Wana Tabora kumlilia Rostam na siyo Selelii! Wana nini?

akajasembamba

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
1,012
1,475
Nilisikitishwa na kufadhaika sana, kuona baadhi ya wananchi wa jimbo la Igunga wakiangua kilio na baadhi yao kupoteza fahamu kisa Mbunge wao Rostam Aziz kajiuzulu! Mbunge aligubikwa na tuhuma na kashfa lukuki,ambaye Tanzania nzima ilikuwa ikipaza sauti ya kumkataa wakiwemo wana CCM wenyewe! Mbunge ambaye Bungeni hachangii hata hoja moja kimya muda wote, alinukuliwa bunge lililopita kukaa kimya miaka yote! Najiuliza Wanyamwezi hawa wanaelewa haswa maana ya Mbunge?!

Au kwao wao ni MFADHILI anayegawa tu pesa na kugawa Mahindi na Vyerehani!!Bila kujua hizo gharama anazotumia pesa amezitoa wapi!! Anatoa hela mfukoni wakati bungeni anaachia mabilioni ya fedha zinazotokana na kodi walizotozwa wao wenyewe katika madini, mazao yao na ng'ombe wao yakipotea katika Bajeti mbovu!

Wanategemea maendeleo ya nchi yataletwa kwa fedha za mfuko wa mfanyabiashara mmoja na siyo Mbunge mwenye hoja nzito bungeni, anayehoji zinapokwenda fedha zinazotokana na madini yetu!! Wanatabora hao hao hatukuona wakilia walau tone moja kumlilia Mbunge GODWIN SELELEIII ambaye Watanzania wengi wenye fikra timamu walikuwa wakimpenda na kumtegemea kama mtetezi wao bila kujali ni wa chama gani!

Huu mkoa una tatizo wajiangalie upya.

Rostam Aziz ni kipenzi cha watu wa Igunga. Nyinyi hamukijui alichokifanya Igunga ndio maana munamkashifu. Aliyoyafanya Mkapa hakuna anayeyataja. Munamuogopa au kwa kuwa ni mwenzenu?. Rostam haja fanya jipya lolote isipokuwa alikifuata maagizo ya wakubwa tu.

wanatabora kweli walimlilia Rostam kuna mengi hata kwenye msiba kunamtu anaweza lia sana kumbe moyoni anashukru kuondoka kwa marehaemu ndio walichokifanya igunga walikuwa na furaha sana yakuondoka mwizi na mhujumu uchumi ndio maana walilia hata kudhirai

Hivi Mbunge anaechangia sana kwa kupiga kelele pale bungeni ndio unamuona ana maana sana?

Duhh, ikiwa Watanzania fikra zetu ni kama wewe, basi tuna kazi kubwa sana.

Wewe unajuwa katika wilaya za zenye Bima Tanzania zenye bima ya afya kila kata ni Igunga pekee? wewe unajuwa katika wilaya zenye mafanikio makubwa kwa muda mfupi wa Rostam kuwa Mbunge ni Igunga? nenda Igunga au waulize watu wa Igunga Rostam kafanya nini Igunga wakueleze. Unatuletea Selelii, Selelii kafanya nini zaidi ya kuserereka?

wanatabora kweli walimlilia Rostam kuna mengi hata kwenye msiba kunamtu anaweza lia sana kumbe moyoni anashukru kuondoka kwa marehaemu ndio walichokifanya igunga walikuwa na furaha sana yakuondoka mwizi na mhujumu uchumi ndio maana walilia hata kudhirai

Lete ushahidi wa hayo uyasemayo, au mtu akiwa tajiri basi kisha kuwa mwizi? kwa sababu tu wewe hujui uwe tajiri vipi?

Wakati tz anatuliza kidogo anawapoza watu wa igunga so lazima wamlilie as wengine walikuwa wanapata posho kwake za kuwaweka sawa wapiga kura so ulaji kushney

Kila mtu anajua Rostam alitumia umahiri wake ktk biashara kuwafungua macho akina mangula, mkapa na wenzake ili wafanikishe wizi wa fedha zetu, zaidi ya hapo hana kosa lolote. Rostam amefana makubwa saana kwa watu wa igunga kuliko mbunge yoyote
ktk jimbo lake ktk nchi hii. CCM wanajua fika Rostam personally hakuiba ila fedha zimetumiwa na CC wenyewe.
Watu wa tabora hawawezi kumlilia Selelii kwani yuko group moja na akina Sitta waliotufikisha hapo na siasa zao za chuki na kutumiwa na KANISA kuiangusha serikali

Pole Faiza Foxy kwa kukosa uelewa wa kujua kazi na majukumu ya MBUNGE unamsifu golikipa kwa kuwa forward striker na kufunga magoli!!!!????? Huku golini hakuna mtu na magoli yanaingia!!!! Mbunge na Bunge kazi yake ni KUISIMAMIA SERIKALI NA KUTUNGA SHERIA hakuna haja ya kuwa na bunge kama halisimamii serikali kodi tunayokatwa, na Mbunge wa aina hiyo unayoitaka wewe si Mbunge labda ungempa Ukuu wa Wilaya au U DED au Ufadhili wa Jimbo kama mtazamo wako ulivyo. Bima ya Afya??? Hata angejenga shule au nyumba kwa kila mwana Igunga hiyo ndiyo kazi ya bunge au Mbunge!!!! Mwisho wa siku tutakuja kuwa kama Colombia nchi itanunuliwa na wauza Bangi, kama kigezo chako cha kuchagua Mbunge ni hela anayopeleka jimboni kwake. Unamsifu Rais kwa kuhukumu kesi wakati Per Capital Income na G.D.P zinaporomoka!!!! YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOME TIMES BUT NOT ALL THE PEOPLE ALL THE TIME, Ipo siku watanzania wataamka. Its a total shame kumlilia Mbunge kama huyo na kuchekelea kifaa kama Selelii kikienda. Tanzania tutazidi kuwa Maskini kwa kuwa na watu wenye mtazamo kama wako!

mkuu ulitaka wamlilie selelii kwa ajili ya kupigana vita ya kinafiki iliyoitwa vita dhidi ya ufisadi kumbe ilikuwa ni kwa ajili ya maslahi binafsi?

Rostam Aziz ni kipenzi cha watu wa Igunga. Nyinyi hamukijui alichokifanya Igunga ndio maana munamkashifu. Aliyoyafanya Mkapa hakuna anayeyataja. Munamuogopa au kwa kuwa ni mwenzenu?. Rostam haja fanya jipya lolote isipokuwa alikifuata maagizo ya wakubwa tu.

Mkuu umesema kweli. Mkapa kafanya ufisadi zaidi ya Rostam, tena kwa kutumia ofisi/madaraka

Pole Faiza Foxy kwa kukosa uelewa wa kujua kazi na majukumu ya MBUNGE unamsifu golikipa kwa kuwa forward striker na kufunga magoli!!!!????? Huku golini hakuna mtu na magoli yanaingia!!!! Mbunge na Bunge kazi yake ni KUISIMAMIA SERIKALI NA KUTUNGA SHERIA hakuna haja ya kuwa na bunge kama halisimamii serikali kodi tunayokatwa, na Mbunge wa aina hiyo unayoitaka wewe si Mbunge labda ungempa Ukuu wa Wilaya au U DED au Ufadhili wa Jimbo kama mtazamo wako ulivyo. Bima ya Afya??? Hata angejenga shule au nyumba kwa kila mwana Igunga hiyo ndiyo kazi ya bunge au Mbunge!!!! Mwisho wa siku tutakuja kuwa kama Colombia nchi itanunuliwa na wauza Bangi, kama kigezo chako cha kuchagua Mbunge ni hela anayopeleka jimboni kwake. Unamsifu Rais kwa kuhukumu kesi wakati Per Capital Income na G.D.P zinaporomoka!!!! YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOME TIMES BUT NOT ALL THE PEOPLE ALL THE TIME, Ipo siku watanzania wataamka. Its a total shame kumlilia Mbunge kama huyo na kuchekelea kifaa kama Selelii kikienda. Tanzania tutazidi kuwa Maskini kwa kuwa na watu wenye mtazamo kama wako!

Kazi ya mbunge siyo kupiga gumzo bila kufikiria, wasemaji wazuri wengi sana wanakuwa ni wanasiasa na watendaji wabovu, mfano ni Nyerere. Rostam ni mtu wa action na ndio maana unaona mafanikio yake kwenye Ubunge na kwenye biashara zake binafsi.

Ni jimbo gani la Tanzania zaidi ya la Rostam lenye bima ya afya kila kata? hapo kishapiga teke adui maradhi kwenye jimbo lake. Jimnbolake lina shule nyingi zaidi ya wanafunzi, lina walimu wa kutosha kila shule, hapo kisha piga teke adui ujinga.

Bado hayakutoshi? Nipe mfano hai kama nnavyokupa mimi, Selelii kafanya nini kipindi chake jimboni kwake?

we faiza ulishafika lini Igunga, we si kila siku upo kariakoo, acha ushabiki, unanini weye!

mibaba selelii aliyeshindwa na bashe. watamlilia kwa kupiga kelele zisizo na mafaniko bungeni.

kujiuzulu kwa rostam kumewaumbua wabunge wengi. watu tumejua kumbe wabunge wetu sifuriiii
wabunge wangapi leo wanaweza kuziuzulu na wakaliliwa na wapiga kura wao.

RA hakuliliwa na wapigakura wake tu, kujiuzuru kwake kumeifanya hata CC ichanganyikiwe

Nilisikitishwa na kufadhaika sana, kuona baadhi ya wananchi wa jimbo la Igunga wakiangua kilio na baadhi yao kupoteza fahamu kisa Mbunge wao Rostam Aziz kajiuzulu! Mbunge aligubikwa na tuhuma na kashfa lukuki,ambaye Tanzania nzima ilikuwa ikipaza sauti ya kumkataa wakiwemo wana CCM wenyewe! Mbunge ambaye Bungeni hachangii hata hoja moja kimya muda wote, alinukuliwa bunge lililopita kukaa kimya miaka yote! Najiuliza Wanyamwezi hawa wanaelewa haswa maana ya Mbunge?!

Au kwao wao ni MFADHILI anayegawa tu pesa na kugawa Mahindi na Vyerehani!!Bila kujua hizo gharama anazotumia pesa amezitoa wapi!! Anatoa hela mfukoni wakati bungeni anaachia mabilioni ya fedha zinazotokana na kodi walizotozwa wao wenyewe katika madini, mazao yao na ng'ombe wao yakipotea katika Bajeti mbovu!

Wanategemea maendeleo ya nchi yataletwa kwa fedha za mfuko wa mfanyabiashara mmoja na siyo Mbunge mwenye hoja nzito bungeni, anayehoji zinapokwenda fedha zinazotokana na madini yetu!! Wanatabora hao hao hatukuona wakilia walau tone moja kumlilia Mbunge GODWIN SELELEIII ambaye Watanzania wengi wenye fikra timamu walikuwa wakimpenda na kumtegemea kama mtetezi wao bila kujali ni wa chama gani!

Huu mkoa una tatizo wajiangalie upya.

alikuwa anawasaidia kupata kazi za kuosha vyombo kwenye nyumba za waarabu na wahindi. hili kusema kweli ni pigo kubwa kwa watu wa mko huu ambao kwao umasikini wa fikra ni sehemu ya maisha yao.

Watu wa Igunga niwabinafsi,wameangalia maslai yao wala awakuangalia maslai ya nchi,wangeangalia maslai yanchi wasingeweza kumlilia fisadi ambaye alikuwa anaitumia igunga kujitengenezeanjia ya kvfanya ufisadi

Back
Top Bottom