Wana Udom wadanganywa mswada wa katiba kufanyikia Chimwaga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana Udom wadanganywa mswada wa katiba kufanyikia Chimwaga

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by SOKON 1, Apr 8, 2011.

 1. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Baada ya jana wana Udom kupinga utaratibu wa watu kujifungia ndani na kuchangia mswada uku ukiacha mamia ya watu wakiwa nje hawajui la kufanya leo asubuhi wanachuo wengine wakiondoka mida ya saa kumi na mbili asubuhi kwa mabasi kuelekea mjini ktk ukumbi wa bunge wa zamani uku wengine wakijiandaa kwenda mida ya saa tatu mara habari ikaja chuo kuwa itafanyika chimwaga ila mpaka mda huu wa saa tano asubuhi hakuna dalili yoyote ya kufanyika.

  MY TAKE;
  Walichofanya serikali sio sahihi kwani kwa kuwahadaha watu kwa dhumuni la kufanya mambo yao uko ukumbi wa bunge ila naamini watafanya kila jambo ila hawataweza kuzuia mawazo ya watu wenye uzalendo wa nchi yao kwani baada ya Udom kuonesha wazi hawako upande wa serikali wakaamua kuwadanganya utafanyika ukumbi wa chimwaga uku fika sio kweli.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mi naona mambo yanachelwa ifanyike kama ilivyofanyika Tunisia na Egypt tumechoka kufanywa wajinga hawa wapuuuzi
   
 3. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waonee huruma mwanangu, hizi ni dalili kwmba tumeshawakamata pabaya.

  Jana tuliwafikisha kwenye mlima mkali tukawasukuma wakiwa kwenye gari waanze kuteremka, kumbe gari yao breki zimefeli!

  kuruka wataumia na pengine kufa, na kubaki kwenye gari wakati linateremka kwa kasi bila control wanajua wakifika bondeni ni kiama kitupu. matokeo yake wanahaha kama ifuatavyo

  1. public hearing ya Msekwa itafanyika mara mbili kwa siku (jana)
  2. mara wakasema itafanyika kwa siku tatu mfululuzo
  3. mara wakadai kwamba wanaodai fursa ya kutoa maoni ni wanafunzi tu! (as if siyo watz)
  4. mara wakadai wanaozomea ni chadema (as if siyo watz)
  5. leo wameahirisha bunge
  6. mara watakuja chimwaga lakini hawakuwa wamejiandaa hivyo hawajafika
  .
  .
  . (mpaka mswada utakapopitishwa hii list itakuwa ndefu sana.

  kwa ujumla hawakujipanga hivyo "they are managing by wondering about, and on ad-hoc basis"
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ccm naomba watambue kwamba sisi wa Tanganyika tunataka katiba mpya km wao wanadhani nchi yao basi tutaleta cha misri very soon!
   
 5. A

  Ame JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Wakati haya yakitokea hawajui chakufanya ndani ya chama chao dhidi ya hiyo migawanyiko ambayo iko kama ultra violet chain of reaction. I told them they could not listen they thought I was dreaming. Hawajui kuna power na powers this time they would understand that in this world some people are princes and whatever they say is a decree!
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Inabidi wajitahidi kuondoa hii aibu hawawezi wakawa na chuo kikubwa kuliko vyote nchini pale Dodoma washindwe kwenda kutumia ukumbi mkubwa ambao ungeingiza wananchi wengi zaidi hata wengine wangekuwa nje wangefuatilia kwenye screen jamani hilo nalo shida
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,079
  Trophy Points: 280
  Ndo hvyo... hawa wetu hawatoki hawa, tushawashka ...hawataweza kuwadanganya watu wote kwa mda wote,
   
 8. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali na chama kinachoiongoza havikuwa na Agenda ya kufanya Mchakato wa Katiba ndani ya Miaka
  mitano hii (2011-2015). Haya yote tunayoyashuhudia sasa ni zimamoto za kikwete sababu, mwanzoni
  kwa uoga alionao sababu ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi, na hivi karibuni uoga wa nguvu za
  UMA kama inavyoendelea kufanyika katika nchi za kiarabu ndio vilivyompelekea kuridhiwa swala la
  Katiba mpya.

  Hivyo, haijawahi kuwa moyoni mwa kikwete kuipatia katiba mpya Tanzania muda wowote kuanzia sasa,
  haijawahi kuwa ni mkakati wa CCM wala Serikali, wamedandia hoja ambayo hawako tayari kuisimamia
  na ambayo wanahofu kubwa kwayo kwamba haitawaletea faida bali anguko.

  Hivyo, Watanzania wanatakiwa wakumbuke wakati wote wakati wa mkakati huu, chochote
  kitakachoonekana kuwa kizuri huku kinatoka serikalini sio kweli, ni uongo,ktk swala la katiba hawaitaki.

  Tunachotakiwa kukumbuka ni kwamba, Mabadiliko ya katiba hayatawanufaisha wanasiasa walio ccm, wala
  viongozi wakubwa wa serikali, wakiachwa wafanye wanavyotaka katika mchakato huu wako tayari hata kuusitisha
  sababu unawapa kero
   
Loading...