Wanaamua juu ya maisha yetu, na wanaandaa watoto wao kuamua juu ya watoto wetu.

Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
386
517
Siasa ya TANU ni kujenga nchi ya Ujamaa, misingi ya Ujamaa imetajwa katika katiba ya TANU,
nayo ni hii;
Kwa kuwa TANU inaamini:
(a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
(b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
(c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika
serikali tangu ya mitaa, ya mikoa hadi serikali kuu;
(d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo yake, ya kwenda anakotaka, wa
kuamini dini anayotaka na wa kukutana na watu mradi havunji sheria;
(e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake na
mali yake aliyo nayo kwa mujibu wa sheria.

Nimeanza mada yangu kwa kuweka sehemu ya Imani ya tanu...
Nchi hutawaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo kwa kuwa katiba iliyopo haijaeleweka kwa wanaoongoza taasisi muhimu hasa majeshi na usalama wa taifa, watawala wametumia fursa hiyo ya "UJINGA WAKUJITAKIA" wa viongozi wa majeshi na idara nyeti TISS unaotokana na kutokuisoma nakuielewa katiba ili kulinda maslahi ya raia dhidi ya watawala.Sasa ni wazi watawala wamegeuza hivi vyombo vya wananchi kuwa fimbo yao yakusimika utawala wao...Sasa wanaamua watakavyo juu ya hatima yetu watakavyo, na wanaandaa watoto wao kuja kuamua juu ya hatima ya watoto wetu.

Sasa ni wazi ya kuwa:
(a) Kwamba binadamu wote SI sawa;
(b) Kwamba kila mtu hastahili heshima;
(c) Kwamba kila raia SI sehemu ya Taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika
serikali tangu ya mitaa, ya mikoa hadi serikali kuu;
(d) Kwamba kila raia HANA haki ya uhuru wa kutoa mawazo yake, ya kwenda anakotaka, wa
kuamini dini anayotaka na wa kukutana na watu mradi havunji sheria;
(e) Kwamba kila mtu HANA haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake na
mali yake aliyo nayo kwa mujibu wa sheria.

Hivyo basi ni muhimu kila raia wa nafasi yake kushinikiza watawala kuheshimu katiba iliyopo na wasaidie kupatika katiba iliyo BORA...Ili kila raia awe sehemu ya jamhuri iliyo huru
 
Back
Top Bottom