Wana Kagera wa Dar misaada yenu inawafikia walengwa?

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
unnamed+%2820%29.jpg


Sipendi kubeza jitahada za wadau hasa wanaoishi katika jiji la shida na raha la Dar salaam kuendesha harambee na harakati za kuchangia sekta kadha katika mikoa ya walikozaliwa.Matukio ya aina hii ni mengi lakini leo naongelea ‘harambee ya kuchangia maendeleo ya jimbo la Nkenge' iliyofanyika jijijini Dar na kuhudhuria na makamu wa rais dk ghalib bilali ambapo jumla ya fedha sh milioni 114 zilichangwa na kati yake milioni 65 zikiwa ni taslimu.Nawapongeza waandaaji na waliochanga!.

Kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kufanyika kwa jina la ‘Kagera day' na taarifa ni kwamba mamilioni yaliyochangwa wakati huo yakilenga kuboresha elimu mkaoni humo yalitafunwa na ‘wajanja' hadi kusababisha serikali ya mkoa kutoa ufafanuzi ‘mwepesi' juu ya kufunjwa kwa hizo fedha.

Soma hapa…
TOVUTI YA MKOA WA KAGERA ...............

Sasa juzi wadau wamerudia makosa yale yale (kwa maoni yangu) kufanya harambee kama hiyo eti wanalenga kutatua tatizo la madawati katika wilaya ya missenyi.

Nimekuwa kizunguka katika shule za msingi na sekondari wilyani humo wala sijui nani alifanya utafiti wa kubaini kwamba suruhisho la kuboresha elimu wilayani humo ni kuchangisha fedha ili wanunue madawati.

Soma hapa
DKT.BILAL AENDESHA ZOEZI LA HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU JIMBO LA NKENGE - Kagera Yetu

1.Je hizo fedha zitawafikia walengwa? Kwa njia gani
2.Nkenge Foundation ni mali ya nani? Imesajiliwa kwa jina la nani?
3.Nani msimamizi wa hizo fedha,ziko kwenye account ya nani?
4.Hizi hazitafunjwa kama zile za kagera day ?
5.Hakuna malengo ya kisiasa katika hizi harambee? Yasipotimia itakuwaje?

Ninaomba wenye michango ya kujenga kagera na taifa kwa ujumla tujadili kwa maslahi kuntu.


M.Byabato

Bukoba

cc. Phinias Bashaya Anna Tibaijuka
@Ta Muganyizi
 
Mzalendo Halisi said:
Kagera Day ni balaa

Uchangiaji fedha katika siku ya Kagera day ni vituko tupu. Kiasi cha
shilingi Bilioni 1.4 zilichangwa mbele ya Lowasa ikiwa nipamoja na zawadi.

1. Prof. Rweikiza wa Marekani- Sh. milioni 50

2. Prof.Rutashobya wa Chuo kikuu cha Havard-Milioni 40

3. Prof. Rweyimamu wa Afrika Kusini hakuweza kuja leo lakini ametuma
hundi ya USD 20000

4. Prof Rwabuyongo wa Ufaransa ametoa Sh. millioni 20

5. Prof. Rwebangira yeye amemtuma mkewe Kokushubira na yupo hapa na
Cash. Milioni 15000 amechelewa ndege ifwakti akitokea kutoa matibabu
Canada kwa mgonjwa anaye mhudumia huko.

6. Prof. Kokubenza ambaye nimewasiliana naye kwa simu na amedai kuwa
ameshikwa na mafua amesema hakuna tatizo tumtume mtu aende London
akachuklue Milioni 45.

7. Dk. Kagirwa huyu alikuwa Mzumbe miaka ya 90 lakini sasa yupo chuo
Kikuu cha Oxford amesema atatoa milioni 30.

8. Dk. Muganyizi ametoa milioni 20.

9. Dk. Mchunguzi ambaye sasa anamalizia Reseach yake ili aupate
Uprofesa amesema yeye na mkewe ambaye ametunukiwa PhD juzi hapo
mlimani pamoja na mtoto wao Rwechungura atatoa milioni 20.

10. Wengine wengi kama akina Katabazi, Kavodago, Kaceritale,
Kazenitalema, Katalyeba na akina Kokushuma wao wametoa kiasi kidogo na
wao wamekaa kule nyuma hata hatukuona haja ya kukupa mkono kwa kuwa
wametoa cash milioni kati ya 5 na 9. Pia mheshimiwa hawa nikuwa wana
Masters tu ndo hata tumeona elimu bado ndogo sio sawa na akina Rwegasira..

Hapa
https://www.jamiiforums.com/jokes-u...wahaya-bwana-kagera-day-balaa-tupu-print.html
 
Mkuu Byabato, Hizi ishu za kagera mtajuana nyie wahaya maana kila mtu much know, na hamchelewi kuleta posti za kihaya humu ndani. Infwakiti, sie tuko kwa ajili ya ishu za kitaifa na kimataifa. Huto tuvijisent kwa jimbo zima mbona tuchache mno kulingana na gharama na muda mliotumia? Nyie haya vp bwana?

elimu mkoani kagera na mikao ya kandaya ziwa inaporomoka kwa kasi ya ajabu.inahitajika mikakati
 
elimu mkoani kagera na mikao ya kandaya ziwa inaporomoka kwa kasi ya ajabu.inahitajika mikakati

mikakati si ndiyo hiyo inayoanzishwa kupitia harambee? issue hapa ni je hizo harambee zinazofanyika nje ya maeneo ya tatizo zina tija?
 
Ijapo haujataka kuniorodhesha kama mwana Kagera bado nahisi mawazo yangu yangesaidia kuliko kuzunguka peke yako na post huku ikikosa wachangiaji

Umeshajiuliza ni kwanini hata uliowataja hawajataka kuchangia post hii?
 
Ijapo haujataka kuniorodhesha kama mwana Kagera bado nahisi mawazo yangu yangesaidia kuliko kuzunguka peke yako na post huku ikikosa wachangiaji

Umeshajiuliza ni kwanini hata uliowataja hawajataka kuchangia post hii?

samahani sana! siyo lazima kuwakumbuka wadau wote ambao ni members wote humu JF .
Pia nimepokea mail zaidi ya 10 kutoka kwa wadau hasa walioko kwenye dola wakitoa maoni yao amabyo hawakuona umuhimu wa kupost humu Jf.Siyo kila post ipate wachangiaji wengi ili ionekane imeleta impact tarajiwa!

taarifa kuwafikia tu walengwa ni impact tosha mkuu.
Lakini mchango wako au kubadilika kwako juu ya namna ya kuboresha maendeleo ya kagera ni muhimu sana!

mbali na hapo nitakupigia no yako ninayo mkuu.

Niwe radhi Rweye
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la hizi ishu ni zile zile ambazo mie na wewe tumekuwa tukijadiri mpaka vichwa vinachemka,anyway hoja yako ina maana sana kyoma ila nakupa B nyingine kama siyo kichekesho

Mie nilivyosikia kupitia Clouds na TBC ishu ilionekana kuandaliwa na N.Foundation ikiwa ni ya mkoa wa Kagera wote lakini kumbe ilikuwa ya sehemu tu tena chini ya mtu na begi lake ..kyoma obu 'burushu'
 
Tatizo la hizi ishu ni zile zile ambazo mie na wewe tumekuwa tukijadiri mpaka vichwa vinachemka,anyway hoja yako ina maana sana kyoma ila nakupa B nyingine kama siyo kichekesho

Mie nilivyosikia kupitia Clouds na TBC ishu ilionekana kuandaliwa na N.Foundation ikiwa ni ya mkoa wa Kagera wote lakini kumbe ilikuwa ya sehemu tu tena chini ya mtu na begi lake ..kyoma obu 'burushu'

Alichosema mathabane hapa chini naona kinaanza kujitokeza mh Rweye

Mkuu Byabato, Hizi ishu za kagera mtajuana nyie wahaya maana kila mtu much know, na hamchelewi kuleta posti za kihaya humu ndani. Infwakiti, sie tuko kwa ajili ya ishu za kitaifa na kimataifa. Huto tuvijisent mlochangishana (m.14) kwa jimbo zima mbona tuchache mno kulingana na gharama na muda mliotumia? Nyie haya vp bwana?
 
Last edited by a moderator:
Mwendelezo wa hili,napata taarifa kuwa shule kadhaa za msingi katika wilaya ya missenyi zimefungwa kwa ukosa vyoo,je fedha hizi zilifanya kazi gani?
 
Back
Top Bottom