Wana Kagera Njooni Hapa Tutete, Tujadili, Tuzungumze, Tufanye Maamuzi, na Tuchuke Hatua!

Hii hali inasikitisha mno lazima tutafute muarobaini wa kuiondoa CCM Kagera. Kama Jimbo langu la Nkenge mpaka leo siamini huyu mwanamama alipitapita vipi? Wapiganaji tuamke ukombozi unaanza na sisi. Wasomi tumelala
Halafu kakatutukana kwamba tusiokunywa chai asubuhi ni sababu ya uvivu wetu na si umaskini.
 
Ndugu,

bakuza, Bigaraone, Chaimaharage, evoddy, Gagnija, Hagga, Jaji, james chapacha, Kagalala, Kaitampunu, kanyagio, Kibera, Lonestriker, Mkomamanga, MPIGA ZEZE, MUGUNDA, naivasha, Ngeleshi, PrN-kazi, Qixima mQiqa, RUBERTS, Rwamarungu, Rweza, sangija, Seneta,mukama talemwa,Speedy, timbilimu, Tukundane, Yakuza, Tata, KASHOROBANA na wengine nyote mnaoipendea mema na maendeleo Kagera

Hapo chini ni mabadiliko yanayoendelea kutokea nchini. Yameninyong'onyesha na kunifedhehesha sana nilipojaribu kulinganisha Shinyanga na Kagera.

Nawaomba mje hapa tufanye mjadala mpana utakaoishia katika maamuzi na kuchukuliwa hatua kivitendo juu ya nini kifanyike toka sasa mpaka 2015 ili nasi walau tuweze kuwemo kwenye basi la Mabadiliko na Ukombozi wa Tanganyika
Mukulu waitu wakola sasa hii ndio kianzio, kwanza Kagera tuna strategy starting points nyingi; tumefanyiwa umafia siku nyingi na hiki chama cha Magambas; waliua ushirika wetu fedha zikitumika kwa kazi za chama (eti chama kushika hatamu) wakafilisi vyama vyetu!!!! Kahawa sasa hivi haina bei and we don't have access to outside markets with out intervention from these dictators!!! Migomba yote inakufa serikali kwanza ndio inachekelea maana wanasema tuwaone sasa watafanyaje mshomile!!!! Sijui sasa tufanyeje kuweza kujikomboa, ni bora tugeukie CHADEMA kuliko huyu muuaji wetu CCM!!!

Kweli maneno yako huyu jamaa Phocas alifanya ESAKILILIGO hapashwi kusamehewa hata mbinguni, wananchi walimuamini akapewa pesa akasepa ni mtu wa ajabu sana.
Wananchi ni muda wao kujiandaa muda bado upo wa kutosha, nimshukuru mletaji wa mada maana kama Shinyanga wameweza wengine tutashindwa vipi? Mimi Naenda kuanzia kwetu Bugabo wananchi wajue kuwa samaki wetu wanapelekwa EU wakati hakuna tunachopata, mikataba ya Karl Peters.
MWAMI WAKOLA KULEETA EKIGAMNO EKI TWEECHONCHE.
Sawa Mjomba ogendege okwate mashaija onkeisheze aba Kibengwe, Kayungwe na Bishaka!!!!

Nina mfano mdogo wa kusaidia kukoleza hasira zetu. Sisi tuna zaidi ya kilometa za mraba kama 7000 kuzunguka mipaka ya nchi mbalimbali Afrika. Hakuna mkoa mwingine Tanzania wenye eneo kubwa la mipaka kuliko Kagera. Na kwa upande wa Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, Kagera ndo imezungukwa na ina ukaribu na nchi hizi zote. Lakini pamoja na kujipendekeza kwa ccm wakati G. Lema na CDM wakitetea haki za wana Arusha kwa mtindo ambao ccm walidai unahatarisha amani ya Geneva ya Afrika, hakuna hata Kiongozi mmoja awe mzaliwa wa Kagera au yeyote awaye amewahi kufikiri kuwa na walau ofisi ndogo ya Umoja wa Afrika Mashariki mkoani Kagera.

Sasa kama Arusha, Moshi, Mwanza, Karatu, Shinyanga, wanaweza kupigania maendeleo pasipo kujikomba kwa ccm na wakayapata kwa mwendo wa roketi nje ya ccm, kwa nini nasi tusiasi na kujiunga na wanaojitafutia maendeleo bila upendeleo unaodumaza fikra, uchumi, elimu na kudhaulisha utu wetu?
 
Mabadiliko yote chanya huanza na wasomi. Hawa ndio wanaopaswa kutuonyesha tunataka kwenda wapi. Sasa tunao wasomi katika nyanja mbalimbali. Hawa wanapaswa washikane mkono ili tukaweze kwenda mbele. RAI yangu ni kwa walioko SOKOINE University of Agriculture (SUA). Waangalie issue ya ugonjwa ulioshambulia migomba na kuifanya inyauke. Hawa waje mpaka mashambani wafanye utafiti on grounds ili tupate kujua tatizo ni nini? Maana Kagera imwkuwa kichwa cha mwenda wazimu. Tuliletwa species za migomba mara "mtumwishe na majina mengine ya ajabu. Wakulimwa wakaacha zao la asili wakaanza hii specie ya kigeni that is not friendly by all aspects maana it creates a canopy of which underneath nothing can grow wakati kwa asili maharage upandwa ndani ya migomba. Sasa ili zao linalotengeza mwavuli kaisi mvua na mwanga havipenyi je linafaa. Lakini zaidi hayo migomba ya asili ilianza kutoweka kama aina za samaki ndani ya ziwa Victoria. Baada wakaja wajanja wachache wakaleta pine trees and capitalised on economic decadence and ignorance of th great majority. Na hii miti ilipndwa karibu na mashamba ya migomba, mingine mashmbani nayo ina matatizo yake. Cha msingi ni kwamba huwezi kuwabadilisha watu walio na matumbo ya njaa na mifuko iliyotoboka. Hii inatakiwa pamoja na mengine iingie kwenye frameworks. Wataalamu wa research mko wapi tuwekee conceptual framework
 
Ndugu zangu Mtumishi Wetu,Rweyemam,Gagnija, Babuyao, mtufulani, Blandes, Kaitampunu, Kyaka, Davie, cham, Muadilifu, Babuyao, mtufulani, Blandes, Kaitampunu nawaona, acheni kuchungulia. Leteni mipango. Tufanyeje? Twagoshoka aboomwaitu....ensi ngigyo yagella n'engoma n'etwalwa tuleebile?! Engoma eshuba mbali elagile, ichwe ntugitaishura!
Nomanya ichwe ekyatuisile ichwe ABAHAYA KWEKOLA TULIBAMANYI, taliyo alikwenda katukola bumoi, tugila amagayangane; ogu ati inye ndi Muhamba, ondijo ati ndi Muziba ,ogu Muhangaza, Munyambo etc, etc!! Sasa Omutwale nolenga tulakola tutai, abantu chwena aba Bahaya tukaba bamoi???? Olwokuba enaku nizitutela chwena, iwe kolaba oshomile well and good chyonkai barumuna bangi tibashomile nkaiwe!!! Please we should have a united strategy to come together and evaluate our Kagera Region future destiny!! Wakola Mutwale nindenga talio balagaya ebi ebyo watandika!!! Mungu Rugaba akue emigisha!!!

Asante sana kwa kutuwekea mada mahsusi kwa ustawi wa mkoa wetu pendwa-Kagera. Naomba nichangie hapa:
......RAI yangu ni kwa walioko SOKOINE University of Agriculture (SUA). Waangalie issue ya ugonjwa ulioshambulia migomba na kuifanya inyauke. .... Wataalamu wa research mko wapi tuwekee conceptual framework
Kuna tatifi mbalimbali zilikwisha fanyika kuhusiana na tatizo hili. Fuatilia hapa: Reduced cost of tissue culture banana can help control spread of Banana Bacterial Wilt in Great Lakes region na Farmer Capacity Building in Tissue Culture Banana Cultivation labda walakini uko katika uwezo wa mtu wa Morogoro kumfundisha mzaliwa wa Dar es Salaam kuogelea Baharini!
 
Nina mfano mdogo wa kusaidia kukoleza hasira zetu. Sisi tuna zaidi ya kilometa za mraba kama 7000 kuzunguka mipaka ya nchi mbalimbali Afrika. Hakuna mkoa mwingine Tanzania wenye eneo kubwa la mipaka kuliko Kagera. Na kwa upande wa Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, Kagera ndo imezungukwa na ina ukaribu na nchi hizi zote. Lakini pamoja na kujipendekeza kwa ccm wakati G. Lema na CDM wakitetea haki za wana Arusha kwa mtindo ambao ccm walidai unahatarisha amani ya Geneva ya Afrika, hakuna hata Kiongozi mmoja awe mzaliwa wa Kagera au yeyote awaye amewahi kufikiri kuwa na walau ofisi ndogo ya Umoja wa Afrika Mashariki mkoani Kagera.

Sasa kama Arusha, Moshi, Mwanza, Karatu, Shinyanga, wanaweza kupigania maendeleo pasipo kujikomba kwa ccm na wakayapata kwa mwendo wa roketi nje ya ccm, kwa nini nasi tusiasi na kujiunga na wanaojitafutia maendeleo bila upendeleo unaodumaza fikra, uchumi, elimu na kudhaulisha utu wetu?
Enaku zaitu niziletwa okwekola tuina akalyo, tunajipendekeza kwenye serikali na ruling party huku tukiendelea kwenye mkoa wetu kukandamizwa, umasikini mkoani hadi puani, lazima tubadilike kupata ukombozi!!!!

Mabadiliko yote chanya huanza na wasomi. Hawa ndio wanaopaswa kutuonyesha tunataka kwenda wapi. Sasa tunao wasomi katika nyanja mbalimbali. Hawa wanapaswa washikane mkono ili tukaweze kwenda mbele. RAI yangu ni kwa walioko SOKOINE University of Agriculture (SUA). Waangalie issue ya ugonjwa ulioshambulia migomba na kuifanya inyauke. Hawa waje mpaka mashambani wafanye utafiti on grounds ili tupate kujua tatizo ni nini? Maana Kagera imwkuwa kichwa cha mwenda wazimu. Tuliletwa species za migomba mara "mtumwishe na majina mengine ya ajabu. Wakulimwa wakaacha zao la asili wakaanza hii specie ya kigeni that is not friendly by all aspects maana it creates a canopy of which underneath nothing can grow wakati kwa asili maharage upandwa ndani ya migomba. Sasa ili zao linalotengeza mwavuli kaisi mvua na mwanga havipenyi je linafaa. Lakini zaidi hayo migomba ya asili ilianza kutoweka kama aina za samaki ndani ya ziwa Victoria. Baada wakaja wajanja wachache wakaleta pine trees and capitalised on economic decadence and ignorance of th great majority. Na hii miti ilipndwa karibu na mashamba ya migomba, mingine mashmbani nayo ina matatizo yake. Cha msingi ni kwamba huwezi kuwabadilisha watu walio na matumbo ya njaa na mifuko iliyotoboka. Hii inatakiwa pamoja na mengine iingie kwenye frameworks. Wataalamu wa research mko wapi tuwekee conceptual framework
mkuu nakuunga mkono uwepo wa migomba kagera upo kwenye hatihati wakati tunafanya mapinduzi ya kisiasa na maendeleo twende nayo sambamba, Omukama Mungu atuhabukile
 
Nani anaweza kunitegulia sababu inayofumbua mafumbo haya:

Mkoa wa Kegera
Mkoa wa Kilimanjaro
Tunalima migomba
Wanalima migomba
Migomba yetu iko mahututi
Migomba yao ina uhai

Tunalima kahawa
Wanalima kahawa
Bei anayopewa mkulima wa kahawa Kagera imemkatisha tama mpaka ameamua kung'oa mibuni
Bei ya mkulima wa Kilimanjaro imemhasisha kuongeza idadi ya mibuni mipya kila mara
Kahawa ya Kagera imeathiriwa na bei katika "soko la dunia"
Kahawa ya Kilimanjaro imeshamiri kwa bei za mnada wa Moshi

Hawa Wahaya wanajadili M4C au ni yale ya UAMSHO? Naona mchanganyiko wa lugha hapa, MODs naomba hii ipelekwe Chitchat.
 
qualification za kuwa mwana kagera ni zipi?
si kuishi huko tu, au?
njuna wejune embwa yagenda ne ekirumiko!

Ni hayo tu yenye rangi hapo kwenye maandishi yako ndiyo yamenifanya kuuliza kama nawe ni mwana-Kagera?

......KUSHUKA KWA UCHUMI KATIKA ENEO HILO (mnawazidi DODOMA na SINGIDA TU) .Mimi ...... haikubali (awali mlizoea kutifua udongo kidogo tu na kuisimika aridhini, JEMBE HAMJUI KUSHIKA, MNANYOFOA MAGUGU SHAMBANI MKIWA MMEKAA,KUSOGEA HATUA NYINGINE MNAJIVUTA). .... jifunzeni kukamata jembe au mnasubiri matrekta ya kilimo kwanza? ... mnasubiria msimu tu... watu wavivu mkashindwa.
....anaona uvivu. mnapenda sana kula bata ndugu.hampendi kazi ngumu.komaeni, pigeni kazi, .... kiasi kwamba hadi mambo yenu yaleeeeee ya SHULE yanawashinda siku hizi.

Nafikiri sikuwa peke yangu maana hata alberaps naye ameonyesha kushangaa!
Mkuu mbona kama ulikuwa umewapania wenzako? Ndo hasira gani sasa hizo?

Alexism
+ habari za siku nyingi, Nkindo hawajambo? Karibu kwenye mada
 
Wazo zuri sana mno:
'''Kagera katuta-gi-mukile ya-kuliba'''

ingependeza kabla ya yote tukakutana wana-Kagera wote tukaweka mpango mkakati wa jinsi ya kuukomboa mkoa wetu: tutumie JF kama njia ya kupitishia taarifa lkn kukutana ni muhimu kwani SAA YA UKOMBOZI NI SASA.
 
Waitu Shumalamu.
Week kama mbili zilizopita niliweza kwenda kijijini kwetu sehemu za Bugabo kulikuwa na harusi ya mtoto wa kaka yangu. Baada ya kuwanunulia wana kijiji chupa mbili tatu za kapombe ketu nikaingiza mjadala wa siasa nikasema wanaotaka mabadiliko katika nchi hii ni wangapi. Mzee mmoja alinipa jibu ambalo lilikuwa la kufurahisha. Alisema yeye ni mwanachama wa CCM tangu TANU lakini anataka vijana walete mabadiliko kwani haoni tena faida ya CCM.
Vijana nao wakasema wao wakipewa sukari kilo moja inatosha na CCM ndo huwa wanafanya hivyo. Basi nikajua umasikini wetu ndo mtaji mkubwa wa CCM.
 
Magufuri kahamisha barabara kuu, toka biharamulo kapitishia jimbon kwake chato. Kajiwekea lami huku barabara kongwe ya kutoka njia panda- biharamulo- mpaka muleba haina lami. Kweli hii ni haki, au ndio matumizi mabaya cheo? Tu amke jaman!
CPA(T) - Kutoka KAMACHUMU (kagera kwetu)
 
Hili linatatulika hivi: Kila wilaya mkoani Kagera inalo jambo ambalo ikilichagua na kulitekeleza, itakuwa na nafasi kubwa ya kiushindani (competitive advantage). Mfano Muleba kuna maeneo yenye ardhi nzuri na vijito vya maji visivyokauka. Wanaweza kuamua kuanzisha Kilimo cha Mpunga, mboga mboga na matunda kwa ajili ya kulisha mkoa mzima.

  • Missenye ni lango la bidhaa zitokazo na ziendazo Somali, Uganda, Kenya, na Sudan. Hii wilaya inaweza kufanywa soko la mpakani lenye maghala makubwa ya nafaka na viwanda vya usindikaji wa chakula.

  • Ukiachilia uzuri wa ardhi, Karagwe inao wafugaji wengi wenye mifugo mizuri. Hii inawawezesha kujikita katika kusindika nyama na mazao ya mifugo (maziwa, jibini, ngozi, n.k)

  • Maeneo ya pembezoni mwa Bukoba mjini kuzunguka Green Belt na sehemu za Bukoba vijijini kwenye mialo kama Bugabo, Kemondo, na Kabuara yanaweza kufanyiwa mpango maalumu yawe maeneo ya recreational and hosptality services

  • Bukoba vijijini itengwe maalumu kwa ajili ya masuala ya Elimu. Hapa namaanisha elimu ya juu na stadi za maisha (vocational trainings). Maana tunahitaji shule za msingi na sekondari katika kila kata kwenye wilaya lakini hatujafikia Uwezo wa kuwa na vyuo vikuu au vyuo vya ufundi mahiri vilivyosheheni kama DIT, Arusha Tech, Mbeya Tech, n.k kila wilaya

  • Gold belt inayopita kanda ya ziwa inaiweka B'mulo kwenye nafasi nzuri ya uchimbaji wa madini. Ukitupia kando dhahabu, Kagera kuna gemstone reserve kubwa na hazijaguswa hata kidogo. B'mulo inaweza kuamua kati ya kuchimba madini au kujidhatiti katika kilimo cha alizeti na pamba, usindikaji wa mafuta ya kula na vyakula vya mifugo. Katika yote haya B'mulo inaweza kufanya vema. Na miaka ya nyuma iliwahi kufanya vema katika hili la mwisho.

  • Eneo la Nyakahura, Mulusagamba, Kabanga mpaka Ngara kwa ujumla linaweza kuandaliwa kuwa bandari ya nchi kavu kwa mizigo iendayo Rwanda, Burundi, na DRC-Congo.
Ni kwa kugawana maeneo ya kufanyika kazi kulingana na faida za kiushindani ndo tunaweza kusonga mbele. Ama sivyo hatutakomesha misuguano ya sisi kwa sisi inayoibuka kutokana na mashindano miongoni mwetu.

Back
Top Bottom