broke, don't fix it and be careful what you wish for, lest it come true''!
WanaCCM acheni kujitakia matatizo ambayo ninaamini hamjui utatuzi wake!