Wana-Kilimanjaro/Moshi fanyeni maombi walau mvua inyeshe!!!

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,099
630
Wanajamvi....

Binafsi nimekuwa na tabia ya kupenda kutembelea Mkoa wa Kilimanjaro hususani wilaya ya Moshi mjini. Na kwa wakati huu niko Moshi, japo mimi si mwenyeji wa Mkoa huu ila huwa napenda kuja bila kujali ni mwezi gani au wakati gani.

Ki ukweli hali ya Mji wa Moshi si nzuri kabisa, joto la ajabu ajabu sijui linatoka wapi!! Kwa kweli nduguzangu mmepoteza uzuri wa mji wenu. Na huenda tunatunza tuu mji kwa kusafisha wakati hatujali kutunza miti wala kupanda miti. Joto kali, utadhani uko nchi ya Jangwani kumbe ni moshi.

Nduguzangu kama mmeshindwa kurudisha uoto wa asili, basi anzeni kusali na kumlilia Mungu walau mvua inyeshe. Hali ya joto ni kali sana, nilidhani nitakaa mpaka January lakini sidhani kama nitaweza.

Kwetu Dodoma panafahamika, kwa hali yake ya joto kutokana na asili ya mkoa wetu. Sasa nyie ambao mlikuwa na mji mzuri mmeuharibu kwa tamaa zenu. Kesho itabidi nifanye utafiti katika maeneo mengine ya nje ya mji walau nione, na nitarudi kuwapa majibu.

Nduguyenu,

Mandla.
 
Back
Top Bottom