Wana SESESCO 1990's,mnaikumbuka Chaka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana SESESCO 1990's,mnaikumbuka Chaka?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Konzogwe, May 4, 2009.

 1. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mliopita sengerema sec hebu tukumbushane mawili matatu.
   
 2. tzengo

  tzengo Member

  #2
  Jul 4, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mkuu heshima yako.
  nimesoma chaka nikakumbuka mambo mengi na hadi sasa naamini chaka bado ipo.kulikuwa na mambo ya kunywa kangala na kula machimbo.
   
 3. Robweme

  Robweme Senior Member

  #3
  Jul 5, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu;
  umenikumbusha mengi, je mnamkumbuka katendele mzee wa kupenda kuku, mnamkumbuka yule mama rose, aliyekuwa anapika wali na kutuuzia.Nawakumbusha trip za nyampurukano kutafuta maji ya kunywa ya kisimani kupitia nyazugo road.Mkuu unaikumbuka ile baha maarufu ya bulawayo pale karibu na chuo cha maendeleo ya jamii.
  Sijui kama lile bwawa tulikuwa tunafuata maji ya kunywa bado lipo, tuliogelea sana bwawani sesesco haikuwa na maji kipindi hicho.
  Mzee Igosha na headmaster sijui wapo au, ilikuwa miaka ya 1995-1997.
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Daayum, and I thought wali wenye mijiwe wa Mwinyi was such a bad deal.
   
 5. tzengo

  tzengo Member

  #5
  Jul 5, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mkuu robwene bwawa naamini bado lipo.
  Kuna taarifa nilipata Mr Matu(headmaster wakati ule) alifariki dunia last year.
  Umenikumbusha Mr katendele nilisikia alipewa ukuu wa shule sijui wapi,na huyo mama rose na wali wake duh.ukiacha bulawayo unakumbuka maeneo ya Alfa & Omega?umenikumbusha pia mambo ya maji ya nyampu ambapo pamoja na umbali bado ulitakiwa kupata lita tano tu.
   
 6. Robweme

  Robweme Senior Member

  #6
  Jul 5, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu unakumbuka Ibisabagenyi,unamkumbuka mama igosha na igosha, nakumbuka alikuwa hapendi watu kuvaa sweta, nililamba viboko vyake viwili wakati ule.
  Unakumbuka vyoo vya sesesco, ilikuwa inabidi kuvikwepa tunakula winga la kuelekea chaka baada ya lunch.
  Mkuu mmoja amenikumbusha machimbo, saa nne wakati wa break.Mnakumbuka mwalimu manoni mzee wa chemistry ,mwalimu rugaimukamu aka "buga" mzee wa chemistry pia sijui wako wapi.
  Kweli mwalimu matu alifariki, nilikutana na kijana wake ambaye ni mkuu wa chuo cha uganga mugumu.Mungu amlaze mahari pema peponi.Nimekumbuka mvua ilivyokuwa ikinyesha, kinyesi kinatililika hadi bwawani tulikokuwa tunachota maji ya kuoga jioni na asubuhi aisee yalikuwa yanawasha sana baada ya kuoga.
  Nimemkumbuka jamaa mmoja alikuwa anaitwa mwita alikuwa baunsa wa misosi wakati wa foreni la chakula bwawani.
  Nimewakilisha.
   
 7. locust60

  locust60 Senior Member

  #7
  Jul 6, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Du robweme.
  umenikumbusha mbali sana yaani singapole.nimekumbuka maji ya nyapulukano na samaki wa sokomjinga kweli siku zinasonga.kusomea chemli na karabai kweli haikuwa rahisi.Namkumbuka mama Igosha alikuwa anatujuza geography,Kamungo Math na Physics.
   
 8. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Da!...Nasikitika kumbe "Kenge" ameshadead!.Naikumbuka ile fimbo yake ya kufuli la baiskeli,siku moja aliadhibu walokole walikuwa wakisali chini ya meza sisi acha tucheke.Igosha siku moja tulikutana Moro yuko na kale katoto kake ka mwisho ka kike,aliniambia ameshastaafu na anaishi maeneo ya Mzumbe na hako katoto kanasoma secretarial VETA 1st year.Malemba yuko Kilosa na Kachecheba nilisikia yupo Kilombero Moro anabiashara.Aisee nikikumbuka siku moja kajenereta kaliibiwa kwenye gradu acha tukimbie tukaambulia patupu.Ndiyo kama tungetumia majina yetu halisi humu jf nadhani kati yetu yupo tulichunga nae ng'ombe,au tulikunywa nae tangawizi busisi road kwa mzee Iddi,au tulipigwa mnyengo pamoja nae kwenye bondo,maana namkumbuka Mwita,Okonkwo,Maganga,Labda Mishamo,Buzinzira hawa jamaa walikuwa noma.Natamani kujua Ndaki ndugu yake Mattu yuko wapi sasa,Masanja secretary alikuwa msabato nae yuko wapi,Bahati Sosthenes na hizi ndume zilitoka Tambaza?Escoba,gamtu,msimbano.Ebwana eeeh!!Nitafurahi zaidi kuendelea kupata habari za wana singapore.
   
 9. tzengo

  tzengo Member

  #9
  Jul 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mkuu konzogwe,
  umenikumbusha mengi sana hayo majina uliyotaja kweli yanarudisha kumbukumbu zangu singapore.na yale mambo ya kuchunga ng'ombe chaka nakumbuka jamaa wakiwa zamu kuchunga wanapata bondo lao mapema na hakuna mnyengo maana kundi la kina mwita walikuwa hawatanii.nakumbuka miaka kama 5 imepita nilikutana na maganga Mwanza akasema ni mwalimu maeneo ya Igogo,na hiyo mijitu ya tambaza namkumbuka dogo mmoja alikuwa anajiita OG-kweli sesesco kipindi kile ilikuwa na raha yake.
  umenikumbusha pia kachecheba,jamaa alikuwa anachapa kwa sifa sana na biashara yake ya kupiga picha.unamkumbuka mwalimu msela?jamaa alifukuzwa ama aliacha kazi,niliwahi kumuona miaka ya 2000/01 jamaa kweli hakuwa katika hali nzuri,sijui yuko wapi kwa sasa.mnamkumbuka yesu wa kiswahili?mwalimu mbogora,mzee elifuraha,msungang'humbi,bituro,yohana,wile na yule mwalimu aliyekuwa na papara alikuwa na mvi na kipara fulani hivi?mnakumbuka mambo ya kusomba maji kutoka bwawani?
   
 10. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu tzengo,
  umenipa raha sana!! Yesu wa kiswahili bwana alinifundisha,nakumbuka siku moja aliandika maneno "mathematical set" kwa mwandiko wa kisanii sana then akarudi nyuma na kunyanyua mikono juu kibingwa.Msela niliwahi kukutana nae Kahama mine akiwa pombe sana akaniomba 500 nikampa kwa huruma.Namkumbuka pia ticha wangu wa FineArt Magambo na kiingereza chake "i plant plant here mwabaruhi" akimaanisha napandapanda hapo mwabaruhi na ile "near bwana" akimaanisha karibu bwana.Da! Inanipa raha sana.Unamkumbuka Charles Metela? Huyu jamaa nakumbuka alikuwa refa kwenye ka mgomo fulani kalipelekea shule ifungwe.Halafu kuna mkuu mmoja amenikumbusha Bulawayo inn,pale alikuwepo binti wa boss anaitwa Rose Mlela alikuwa akisoma Nyampu aliwah kuwa rafiki yangu.
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tehe tehe tehe ...!!!

  Mkuu Konzogwe umenikumbusha mbali sana! Wengine tulikuwa huko miaka ya '80s na CHAKA likuwepo na wakati huo bwaloni paliitwa MAPUTO.

  'MAbuga' wa Chemistry? na Elifuraha tulizoea kumwita 'BALBU'. Mr. Gambo na Ki-english chake?
   
 12. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 180
  Wanaoifahamu chaka zaidi ni wale waliopita pale o-level,Namkumbuka sister kutoka indonesia aliyekuwa akitufundisha advanced maths,nilisikia alihamia Tambaza.Namkumbuka Manoni mwalimu wa chemistry,sasa ni miaka 11 tangu nimalize six pale.
   
 13. tzengo

  tzengo Member

  #13
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  heshima yako mkuu kakalende,
  naona ulikuwepo sesesco zamani sana sijui unafahamu hilo jina buga lilitokana na nini?maana wengine tulilikuta na hatukujua maana yake japo ilikuwa hatari sana kama ukikamatwa na mwenye jina ukijaribu kulitumia.
   
 14. b

  babalynn Member

  #14
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule sister alikuwa anaitwa Sr Laura aisee, na yule jamaa alikuwa anafundisha Geography A level na English yake ya ajabu Mr Igoshi yuko wapi jamani?
   
 15. Robweme

  Robweme Senior Member

  #15
  Jul 19, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu locust, asante kwa kunikumbusha teacher kamungo, kwa fluid mechanics, alikuwa mchawi sana, ila noma alikuwa haieleweki sana.
  Aisee maisha ya sengerema miaka ya tisini ilikuwa nuksi ingawa yalikuwa ya shida.
  Hivi kamungo yuko wapi?, nimeenda sengerema mwaka juzi, aisee kumebadilika sana, hakuna mwalimu nilimfahamu pale.Wote walikuwa wapya.
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huyu mabuga aliingia pale mwaka 1986 kutokea Old Moshi, suruali zake zote suruali zilizoshonwa kwa staile ya miaka ya '70 enzi hizo ikiitwa 'bugaluu' - inabana sana matakoni na pana sana miguuni, basi wanafunzi wakampa jina la 'mabuga' alikuwa anavaa 'raizoni' vilevile.

  Alipewa darasa la Chemistry form 4 ya 1987 na mwaka huo walivunja rekodi ya kufaulu. Tangia wakati huo, Mabuga akawa mtu muhimu sana SESESCO na kukabidhiwa ukuu wa idara.
   
 17. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,363
  Likes Received: 6,701
  Trophy Points: 280
  wakuu mnamkumbuka sister laura!!du long time nasikia alijitoa duniani!!
  singapole ilichafuka 97 washikaji tukigomea ugali wa mwita!!hivi huyo mwita yuko wapi?hivi aliendelea kitaaluma kweli yule jamaa!!manake alikuwa ana mind zaidi jiko kiliko shule!
   
 18. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 180
  Alijitoa duniani maana yake nini?hebu fafanua..
   
 19. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,363
  Likes Received: 6,701
  Trophy Points: 280
  alijitoa duniani!maana yake ni kuwa alicomit suicide!!sababu siijui!!
   
 20. tzengo

  tzengo Member

  #20
  Jul 23, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Asante sana mkuu,
  Umenipa furaha sana maana Miaka yote nilikaa Sesesco hadi leo hii sikuwahi kujua asili ya jina hilo.
  Mkuu Zamaulid
  hilo la sister Laura kujitoa duniani kama ni kweli ni habari mbaya sana.mchango wa sister Laura kwa SESESCO ulikuwa mkubwa sana na utakumbukwa daima.
   
Loading...