Wanaanga 4 kuelekea katika kituo cha anga za mbali Oktoba 5

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Mara baada ya miezi sita kupita ni zamu nyengine kwa wanaanga wengine kwenda katika kituo cha anga za mbali ili kwenda kuendelea na majukumu ya kuhudumia kituo hicho mara baada ya wale wengine kumaliza muda wao wa miezi 6 katika kituo hicho

Ni kawaida kwa mataifa 2 ya marekani na russia ambayo kwa kiasi kikubwa ndio wamiliki wakubwa wa kituo hicho cha anga kwakuwa wanamiliki eneo kubwa la segment katika kituo hicho , ambapo kila baada ya miezi sita hufanya mabadiliko ya wanaanga wao ili waingie wengine

Josh Cassada na Nicole Mann (Usa) huku Koichi wakata (Japani) na Anna kikina (Russi) wote kwa pamoja wataweza kuruka katika rocket ya Falcon 9 ambayo safari nzima zipo katika usimamizi wa shirika la uchunguzi wa anga NASA

Tunaweza kuona kwa mara nyengine tena Marekani na urusi wanaendeleza ule ushirikiano wa jadi katika masuala ya anga za mbali ambayo kwa makubaliano yaliyowekwa hapo zamani kwamba masuala ya anga yatabaki kuwa katika mashirikiano kwakuwa dunia ni yetu sote

Kumbuka wanaanga hawa 4 watakwenda kuishi katika kituo hicho kwa kiasi cha siku zitatazo 180 ambazo ni sawa na makadirio ya miezi sita huku wakihudumu katika marekebisho ya kituo hicho na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi anga za mbali

Safari itafanyika siku ya kesho October 5 katika majira ya saa tisa mchana kwa masaa ya afrika ya mashariki ambapo tutaweza kushuhudia suala hilo kwenye linki nitakayoiweka hapo chini kesho mapema kabisa

Pichani ni rocket ya Falcon 9 ikiwa katika eneo maalumu la Launch pad complex 39A ambalo ni maalumu kwa kurusha mission za zote zinazohusu binadamu ndani ya rocket

#🇬 🇪 🇷 🇦 🇱 🇩  #Tanzaniascienceyetu #Elimuyaangazambali
FB_IMG_1664911038282.jpg
 
Back
Top Bottom