Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Joel360

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
981
631
Habari zenu wana-MMU.

Nataka maoni yenu katika hili swala. Swala hili linaonekana la ajabu kutokana na mila na tamaduni zetu za ki-Afrika ila SIO DHAMBI kabisa.

Mimi siitaji kuja kuwa na mtoto katika maisha yangu yote ila nataka kuoa niwe na mke TU. Hii ni kawaida sana kwa nchi za ulaya na marekani unakuta kuna familia/ndoa za namna hii nyingi sana lakini sio hapa Afrika. Hapa nyumbani(Tanzania) formula ni Ndoa = Watoto.

Ili ndoa ionekane imefanikiwa basi iwe na watoto japo mimi binafsi siamini hivyo.

Katika maamuzi hayo yawezekana ntakumbana na changamoto nyingi, lakini Kubwa ni Kupata mwanamke ambae atakubali kuwa ndani ya ndoa bila mtoto.

Wana MMU nipeni maoni yenu kuhusu hili swala kwa sababu sijiskii KABISA kuwa nina deni la kuwa na mtoto, sina tatizo lolote kiafya la kunizuia kuwa na mtoto ila SITAKI TU.

1. Mna maoni gani ?

2. Je, kuna msichana ambae anataka kuolewa lakini hana mpango wa kuzaa ?(kama baadhi ya wanawake wa ulaya/marekani)

Asanteni, mchana mwema.
 
Lakini kutia unatia? ama ndio wale wa kulala na mwanamama halafu wanaishia kuugulia maumivu ilhali chiu wanautaka?
 
furaha ya maisha ni watoto hasa wa kuwazaa mwenyewe,, kwahivyo mkuu acha kutulisha matango pori sema tu ukweli kuwa una tatizo la kutopata mtoto basi,, ikiwa ni kweli sasa kuna ulazima gani wa kuoa ?,
 
furaha ya maisha ni watoto hasa wa kuwazaa mwenyewe,, kwahivyo mkuu acha kutulisha matango pori sema tu ukweli kuwa una tatizo la kutopata mtoto basi,, ikiwa ni kweli sasa kuna ulazima gani wa kuoa ?,
Kwani mwanamke ukishazaa nae watoto wajibu wake unakuwa umeisha ndani ya ndoa ?
 
Back
Top Bottom