Wana Yanga SC Wenzangu hivi ni mpaka lini Simba SC itaendelea 'Kutunyayasa' namna hii katika Usajili? Tuwafukuzeni upesi GSM na Msola watuachie Timu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,249
110,830
Nikiwa kama Mshabiki Mwandamizi kabisa wa Yanga SC 'nimekerwa' sana na aina ya 'Unyanyasaji' wa 'Kimafia' kabisa tunaofanyiwa na Timu bora si tu Tanzania bali Afrika ya Mashariki na Kati, Duniani hadi hadi Mbinguni ya Simba Sports Club halafu Sisi Wanayanga tunabaki 'Kunyamaza' tu pekee.

Wiki ya Jana Yanga SC tulikuwa tunamleta Bonge la Beki ambaye ni zaidi ya Bakari Nondo Mwamnyeto aitwae Ibrahim Ami aje 'Kusinya / Kusaini' Kwetu Yanga SC cha 'Kushangaza' Klabu tusiyoipenda ila inayopendwa mno na Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club ikamsajili na sasa ni Mali yao kabisa.

Mwanzoni mwa Wiki hii wana Yanga SC tulikuwa tunajua kabisa kuwa Kiungo 'Mahiri' kutoka Ghana ambaye pia ni Wakili Msomi na wa Kujitegemea Bernard Morrison ni Mali ya Yanga SC kumbe ameshakuwa ni Mali ya Simba Sports Club kitu ambacho ni 'Hatari' sana Kwetu kwani mpaka hivi sasa ndani ya Yanga SC sijaona Beki ya 'Kumkaba' huyu Morrison ukiachia akina Chama na Miquissone.

Kubwa kuliko na hii ndiyo 'imeniuma' sana hadi sasa nataka wanayanga Wenzangu wowote popote pale mlipo 'tujitokeze' na 'tuwatimue' hawa 'Wanafiki' akina GSM pamoja na Mwenyekiti Wetu Mshindo Msola kwani wameshaonyesha kuwa ni 'Waongo' na 'Matapeli' tu pia hasa linapokuja Suala zima la Usajii.

Ni muda mfupi tu umepita Yanga SC tulikuwa tunategemea 'Kumpokea' Kiungo Mshambuliaji 'Hatari' kabisa ambaye uwezo wake Uwanjani ni 'maradufu' ya Clatous Chama aitwae Larry Bwalya. Cha 'Kushangaza' GSM na Mwenyekiti Msola pamoja na Magazeti ya Michezo 'yalituaminisha' Wiki nzima kuwa ni Mali ya Yanga SC na hatimaye 'ameshasinya / ameshasaini' Simba Sports Club.

Kwa hasira nilizonazo GENTAMYCINE nawapa GSM na Mwenyekiti Msola Saa 72 tu zijazo watuachie Yanga SC yetu na itakuwa chini yetu Mashabiki.
 
kila nikiona Post zako huwa najiuliza wewe jamaa utakua una tatizo kama sio matatizo, ila navyoona inawezekana kabisa una stress ila sijui ni za nini, nakushauri tu jaribu kutafuta watu wasaikolojia wanaweza kukusaidia, kwani licha ya kua unaleta thread zisizo na mahana ajabu hua unajikubali nakujiona kua wewe ni genius kumbe inawezekana dishi limeyumba.

Lakini isiwe inshu sana, najaribu tu kukupa ushauri
 
Nikiwa kama Mshabiki Mwandamizi kabisa wa Yanga SC 'nimekera' sana na aina ya 'Unyanyasaji' wa 'Kimafia' kabisa tunaofanyiwa na Timu bora si tu Tanzania bali Afrika ya Mashariki na Kati, Duniani hadi hadi Mbinguni ya Simba Sports Club halafu Sisi Wanayanga tunabaki 'Kunyamaza' tu pekee.

Wiki ya Jana Yanga SC tulikuwa tunamleta Bonge la Beki ambaye ni zaidi ya Bakari Nondo Mwamnyeto aitwae Ibrahim Ami aje 'Kusinya / Kusaini' Kwetu Yanga SC cha 'Kushangaza' Klabu tusiyoipenda ila inayopendwa mno na Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club ikamsajili na sasa ni Mali yao kabisa.

Mwanzoni mwa Wiki hii wana Yanga SC tulikuwa tunajua kabisa kuwa Kiungo 'Mahiri' kutoka Ghana ambaye pia ni Wakili Msomi na wa Kujitegemea Bernard Morrison ni Mali ya Yanga SC kumbe ameshakuwa ni Mali ya Simba Sports Club kitu ambacho ni 'Hatari' sana Kwetu kwani mpaka hivi sasa ndani ya Yanga SC sijaona Beki ya 'Kumkaba' huyu Morrison ukiachia akina Chama na Miquissone.

Kubwa kuliko na hii ndiyo 'imeniuma' sana hadi sasa nataka wanayanga Wenzangu wowote popote pale mlipo 'tujitokeze' na 'tuwatimue' hawa 'Wanafiki' akina GSM pamoja na Mwenyekiti Wetu Mshindo Msola kwani wameshaonyesha kuwa ni 'Waongo' na 'Matapeli' tu pia hasa linapokuja Suala zima la Usajii.

Ni muda mfupi tu umepita Yanga SC tulikuwa tunategemea 'Kumpokea' Kiungo Mshambuliaji 'Hatari' kabisa ambaye uwezo wake Uwanjani ni 'maradufu' ya Clatous Chama aitwae Larry Bwalya. Cha 'Kushangaza' GSM na Mwenyekiti Msola pamoja na Magazeti ya Michezo 'yalituaminisha' Wiki nzima kuwa ni Mali ya Yanga SC na hatimaye 'ameshasinya / ameshasaini' Simba Sports Club.

Kwa hasira nilizonazo GENTAMYCINE nawapa GSM na Mwenyekiti Msola Saa 72 tu zijazo watuachie Yanga SC yetu na itakuwa chini yetu Mashabiki.
Nyinyi Yanga mtaendelea kunyanyasika mpaka mtakapogundua Fredrick Mwakalebela ni mtu wetu. Pia Senzo bado yuko kwenye Payrol ya MO kimtindo.

Siri zenu zote tunazo, yaan hata kabla hamjamaliza vikao vyenu vya Siri huku tushapata mkanda mzima kilichojadiliwa.
 
Yaelekea GSM hawana hela hawa ni wababaishaji na Mwenyekiti mara laliga mara huyu mali yetu,Makambo kesho anatambulishwa na Simba.
Hawa GSM wanatumia nembo ya yanga kujipatia kipato
Yanga ni enzi Manji mkamnyima timu mkafuata ya maehemu Akilimali.Msipoangalia msimu ujao wa ligi Simba inawatandika magoli 11 bila.
 
kila nikiona Post zako huwa najiuliza wewe jamaa utakua una tatizo kama sio matatizo, ila navyoona inawezekana kabisa una stress ila sijui ni za nini, nakushauri tu jaribu kutafuta watu wasaikolojia wanaweza kukusaidia, kwani licha ya kua unaleta thread zisizo na mahana ajabu hua unajikubali nakujiona kua wewe ni genius kumbe inawezekana dishi limeyumba.

Lakini isiwe inshu sana, najaribu tu kukupa ushauri

Baada ya kuwa nae kwa muda mrefu 'Kimahusiano' Yule aliyekufanya leo hii upo nasi hapa duniani na 'Kuachana' nae ndiyo kaniharibu Kisaikolojia.
 
Yaelekea GSM hawana hela hawa ni wababaishaji na Mwenyekiti mara laliga mara huyu mali yetu,Makambo kesho anatambulishwa na Simba.
Hawa GSM wanatumia nembo ya yanga kujipatia kipato
Yanga ni enzi Manji mkamnyima timu mkafuata ya maehemu Akilimali.Msipoangalia msimu ujao wa ligi Simba inawatandika magoli 11 bila.

Mkuu sasa mbona hujasema pia kuwa hii Taarifa ya Heritier Makambo 'Kutua' Kesho Msimbazi ( SSC ) umeipata Sports Extra ya Clouds FM ya Leo?
 
Back
Top Bottom