Wana Kagera Njooni Hapa Tutete, Tujadili, Tuzungumze, Tufanye Maamuzi, na Tuchuke Hatua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana Kagera Njooni Hapa Tutete, Tujadili, Tuzungumze, Tufanye Maamuzi, na Tuchuke Hatua!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omutwale, Jun 25, 2012.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndugu,

  bakuza, Bigaraone, Chaimaharage, evoddy, Gagnija, Hagga, Jaji, james chapacha, Kagalala, Kaitampunu, kanyagio, Kibera, Lonestriker, Mkomamanga, MPIGA ZEZE, MUGUNDA, naivasha, Ngeleshi, PrN-kazi, Qixima mQiqa, RUBERTS, Rwamarungu, Rweza, sangija, Seneta,mukama talemwa,Speedy, timbilimu, Tukundane, Yakuza,rugumisa,GALIMA,BigTime,Kakalende,PrN-kazi, Alexism+, kilikiliani,kanyagio,BUSHAIJABWE, Libaba, Smarty, Baba Collins,Eddy M, BUBE, Tata, KASHOROBANA na wengine nyote mnaoipendea mema na maendeleo Kagera

  Hapo chini ni mabadiliko yanayoendelea kutokea nchini. Yameninyong'onyesha na kunifedhehesha sana nilipojaribu kulinganisha Shinyanga na Kagera.

  Nawaomba mje hapa tufanye mjadala mpana utakaoishia katika maamuzi na kuchukuliwa hatua kivitendo juu ya nini kifanyike toka sasa mpaka 2015 ili nasi walau tuweze kuwemo kwenye basi la Mabadiliko na Ukombozi wa Tanganyika   
 2. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Itakuwa ni vyema kama ungekuja na conceptual framework that will serve as a pedestal upon which contrubutors in the genesis of renaiscance will stand tall. Na hili liwekwe kwa umakini mkubwa maana wana Kagera ni sehemu ya Tanzania lakini wana bahati moja nzuri au mbaya kwa kuwekwa kapu pale wanapotenda yale ambayo kwa macho ya wengine wanaona kuwa ni mabaya. Sisemi hawafanyi au hawakuwahi kufanya mabaya maana wanakagera kama walivyo watu wengine ni binadamu lazima walifanya, wanafanya na wataendelea kufanya mema na mabaya. Bahati mbaya kuna value judgement na sterio type hapa Tanzania. Kama mwanakagera mmoja au wawili au namba yoyote ile ilifanya kitu kibaya wanakagera wote walionekana ni sehemu ya makosa hayo. Si siri kila ukipita utasikia sifa ya wanafiki, wabaguzi, wakabila na mengine mengi. Hii value judgement imewagawa wanakagera na hii sio siri. Kukiwa na mjadala mzuri wa wanakagera wamesoma, wana akili, ni warembo aha jinsia ya kike na nyinginezo- wale wanaotoka Biaharamulo, Ngara, Karagwe, Muleba, Bukoba mjini, vijijini na leo Misenyi watapenda watambuliwe kuwa Wahaya. Lakini ikija mjadala wa yale mabaya kama yalivyotajwa hapo juu hapo utaona watu watakavyoruka kimanga. Utasikia mimi ni mnyambo original, mimi mganda kyaka, mimi msubi, mimi mhangaza, mimi Munyihagoro, mimi mziba, mimi muhamba na mengine mengi ali mradi kila mtu anataka asiwe sehemu ya sifa mbaya. Nimeandika haya kwa kifupi ili nitoe changamoto ambazo kwazo wakati tunajadili tuwe na framework ya kutuongoza ili tuwe na mjadala mpana utakaounganisha diversity zote on dialectical and rational basis.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Bigaraone,

  Umetufungulia jamvi la mjadala wetu. Naamini ushauri ulioutoa kuna wataalamu watakuja kutusaidia kuweka hizo nyenzo (Frameworks).

  Lwona baliyo....tubalinde...mbaija!
   
 4. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ndio nyie mlioweka usomi wenu mifukoni kwa kuwachagua magamba sasa ni wakati mwafaka kubadili akili zenu na usomi wenu uwe na manufaa kwa taifa kama walivyofanya arusha,moshi na mbeya,nyie washamba ilikuaje mkamruhusu TABAIJUKA apite bila kupingwa?oneni aibu sasa wasomi wajabu nyie,mumekalia sifa na majigambo tu,TOKENI KWENYE UKUNGU!
   
 5. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Watu wa Kagera wanajifanya wana harakati wakiwa mikoa ya wenzao,wakirudi kwao wanachagua magamba.
   
 6. B

  Bunsen Burner Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Watu wenyewe hao' nshomil'e ndo utakuta mahakinu , majaji, makamishna wa polisi mikoani n.k. serikalini wao wanatumiwa tu lakini ukifika pale mji wao mkuu Bukoba' pako hoi taabani huwezi amini,ujanja wa bure !
   
 7. Blandes

  Blandes JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Chadema walituangusha kutosimamia na kuangalia mtu ambae anagombea ubunge anamtazamo gani,wakachukua dj wakamsimamisha agombee ubunge uko nkenge mwisho wa kampeni akaondoa jina akamuachia nafasi Mushamu atambe nkenge peke yake,ila yote ii ni kwasababu tulimpoteza mtu ambae alikuwa mpiganaji Julius Ndyanabo Mungu amuweke pema,viongozi wa chadema geukia uko ISHOZI,ISHUNJU,GERA,BWANJA,KANYIGO,BUYANGO,BUGANDIKA,KYAKA,BUNAZI,KAKUNYU,MUTUKULA,NK
   
 8. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli maneno yako huyu jamaa Phocas alifanya ESAKILILIGO hapashwi kusamehewa hata mbinguni, wananchi walimuamini akapewa pesa akasepa ni mtu wa ajabu sana.
  Wananchi ni muda wao kujiandaa muda bado upo wa kutosha, nimshukuru mletaji wa mada maana kama Shinyanga wameweza wengine tutashindwa vipi? Mimi Naenda kuanzia kwetu Bugabo wananchi wajue kuwa samaki wetu wanapelekwa EU wakati hakuna tunachopata, mikataba ya Karl Peters.
  MWAMI WAKOLA KULEETA EKIGAMNO EKI TWEECHONCHE.
   
 9. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Tunaweza kubadili hali iwapo kila mmoja atafanya maamuzi na kuchukua hatua stahili kuibadili jamii ili itumie vema uwezo wake kimaamuzi kuleta mabadiliko chanya.

  Haya ndo maamuzi tunayoyahitaji. Lakini kuna umuhimu wa kuwa na mkakati wa pamoja. Nafikiria kufungua group-email ili watakao onyesha nia thabiti tuanze mikakati

  Inye ninsima iwe n'ondijo alakwatwa ekiniga kya amani, akagya kugambila abawenene naabamwataine kabainduka.
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
 11. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280

  Hee! Kweli Mmecharuka! Huu mstari wa mwisho sijaambulia hata neno moja. Haya Move On Msikate tamaa wala kuchoka!
   
 12. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
 13. m

  mtufulani Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .

  WATU WENYE NJAA SIO RAHISI KUCHAGUA UPINZANI, WATADAGANYIKA KIRAHISI KWA WALI NA KOFIA. TATIZO LILILO LA MSINGI NI UCHUMI WA KAGERA ULIODUMAA.

  KUNAWEZA KUWAPO SBB NYINGI ZA KUENDELEA KUSHUKA KWA UCHUMI KATIKA ENEO HILO (mnawazidi DODOMA na SINGIDA TU) .Mimi naona Uvivu uliokithiri na kutojituma ndio sababu kubwa.Hakuna chakula,migomba haikubali (awali mlizoea kutifua udongo kidogo tu na kuisimika aridhini, JEMBE HAMJUI KUSHIKA, MNANYOFOA MAGUGU SHAMBANI MKIWA MMEKAA,KUSOGEA HATUA NYINGINE MNAJIVUTA).

  Wakati wa kulima mahindi na mtama kama zao la chakula umefika. jifunzeni kukamata jembe au mnasubiri matrekta ya kilimo kwanza? Kahawa haina soko tena( mikahawa yenyewe ilikuwa kama miti ya miembe,haifanyiwi chochote mnasubiria msimu tu.Na hakukuwa na jitihada ya kupanda mipya) samaki wanapelekwa nje tu.Kuna wakati nilisikia vanila inakubali sana huko, ila kwa kuwa inahitaji sana matunzo watu wavivu mkashindwa.

  Mtu mvivu sio rahisi kupenda au kukubali mabadiliko na hatimaye akawa na mawazo ya kukabili changamoto mpya kama kuhama au kuchagua chama kingine cha siasa, anaona uvivu. mnapenda sana kula bata ndugu.hampendi kazi ngumu.komaeni,pigeni kazi, enzi za ulangila kwishinei.Wavivu kiasi kwamba hadi mambo yenu yaleeeeee ya SHULE yanawashinda siku hizi.
   
 14. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona kama ulikuwa umewapania wenzako? Ndo hasira gani sasa hizo?
   
 15. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  mtufulani
  Asante kwa ghani zako. Na wewe ni Mwanakagera?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakuu mimi nipo jimboni naanza taraaaaaaaatiiiiiiiiiiiiiiiibu hadi kieleweke.
   
 17. K

  Kyaka New Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hii hali inasikitisha mno lazima tutafute muarobaini wa kuiondoa CCM Kagera. Kama Jimbo langu la Nkenge mpaka leo siamini huyu mwanamama alipitapita vipi? Wapiganaji tuamke ukombozi unaanza na sisi. Wasomi tumelala
   
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Waitu tukwate amashaija,omuhaya ati oshenya na alakutweka.
   
 19. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Asalaaa leh! Naona mnazidi kututenga! haya wacha nifunue kamusi yangu ya swahili--> haya dikshonari
   
 20. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  BUBE, Bishanga, na Kyaka nitatengeneza group-email ili tweme amoi kutelanganila Kagera yaitu.

  Omuli-eki ccm mbatutweka amabale ti nkwi zo tushenyile!
   
Loading...