Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,284
- 10,665
Ni lini GSM au kiongozi wa Yanga alisema kuwa angewasajili hao wachezaji? Mbinu iliyotumika kumng'oa Senzo Simba ndio mbinu hiyohiyo inatumika kwenye usajiliNikiwa kama Mshabiki Mwandamizi kabisa wa Yanga SC 'nimekerwa' sana na aina ya 'Unyanyasaji' wa 'Kimafia' kabisa tunaofanyiwa na Timu bora si tu Tanzania bali Afrika ya Mashariki na Kati, Duniani hadi hadi Mbinguni ya Simba Sports Club halafu Sisi Wanayanga tunabaki 'Kunyamaza' tu pekee.
Wiki ya Jana Yanga SC tulikuwa tunamleta Bonge la Beki ambaye ni zaidi ya Bakari Nondo Mwamnyeto aitwae Ibrahim Ami aje 'Kusinya / Kusaini' Kwetu Yanga SC cha 'Kushangaza' Klabu tusiyoipenda ila inayopendwa mno na Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club ikamsajili na sasa ni Mali yao kabisa.
Mwanzoni mwa Wiki hii wana Yanga SC tulikuwa tunajua kabisa kuwa Kiungo 'Mahiri' kutoka Ghana ambaye pia ni Wakili Msomi na wa Kujitegemea Bernard Morrison ni Mali ya Yanga SC kumbe ameshakuwa ni Mali ya Simba Sports Club kitu ambacho ni 'Hatari' sana Kwetu kwani mpaka hivi sasa ndani ya Yanga SC sijaona Beki ya 'Kumkaba' huyu Morrison ukiachia akina Chama na Miquissone.
Kubwa kuliko na hii ndiyo 'imeniuma' sana hadi sasa nataka wanayanga Wenzangu wowote popote pale mlipo 'tujitokeze' na 'tuwatimue' hawa 'Wanafiki' akina GSM pamoja na Mwenyekiti Wetu Mshindo Msola kwani wameshaonyesha kuwa ni 'Waongo' na 'Matapeli' tu pia hasa linapokuja Suala zima la Usajii.
Ni muda mfupi tu umepita Yanga SC tulikuwa tunategemea 'Kumpokea' Kiungo Mshambuliaji 'Hatari' kabisa ambaye uwezo wake Uwanjani ni 'maradufu' ya Clatous Chama aitwae Larry Bwalya. Cha 'Kushangaza' GSM na Mwenyekiti Msola pamoja na Magazeti ya Michezo 'yalituaminisha' Wiki nzima kuwa ni Mali ya Yanga SC na hatimaye 'ameshasinya / ameshasaini' Simba Sports Club.
Kwa hasira nilizonazo GENTAMYCINE nawapa GSM na Mwenyekiti Msola Saa 72 tu zijazo watuachie Yanga SC yetu na itakuwa chini yetu Mashabiki.