Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 4,941
- 6,191
Acha ni kujibu tu nikiwa mwanakigoma.Wanakigoma ambao ni waha, manyema, watongwe, wajiji, wagoma, wabembe na wafipa na watutsi wachache.Ukifika Kigoma ni mji uliokauka sana kimaendeleo japo imepakana na nchi zaidi ya mbili. Mbaya zaidi harufu ya kule ni harufu ya kichawichawi. Wenyeji wa huko wamelogezewa ubishi wa kijingajinga tu.
Jamani wanakigoma jengini kwenu, embu igeni mfano wa watu wa Kaskazini kama wa Kilimanjaro, Arusha na atlist Tanga.
Yani hadi wapemba na waunguja wamewazidi kimaendeleo na huku wako visiwani. Acheni hizo bana jengeni kwenu.
Futeni hiyo sifa ya kijinga mnayojisifia ya uchawi. Mkiendekeza mtaendelea kuwa masikini hadi sana.
Watu wa kigoma asilia wamehamia kutoka nchi za jirani karne nyingi zilizopita.
Watu wa kigoma kiasilia they are migratory people.Hivyo wamesambaa mikoa mingi.
Watu wa kigoma ni makabila ya kwanza kuanzisha miji hapa nchini kuanzia kigoma ujiji, tabora mjini, mwanza mjini, Dar, morogoro nk.
Watu wa kigoma ni kati ya makabila yalioweza kumiliki viwanja mapema zaidi, kuanzia kariakoo, magomeni, tandika nk ambapo nyinyi mlikuwa bado mnawinda ngedere huko kijinini kwenu.
Watu wa kigoma waliupokea ustaarabu mapema zaidi kuliko wasukuma, wanyamwezi nk.Watu wa kigoma walielimika mapema zaidi kuliko makabila mengi(elimu ya kiarabu).
Watu wa kigoma walikipokea kiswahili mapema zaidi ya makabila mengi tz na ndio lugha kuu pale sio kama mbeya hadi mjini kinyakyusa na kisafa kwa kwenda mbele.Watu wa kigoma(manyema) are travellers, ni watu wanaosafiri na wametawanyika nchi nyingi na mikoa mingi kuliko mnavyofahamu.
Watu wakigoma nii watu wa mabadiliko katika nyakati.
Watu wa kigoma ni watu wanaojifunza na wadadisi wa mambo na hutaka kuyajua kiundani.
Watu wa kigoma ndio watu wa kwanza kupata elimu ya kimazingira ya majini na uvuvi.
Watu wa kigoma ni watu wanaojitoa mhanga kubadili hali zao kiuchumi bila ya msaada wa serikali.
Watu wa kigoma ndio watu wanaomiliki maduka mengi mikoa ya kanda ya ziwa.
Watu wa kigoma ndio watu walioitawala biashara ya masoko kuanzia kariakoo na mikoa ya kanda ya ziwa(ikumbukwe kigoma huzalisha kwa wingi zaidi dagaa, maharage, tangawizi, mawese, sabuni, mihogo, na madini pemba nk).
Watu wa kigoma wengi tu wamesoma pengine kuwazidi makabila mengi japo serikali iliwatenga kwa miaka mingi kutokana na mrengo wa kidini.
Watu wa kigoma ndio wajanja wa mjini utawakuta magomeni, kariakoo, ilala tandika nk.wanapiga dili
Watu wa kigoma ni watu wenye vipaji vikubwa vya sanaa hadi yule wa ulaya kwao ujiji.
Watu wa kigoma wanastrago kwa nguvu yao zaidi kuliko favor za serikali.
Watu wa kigoma uchumi wao ulisimama kutokana na vurugu za kivita za nchi jirani,
Watu wa kigoma ndio watu wa kwanza kuleta mageuzi nchini na mbunge wa kwanza wa upinzani ambae alikuwa Dr.Amani Kaburu.Baadae majimbo yote yalikuwa ya upinzani(sio jambo dogo ila kwa mtazamo wako finyu ni jambo dogo).
Watu wa kigoma walitengwa na serikali ya ccm kwa miaka mingi ikiamini eti sio watanzania ni wakongo na warundi, rejea kesi ya kakobe.Hivyo serikali hii haikujenga miundombinu mpaka awamu ya JK na Magu, lami na SGR (Thanks kwao).
Watu wa kigoma ndio walima tumbaku wakubwa urambo nk.
Watu wa kigoma ni watunza mazingira wakubwa kuliko makabila mengi hasa nyanda za juu kusini na kati ambao huchoma hovyo misitu, walichoma mpaka mlima Rungwe ambao unahistoria.
Kigoma ni kati ya mji unaovutia kimazingira it is very green.Hivyo acha kupotosha.
Watu wa kigoma ndio watu waliotunza mapori yao na wanyama wao tangu enzi za mababu sasa wameingia "fisi" na man'gombe yao baada ya kuharibu kwao.
Nimalizie kwa kusema watu wa kigoma wanachakula cha kujitosheleza na kulisha mikoa ya jirani pamoja na kutengwa na kubezwa tunailisha Tabora, Mwanza, Shinyanga, Singida Dar, na hawajawahi kumbwa na njaa tangu dunia ianze na hii hupelea kuwa na afya nguvu, mvuto wa sura na maumbile yasiofubaa kama makabila mengi.
Mwisho usipende kuwabeza watu wa kigoma wanahistoria kubwa katika nchi hii pengine kuliko kwenu huko na huwafahamu vya kutosha uliza ndugu ujibiwe usikurupuke.Karibu kwa hoja