GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,852
BENARD MORRISON KUMALIZA 'MASINEMA' YAKE NA YANGA
Shirikisho la kabumbu nchini Tanzania (TFF) limesema hukumu ya madai ya kughushi saini ya mchezaji Bernard Morrison itatolewa Agosti 10 baada ya kazi ya uchunguzi iliyofanywa na Jeshi la Polisi kumalizika.
Kiungo huyo mshambuliaji kutoka nchini Ghana aliishitaki Young Africans kwa TFF, akidai kuwa saini yake imefaniwa fojari katika mkataba wa miaka miwili, ambao klabu hiyo yenye maskani yake kwenye makutano ta mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam, imeuwasilisha TFF na Shirikisho la kandanda duniani (FIFA).
Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala amesema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za uchunguzi wa suala hilo na hawana haja ya kuwa na papara ili kupata majibu sahihi.
Mwanjala amesema awali walipanga kutoa uamuzi wa suala hilo mwishoni mwa mwezi Julai na baadaye kupeleka mwanzoni mwa mwezi huu, lakini walishindwa kufanya hivyo kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wao.
globalpublishers
Kuna Watu walidhani ule 'Uhuni' wao waliokuwa wakiufanya wakati JK Yanga Mwenzao akiwa Madarakani basi na kwa JPM huyu watauendeleza tu.