Wana JF yamenikuta ya huyu binti mwenye mtoto, tafadhali naombeni ushauri

Aaaah shit.
Yan dada,kaka na baba wanakupigia simu kuhusu mahusiano ya mtoto wao wa kike ambaye hata hujamuoa?RUBBISH kabsa iyo familia

Simple and clear wampigie yule jamaa alizaaa naye.
 
Kama kweli umedhamiria kuachana nae badili namba yako na uhame unapoishi kama anapajua. Na ofcn kwako toa taarifa kwamba akifika aambiwe haupo au umehamishwa kikazi. Simpo
 
Wameona we ndo kiazi, kwanini wasimpigie aliemzalisha..
Miaka 20....club amenza kwenda akiwa na umri gani? Si ajabu hata huyo baba anakomaa maana anataka umsaidie kulipuka na hilo bomu, yeye mwenyewe analikwepa.
 
Broo siwezi kukulaumu kwasababu hayajakukuta, Kiukweli hii kitu inakua Automatically na hata mimi siamini kama namganda yule mwanamke.... Broo hizi ishu za kupenda kaka zisikie tu kwa watu, ila usiombe zikukute... Yaani utajikuta unaona kahaba kabisa, na unajua kabisa huyu mtu ni kahaba wa kujiuza lakini hilo utaliona lakawaida sana... Broo, usicheke kama bado kijana,.. Na usiombe ukapenda kaka

Nilishaambiwa na kuaswa kukaa mbali na wanawake walio zalishwa na NIKASIKIA. Haiwezekani kamwe kuja kuingia kwenye mahusiano na mwanamke aliyezalishwa na mwanaume mwingine.

Ujinga kama huu wa mleta mada hauwezi kuja nitokea.
 
Nilishaambiwa na kuaswa kukaa mbali na wanawake walio zalishwa na NIKASIKIA. Haiwezekani kamwe kuja kuingia kwenye mahusiano na mwanamke aliyezalishwa na mwanaume mwingine.

Ujinga kama huu wa mleta mada hauwezi kuja nitokea.
Doooooohhhhhh, broo usiseme hivyo ingali bado kijana, labda kama umri wako umeenda.... Kuna wengine wanaingia huko hawajui, na mwanamke hasemi kwasababu masingo maza sasa hivi wamejua wakisema kua wana mtoto.. Hawataolewa... Broo futa kauli yako,.. Utakutana na pisi kali ukidhani ni hajawahi kuzaa kumbe ana watoto wawili... Broo tengua kauli kaka, wanawake sio watu
 
Achana nae atakuua mapema, Kama una huruma sana mfungulie biashara au mtafutie kazi aendeshe maisha take pasi na kuwa na mahusiano nae!
 
Wadau habari, poleni na majukumu.
Kilichonileta apa leo ni kuomba ushauri je nifanye nini juu ya hili,

Niliingia kwenye mahusiano na mwanamke mmoja ambaye alizalishwa na jamaa uko tunduma, mwanzo sikuwa naiona athari yoyote ya kuwa na mwanamke ambaye alizaa nikiamini kwamba sio wanawake wote waliozaa ni shida hasa likija suala la baby dady dramer, lililonipa nguvu zaidi ni pale baada ya mwanamke kunambia yeye alizalizaa tu na huyu mwanaume na hawezi kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi na baba mtoto zaidi ya kumlea mtoto na ukizingatia uyu bwana ni mume wa mtu wa ndoa uko alipo na nilihakikisha hili.

Nimeishi pamoja na uyu mwanamke mwaka sasa, japo tangu mwanzo kulishatokea vitimbwi vingi sana mara kwa mara na nilivivumilia, ni mwanamke flani hivi ambaye alishapitia ujana mwingi sana, ninavyosema ujana namaanisha alishakuwa mwanamke wa kujirusha sana uko ma night club na kadhalika.

Mimi ni kijana mwenye kazi yangu nzuri tu, na kwa kipato changu nna uwezo wa kumtimizia kila hitaji atakalo uyu mwanamke na sio yeye tu hadi uyu mtoto wake ambaye c wangu, namlea mtoto wa mwanaume mwenzangu bila kinyongo ' msinilaumu kwa hili ni kwa upendo tu '.

Sasa shida iliyopo ni hivi,, kila nikizinguana na uyu mwanamke ata liwe jambo dogo tu na hata kama alinikosea yeye then kiume tu nika react kuonyesha kutopendezewa na hilo jambo alilofanya, basi siku hiyo baba mtoto atatafutwa kwa speed zotee, ataitwa dady nikutumie picha za mwanao umwone, dady tutumie pesa za matumizi tumeishiwa, dady iv dady vile..

Hali hii hutokea mara kwa mara kwa huyu binti, kuna nyakati nilichoshwa na huu mtindo wake 'inakera' na nilimuuliza so why kila tukiwa hatupo sawa unamtafuta uyu mtu alinijibu kuwa ata yeye haelewi ni nini huwa kinampata kufanya hivi, lakini ilijirudia hivyo zaidi ya mara 3 hata baada ya kumuuliza tayari na kunijibu kuwa ata yeye haelewi lakini siku zingine alirudia kufanya hivyo.

Ikafika wakati nilichoka, nikamwambia tu kuwa siwezi tena kuwa pamoja nae kwa sababu alimweka baba mtoto kama tishio kwangu, tuliachana kwa ghadhabu sana na kila maneno ya kumkatisha tamaa niliyanena kwake, lakini hakutaka kukubaliana na hili, nilimblock kila kona ya mawasiliano baina yetu, lakini alionyesha kujutia hili na kuni ahidi kuwa awezi rudia tena kufanya hivyo, wakati huo alinifuata adi ofisini bila uwoga wowote alianza kulia na kutia huruma, wafanya kazi wenzangu waliliona hilo na kunishauri kuwa nimpe tu chance nyingine. Basi kwa sababu tumeumbiwa huruma nilimhurumia na kurudiana nae.

Mwanamke ni mzuri tena bado ni mdogo tu, ajachakaa kiivo, nimemzidi karibu miaka 10

Sasa juzi kati tena apa umetokea ugomvi kati yetu mkubwa tu, alicharuka tu ghafla akinambia kuwa anahitaji niende nyumbani kwao nikaonekane ili nimchukue official kwenda kuishi nae, mimi nilimjibu kwamba asubiri asiwe na haraka, basi kujibu kuwa asiwe na haraka ikawa kosa, usiku huo baba mtoto katafutwa, dady mambo, jamaa kajibu poa, dady mimi nimechoka kukaa apa nataka kuondoka kama vipi tuje uko ulipo nitafutie mishe ya kufanya uko mimi apa nimechoka kuishi, au basi nipe pesa ya mtaji nianze biashara uko mbali na apa ' Aisee iliniuma sana na kujiuliza kapata wapi huu ujasiri tena wa kumweleza haya yote uyu bwana '

Mimi ni Afisa Katika Kampuni flani ya mawasilino, hivyo nimetrack simu yake huyu binti kila afanyalo katika simu yake naona, ule usiku alimtafuta sana jamaa ad kujaribu mara nyingi kumpigia lakini jamaa hakupokea simu, zaidi jamaa alimwandikia sms kuwa mbona unanieleza haya yote na hali nimesikia yupo mwanaume uko anayekutunza kwa kila kitu na matumizi anatoa, lakini akajibu kwa kushangaa kuwa hakuna mwanaume yeyote anayefanya chochote juu yake 'alinikana kwa jamaa ' , alinipigia simu nikapokea, nikamuuliza umefanya nini, akanijibu kuwa ajafanya kitu, nikamuuliza umewasiliana na nani na hayo yote uliyomweleza, akanijibu kuwa yeye amechoka kwa sababu nimegoma kujionyesha nyumbani kwao ili tukaishi pamoja, nikamjibu sawa kwaheri.

Nikamblock then program nayoitumia kumtrack nikai remote ifute kila kitu kwenye simu yake, na kweli cm ikawa formated, nilifanya hvo ili asiwe na kumbukumbu zangu zozote kwenye simu yake, ili iwe rahisi kwake kunisahau.

Alinitafuta kwa namba nyingine na kunambia hayupo tayari nitoke kwake kwa sababu bado ananipenda na kunambia kwamba pia sitoweza kutoka kwenye maisha yake, kauli hii ilinitisha kidogo, nikamjibu sawa ila hesabu kwamba mimi sitoweza kurudi tena kwako, TUMEACHANA. Aliwaambia dada zake wakaanza kunitafuta wakinisihi nisimwache mdogo wao bado ananihitaji kwa hasira nao niliwablock, kaka zake pia walianza izo habari nao pia nikawablock, wote nikawajibu kuwa sitoweza rudi kwa mdogo wao. Kama kawaida mwanamke anaonyesha tena hali ya kujuta mno, anaomba msamaha adi kero sasa, kila namba atakayoitumia kunitafuta sikujibu lolote zaidi niliiblock.

Kiukweli nimechoka na haya mapichapicha ninajuta tena kuingia kwenye mahusiano na huyu binti mwenye mtoto, dramer ni nyingi hasa za uyu baba mtoto pindi tukigombana, ni mjeuri, kuna wakati anayamiss yale maisha ya club japo nilimkataza akuna kwenda club na hakwenda, kuna tabia nyingi sana nilimbadilisha na tukaenda sawa, ata kuanza kuhudhuria nyumba za ibada.


SHIDA NI KWAMBA BABA YAKE MZAZI KANIPIGIA SIMU LEO, SIJAWAHI ONGEA NAE HUYU MZEE ZAIDI UWA NAMWONAGA TU KWA MBALI, ALIJITAMBULISHA LAKINI NIKAWA NIMESHAIFAHAMU SAUTI YAKE, MZEE ANANAMBIA BINTI YAO HAWAMWELEWI NI MNYONGE MNO, KULA HALI HAKUNA LOLOTE ANALOWEZA KUFANYA, WALIVYOJARIBU KUMBANA AMENITAJA MIMI NDO CHANZO, BABA ANANIOMBA NIYAMALIZE NA BINTI YAKE NA KWAMBA BINTI ANAONYESHA KUJUTIA SANA, MZEE ANANIOMBA MSAMAHA MIMI TENA!!! NA KUSEMA ANAFAHAMU KUWA YEYE AKUTAKIWA KUINGILIA LOLOTE KATIKA JAMBO HILI LAKINI ANANISIHI SANA NIYAMALIZE NA BINTIYE, AISEEEEEE!! MZEE KATIA HURUMA SANA NA NINAMHESHIMU SANA YULE MZEE DAAAH!!

SASA SIELEWI LA KUFANYA NA NILISHAISET AKILI YANGU KWAMBA SIMTAKI TENA UYU MWANAMKE, KWA HAYA ANAYOFANYA LEO VIPI KESHO NA KESHO KUTWA SI ATAZIDI KUJILENGESHA HIVIHIVI, MWISHO WA SIKU BABA MTOTO AMMEGE.

KWA SITUATION HII NAOMBENI USHAURI NIFANYE NINI?

Nawasilisha..........
Hao ndugu zake, babake sijui na kakake + dadake waambiwe wazi kua ndugu yao ni Kigeugeu. Waambie bado anawasiliana na Njemba aliemzalisha na hizo Dady dady za usiku zote waambie.

Waambie wazi kua Ndugu yao anawasiliana na huyo Jamaa na anamwambia kua huku haihsi na mtu yoyote. Hivyo huwezi kuishi na Mwanamke ambae bado anawasiliana na Mtu wake. Waambie wakibisha wamuulize ndugu yao kwa upole.
 
Hao ndugu zake, babake sijui na kakake + dadake waambiwe wazi kua ndugu yao ni Kigeugeu. Waambie bado anawasiliana na Njemba aliemzalisha na hizo Dady dady za usiku zote waambie.

Waambie wazi kua Ndugu yao anawasiliana na huyo Jamaa na anamwambia kua huku haihsi na mtu yoyote. Hivyo huwezi kuishi na Mwanamke ambae bado anawasiliana na Mtu wake. Waambie wakibisha wamuulize ndugu yao kwa upole.
Tayari nimefanya hayo yote, nadhan ad sasa imeisha iyo, labda nisubir vitimbwi vingne kama vipo

Sent from my Pixel 2 XL using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma huko juu. Kama mkigombana anampigia mzaz mwenzie simu she is askin for attention. Mkogombana muombe msamaha mnunulie hata ka pipi
 
Sasa ngoja nikupe dawa. Tafuta dada poa m'moja pisi kali. Halafu huyo binti mruhusu aje. Halafu siku atayokuja ongea na yule pisi kali aje.....hakikisha siku hiyo unalamba mkongo kabisa. Then aje usiku saa tano au saa sita. Mfungulie mlango muanzie kukiss pale mlangoni, muende hadi ndani mnyooshe hadi room alipo huku mnapeana ile mibusu mizito.

Zama nae hadi kitandani sauleni nguo muanze kupeana mauno ya maana na huyo pisi kali awe anapiga ukelele wa nimpe mtoto...... Piga mashine kisawa sawa mzee usilaze damu.
 
Muache tu mkuu, atakusumbua kisa baba mtoto......

Hapa naongea Kama single mom mwenzie.

Kama huyo mwanaume anampenda Sana wachukuzane wakaishi, acha huruma kwa mtu asiyejihurumia.
Au sio....
 
Muache tu mkuu, atakusumbua kisa baba mtoto......

Hapa naongea Kama single mom mwenzie.

Kama huyo mwanaume anampenda Sana wachukuzane wakaishi, acha huruma kwa mtu asiyejihurumia.
We ni single parent sio single mother........ Rekebisha kauli....
 
Hapana kwa kweli! Hakuna Cha kuwakumbuka.

Ingekuwa ni kuhudumia mtoto hapo yangekuwa Mambo mawili.

Kama mama Hana mahusiano mapya anaweza kuwasiliana na mzazi mwenzie.

Kama yupo kwenye mahusiano/ndoa Kuna mawili ya kufanya. Huyo mzazi wa kiume awasiliane na ndugu wa mzazi mwenzie kufikisha mahitaji ya mtoto au lah, awasiliane na mume wa mzazi mwenzie kama mtoto anaishi hapo

Otherwise ni ujinga Ujinga tu wa wanawake wasiojitambua
Sijui watu wanaotafuta mke mwema wanafeli wapi kukuona.....
 
Back
Top Bottom