Wana Simba SC wenzangu tuvumiliane ila ukweli wa mechi yetu ya tarehe 23 August, ni huu

Je ramli imeshindwa safari hii? Ha ha ha ha.
Kwa waislam ni haram kutazamia na kucheza kamari. Naona kutazamia na kamari safari hii imebuma.
 
Banyamulenge aka chura njoo basi utupe tena utabiri wako uchwara....!!! wee chura tena wa miguu 3...

Najua mtaumia ila kama kawaida yangu mechi ya mwisho ya Simba na Yanga nilikuja humu humu JF na kusema kuwa Yanga itafungwa kwa tofauti ya goli 1 na kwa kwamba kutakuwa na Kadi nyekundu na kweli ndicho kilichotokea na wengi wenu mlinitumia salamu nyingi sana za pongezi japo wapo ambao kabla ya mechi ile kuanza walinidhihaki na kunitukana mno humu Jamvini.

Basi wana Simba SC wenzangu kwa moyo ule ule ambao mlinipa wakati ule naomba leo tena zikiwa zimebaki siku tano ( 5 ) kuelekea huo 'mtanange' wa Dar es Salaam / Mzizima derby ya Simba na Yanga pia na leo mnivumilie na bahati nzuri hata Mimi ni mwana Simba SC mwenzenu tena wa Kindakindaki.

Nipo katika Kamati moja 'Nyeti' ambayo mechi iliyopita tulijitoa sana mhanga hadi kupelekea karibu kuhatarisha hata maisha yetu ili tu Simba SC yetu ishinde na kweli ilishinda. Kataeni kubalini ila mjue kwamba mechi hizi huwa zinachezwa mno 'Kiutamaduni' zaidi na pale Uwanjani huwa ni uwasilishaji tu wa 'majini' na 'tunguri'.

Ni kwamba hii mechi tumeicheza muda mrefu ila ni bahati mbaya sana kwamba Watani zetu Yanga FC 'wameshatutega' sehemu mbili kwanza Bandarini Dar na pale Bandarini Zanzibar ( Watu wa mpira hapa najua mtanielewa ) lakini kama haitoshi walipoenda Yanga FC ni kwa Mtu ambaye siku zote amekuwa 'akituumiza' Simba SC kwani alishawahi kuwa 'Mtaalam' wetu mkubwa ila mmoja wa Viongozi wetu ( ambaye sasa yupo ndani ) alimdhulumu Pesa yake na Yanga FC japo hawana Hela ila wamemfuata huyo huyo kama walivyofanya huko nyuma na mara zote walitufunga.

Ukweli kamili wa mambo ni huu ufuatao na sikulazimishi uukubali ila tunaoihangaikia Simba SC 'Kiutamaduni' hatuna busi kuliweka hili mapema ili wana Simba SC kuanzia leo Ijumaa tuanze kujiandaa Kisaikoloji japo mbele ya Mungu lolote linaweza kutokea na lisitokee ila Mimi hapa nawasilisha 'ripoti' ya masuala yetu haya ya 'Kiutamaduni'.

1. Simba SC tutafungwa goli 1 tena Kipindi cha Kwanza

2. Kuna Kadi Nyekundu za kila Upande ila upande mmoja utamkosa Mchezaji wao muhimu

3. Kipindi cha pili mpira utasimama kwa muda kwani kuna Mchezaji ataumia vibaya

4. Kuna fujo kubwa sana itatokea wakati wa Mapumziko katika moja ya Jukwaa

5. Kuna Nyuki watakatiza Uwanjani ila kuna Njiwa watarushwa na hawataruka

6. Kuna goli litafungwa ila litakataliwa

7. Huenda kabla ya mechi au siku ya mechi au baada ya mechi mmoja wa Viongozi wa hizi Timu tusiwe nae tena duniani

Mtaalam wetu wa mwisho aliyeko Morogoro kasema kuwa anaweza 'Kuicheza' hii mechi na Simba SC tukashinda ila amesema kuwa inabidi 'Kiongozi' mmoja wa Kamati ya Utendaji au wa Matawi ajitoe 'mhanga' Kufa ili 'Nyota' ifunguke kwani 'Kufuru' ambalo Yanga FC wametufanyia Simba SC ni la hatari mno.

Najua fika kuwa Wana Simba SC wenzangu tuna jeuri kwakuwa tuna Kikosi kizuri na imara kuliko Yanga FC na wala hili halina 'ubishi' ila tambueni kuwa hizi mechi huwa zinachezwa sana 'Kiutamaduni / Kindumba' na kuna mengine yanafanyika ambayo nisingependa kuyaweka hapa hadharani kwani naweza nikawatisha au kuwakatisha Watu tamaa.

Hata hivyo Mwenyezi Mungu nae ana yake hivyo wana Simba SC msikate tamaa labda Maulana anaweza kutusaidia na tukashinda ila hadi muda huu tunamaliza 'Kuhangaika' kwa hawa 'Wataalam' wetu bado kuna goli 1 ambalo Yanga FC wanaenda kutufunga na litakuwa la Kipindi cha Kwanza na litakuwa goli lisilo hata na utata wowote.

Naomba radhi kwa nitakaowakera kwa hii taarifa ila nimeona nisiwaficheni kwa kinachoendelea!

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom