chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 11,996
- 20,644
Sisi MATEGE msituone tuko kimya, tuna mawazo sana, tulijua tungemaliza miradi mingi 2021, baada ya hapo tukaanza nyimbo za kuimba na kusifu mafaniko na kumpa send off jamaa yetu iliyojaa furaha na jina lisilosahaulika kwa wananchi.
Ng'ombe wa masikini hazai, kamekuja ka korona, biashara zimesimama,kodi hazilipwi, na sisi wakandarasi wako saiti wanasubiri hela.
Kwa kawaida wanapoondoka, hupenda kuacha alama za kukumbukwa, naona miradi ya alama inaweza isiishe,na wataalam wanasema haka ka kirusi kanaweza kurandaranda mtaani kwa miaka miwili mpaka 2022, sasa tunabakiza miaka miwili au mmoja na nusu, hapohapo tufufue uchumi,ndipo tupate hela za kumalizia miradi.
Halafu huwa inakuwaje kwamba kipindi cha pili cha uongozi huwa kanatokea ka kitu kanakomfanya aliyeshika hatamu aonekane namna gani mbele ya jamii?