Wana MMU kuna ID humu naitafuta, nikiipata natangaza ndoa rasmi na vikao vyote vitafanyika humu

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,268
2,000
Ndugu zangu wana MMU kwanza naomba nimshukuru mungu kwa kuniponya na lile gonjwa kwa kweli ni kwa neema zake tu mimi kuwa hai

Kuna ID humu imepotea kwenye macho yangu, Ile ID ambayo inaogopwa na wanawake kwa wanaume wote hapa jukwaani ambayo iki-comment sehemu ID za kike zote haziwezi kum-QUOTE kwa hali ya uhasi zaidi watagonga like kuonesha wako upande wake, Ile ID babe kwelikweli neno lake moja ni kama ngumi yenye uzito wa tani 10 ambayo inaogopwa hata na uongozi wa jukwaa hili Mzigua90 na financial services ni baadhi tu ya wadada nilioshuhudia wakipitia dhihama za hii ID babe ya kike ninayoipenda

Mama Debora uko wapi mpenzi? Jitokeze nitangaze ndoa mama, sikuoni kabisa tangu nipone nafahamu umuhimu wa kuwa na wewe kwenye maisha yangu hata tukivamiwa na vibaka au majambazi utasaidia kushambulia sio wale wa kujificha ufunguni, na najua kabisa lazma utakuwa kiongozi wa VICOBA mtaa tutakaoishi na hakuna atakayekuuliza kuhusu pesa hizo hivyo mboga hazitatupa shida kabisa kwetu Pia utanifanya nisiwe na michepuko, nani atakubali kuwa mchepuko wangu kwa huo ubondia wako mama na wifi zako (dada zangu) vile viherehere vya kiwifi hawatathubutu kukuletea maana wanajua makwenzi utakayokuwa unawapa,niko radhi uwe mwandani wangu wa maisha wewe jitokeze tu hapa nijue kama uko hai bado

Usije kufikiri nina nia mbaya ukaja kunitolea michambo😊 la hasha! mimi nahitaji tufunge ndoa ya maisha, nafahamu kabisa kwako hakutakuwa na stori za kimbeya wala kuletewa udaku na utanifanya nijifunze Judo au Karate maana tukianzisha mtiti mtaa mzima lazima usimame na utanifanya niwe mwanaume imara na si kama wale wa Kinondoni, hakika mpenzi mimi nakuhitaji sana wewe nambie tu uko wapi mimi nitakufata. Na naomba nitoe tahadhari ukicomment vibaya kumhusu JIANDAE KWA YATAKAYOKUKUTA AKIJA HAPA na kwa hilo mimi sitahusika kabisa :D :D :D , mimi lengo langu ni kumchumbia tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom