Uchaguzi 2020 Wana Mbeya Tumekukataa Mh. Tulia

Hii nimeichota sehemu...

TULIA HATOSHI, NI KIRUSI KINACHOIGAWA CCM MBEYA

Mh. Tulia Ackson kazungukwa na watu wa ovyo. Kwanza ana haraka sana. Kitendo hiki kinawakera Mbeya tofauti na yeye na watu wake wanavyodhani.

Sawa anaweza kuwa mgeni kisiasa. Lakini hawezi kuwa mgeni wa hulka za wana Mbeya. Spidi yake inachefua kuliko kuvutia.

Amepania kubeba bendera ya CCM Mbeya mjini 2020. Lakini harakati zake zinapingana na ukweli halisi. CCM tukichanga karata vibaya 2020 tutasaga meno. Hili halihitaji mnajimu wa nyota.

Anataka kura za watu anaojitenga nao. Magari na ving'ora, misafara na mapikipiki ya nini Mbeya? Watu unaotaka wakupe kura zao hutaki wakukaribie. Unawaogopa wapiga kura wako?

Tulia hatakiwi hata kupandisha vioo vya gari akiwa Mbeya. Siasa ya Mbeya ni ngumu sana kwa sababu watu wanajielewa.

Hata askari anaowatumia hawalipwi posho. Na yeye hawapozi hata na maji ya kunywa. Utasema ni kazi yao kulinda viongozi. Lakini tambua pale anataka kuwawakilisha mpaka hao polisi.

Siasa hufanya kiongozi awe mtumwa wa wapiga kura. Tulia anataka wapiga kura wawe watumwa wake. Ni ngumu kumuuza 2020.

Tunajua anataka Uspika. Lakini Mbeya ya sasa inahitaji uwakilishi wa Mbunge mwenye mashiko. CCM tusimamishe mtu anayeuzika.

La sivyo hatuwezi kupambana na Chadema ya Mbeya yenye Sugu, kwa kumtumia Tulia. Tunajidanganya wana CCM, hilo litakuwa zoezi gumu kuliko lile la 2015.

Mh.Tulia ameigawa CCM. Kuna CCM 'Team Sugu' wa kimya kimya. Anamharibia hata Mh. Rais kwa kujinasibu kuwa kamtuma. Mbeya hawapendi kuburuzwa na hawataki mtu aliyetumwa, au tumesahau ya Bruno Mpangala?

Tulia hana muunganiko (connection) na Mbeya Jiji. Hata nyumba ya kuishi kaanza kujenga hivi sasa ili kuhalalisha achagulike. Tujue kwamba Mbeya sio wajinga. Hawawezi kuacha kumchagua Sugu, kwa sababu ya mgombea anayewaza Uspika. Tutachemka.

Lazima chama kiwe na watu wanaouzika. Wenye mashiko ndani ya Mbeya. Tukiwa vichwa ngumu kwa kushupaza shingo zetu. Sugu atarudi bungeni kwa kura nyingi zaidi kuliko rekodi yake ya 2015.

Ndimi mwana CCM,
Edwin Mwakanyamale,
Forest Mbeya.

Ndaga tununu.
 
Kama mkitaka maendeleo mbeya nendeni na Tulia coz anaushawishi mkubwa kwenye serikali hii ya awamu ya Tano, ila kama no ushabiki basi zichangeni karata deny vintage.
Maendeleo unayatafuta mwenyewe usitegemee kuletewa na mbunge utasubiri sana
 
Kama mkitaka maendeleo mbeya nendeni na Tulia coz anaushawishi mkubwa kwenye serikali hii ya awamu ya Tano, ila kama no ushabiki basi zichangeni karata deny vintage.
Una maana na gani?
Yaani nchi hii tumeigawa kuwa wale waliwachagua wapinzani wasiletewe maendeleo, vipi kodi zao wachukue au nazo waziache?
 
Kama mkitaka maendeleo mbeya nendeni na Tulia coz anaushawishi mkubwa kwenye serikali hii ya awamu ya Tano, ila kama no ushabiki basi zichangeni karata deny vintage.
[/QUOTE

Kumbe maendeleo sio haki ya wananchi, bali ni kwa upendeleo wenye ushawishi
 
Sio tu kirusi bali kirusi hatari,Mtu anashindwa kufadhiri vikundi vya akina mama kuanzisha taasisi ya kusomesha watoto wa wajane eti anaanzisha Taasisi ya Marathon asee only in TZ.
 
Hii nimeichota sehemu...

TULIA HATOSHI, NI KIRUSI KINACHOIGAWA CCM MBEYA

Mh. Tulia Ackson kazungukwa na watu wa ovyo. Kwanza ana haraka sana. Kitendo hiki kinawakera Mbeya tofauti na yeye na watu wake wanavyodhani.

Sawa anaweza kuwa mgeni kisiasa. Lakini hawezi kuwa mgeni wa hulka za wana Mbeya. Spidi yake inachefua kuliko kuvutia.

Amepania kubeba bendera ya CCM Mbeya mjini 2020. Lakini harakati zake zinapingana na ukweli halisi. CCM tukichanga karata vibaya 2020 tutasaga meno. Hili halihitaji mnajimu wa nyota.

Anataka kura za watu anaojitenga nao. Magari na ving'ora, misafara na mapikipiki ya nini Mbeya? Watu unaotaka wakupe kura zao hutaki wakukaribie. Unawaogopa wapiga kura wako?

Tulia hatakiwi hata kupandisha vioo vya gari akiwa Mbeya. Siasa ya Mbeya ni ngumu sana kwa sababu watu wanajielewa.

Hata askari anaowatumia hawalipwi posho. Na yeye hawapozi hata na maji ya kunywa. Utasema ni kazi yao kulinda viongozi. Lakini tambua pale anataka kuwawakilisha mpaka hao polisi.

Siasa hufanya kiongozi awe mtumwa wa wapiga kura. Tulia anataka wapiga kura wawe watumwa wake. Ni ngumu kumuuza 2020.

Tunajua anataka Uspika. Lakini Mbeya ya sasa inahitaji uwakilishi wa Mbunge mwenye mashiko. CCM tusimamishe mtu anayeuzika.

La sivyo hatuwezi kupambana na Chadema ya Mbeya yenye Sugu, kwa kumtumia Tulia. Tunajidanganya wana CCM, hilo litakuwa zoezi gumu kuliko lile la 2015.

Mh.Tulia ameigawa CCM. Kuna CCM 'Team Sugu' wa kimya kimya. Anamharibia hata Mh. Rais kwa kujinasibu kuwa kamtuma. Mbeya hawapendi kuburuzwa na hawataki mtu aliyetumwa, au tumesahau ya Bruno Mpangala?

Tulia hana muunganiko (connection) na Mbeya Jiji. Hata nyumba ya kuishi kaanza kujenga hivi sasa ili kuhalalisha achagulike. Tujue kwamba Mbeya sio wajinga. Hawawezi kuacha kumchagua Sugu, kwa sababu ya mgombea anayewaza Uspika. Tutachemka.

Lazima chama kiwe na watu wanaouzika. Wenye mashiko ndani ya Mbeya. Tukiwa vichwa ngumu kwa kushupaza shingo zetu. Sugu atarudi bungeni kwa kura nyingi zaidi kuliko rekodi yake ya 2015.

Ndimi mwana CCM,
Edwin Mwakanyamale,
Forest Mbeya.
Betina hafai hata kidogo.
 
Mliotumwa humu mnajisumbua bure kwasisi wakazi wa Mbeya hadudanganywi tunataka maendeleo na Dr Tulia ameonyesha mfano
 
Back
Top Bottom